Pombe ina faida gani kwa Mlevi?

Pombe ina faida gani kwa Mlevi?

Mithali 23:29-35,Ni nani apigaye,Yowe? Ni nani aliaye,Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu? Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo,Waendao kutafuta divai iliyochanganyika........33 Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.34 Naam,utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.35 Utasema,"Wamenichapa wala sikuumia;Wamenipiga wala sina habari;Nitaamka lini,nitazidi kuitafuta tena".
 
wanywaji wanakuambia Pombe ni burudani... ukiwa mzoefu wa kilevi hutapenda kuwa sober!! yaani ile akili timamu, kuna raha yake kichwa kisipokuwa sawa. na ukionja kilevi tu, itafikia kipindi utaimiss ile hali ya kulewa. kama hujawahi kuonja pombe usijaribu.:rockon:
 
MLEVI NA MCHUNGAJI WAMEKUTANA;

MCHUNGAJI; "Unakunywa bia!?

MLEVI; "Ndio.

MCHUNGAJI; "Kwa siku unakunywa bia ngapi!?

MLEVI; "Nakunywa bia tano!

MCHUNGAJI; "Bia moja bei gani!?

MLEVU; "2500/

MCHUNGAJI; "Ulianza lini kunywa bia!?

MLEVI; "Miaka 18 iliyopita!

MCHUNGAJI; "Kwa hiyo kwa siku unatumia zaidi ya 10,000??

MLEVI; "Ndio!

MCHUNGAJI; "Kama u gekuwa unatunza hiyo pesa 10,000 kwa siku leo hii si ungekuwa na Range Rover!?

MLEVI; "Samahani, naweza kukuuliza swali!?

MCHUNGAJI; "Uliza!

MLEVI; "Unakunywa bia!?

MCHUNGAJI; "Hapana!

MLEVI; "Nionyeshe Range Rover yako!

MCHUNGAJI; "
 
Duh !, faida ya pombe ipo na hasara za pombe pia zipo. Kila kitu kinafaida na hasara zake, kunywa vinywaji vyenye sukari vina madhara makubwa kiafya pia unatumia pesa kununua hivyo vinywaji. Ukiwa kwenye jiji la Dar utakutana na wataalamu kibao maeneo ya stend wakieleza hatari za kutumia soda hususani coca cola, lakini huji kuwakuta wakieleza madhara ya kutumia pombe, sijajua kwanini
 
Inaongeza damu mwilini,na ikiwa unakunywa kiasi inaleta afya njema
 
Huwa nashangaa kitu kimoja, wanywa pombe wenyewe wapo kimya huwa hawazungumzii wala kuhojimambo ya watu wengine kama vile wenye tabia za kutembea na wake za watu, watumiaji wa vipodozi vikali, watumiaji wa vyakula vya viwandani ambao kila siku wanaharisha mpaka kufa, watumiaji wa soda ambao wanatoka na mavitambi waume kwa wake pia kupata magonjwa ya presha mpaka kifo,

wavuta sigara, wanunuaji malaya tena wanagonga bila condom, wambea na wasimangaji wanaoleta hali ya tafrani katika jamii. Sasa utakuta wasiokunywa pombe vielele kuhoji mambo ambayo hata hawatumii na hawajawahi kuombwa pesa za kwenda kununulia hiyo pombe. Ukitaka upate majibu vizuri nenda bar halafu waulize utapata majibu mazuri sana
 
RAHA NA KARAHA BIA YA SITA!

Kwa wanywaji wazuri wa bia, chupa ya kwanza huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo. Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.

Baada ya kumaliza chupa ya pili kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi.

Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wagonjwa wa Ebola waliopona katika nchi ya Liberia. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.

Bia ya tatu huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza.

Bia ya nne huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia, bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.

Bia ya tano ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu, na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au ‘ Mume wangu sijui yukoje hanijali’

Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.

Kuanzia bia ya sita na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo ---- na hajui kuendesha kampuni.

Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjika.
 
jaribu kunywa ujionee.... Unachokiuliza ni sawa na padre kuuliza raha ya ndoa au shekhe kuuliza utamu wa kitimoto......
 
Vikao hivi vina faida nyie acheni tu. Huku utaelekezwa shule nzuri kumpeleka mwanao, jambo la kufanya kama una kesi mahakamani, fundi ujenzi mzuri na hata mahali pa kupata kiwanja kwa bei poa. Afu kwa ujumla unaburudika...
 
mlevi na mchungaji wamekutana;

mchungaji; "unakunywa bia!?

Mlevi; "ndio.

Mchungaji; "kwa siku unakunywa bia ngapi!?

Mlevi; "nakunywa bia tano!

Mchungaji; "bia moja bei gani!?

Mlevu; "2500/

mchungaji; "ulianza lini kunywa bia!?

Mlevi; "miaka 18 iliyopita!

Mchungaji; "kwa hiyo kwa siku unatumia zaidi ya 10,000??

Mlevi; "ndio!

Mchungaji; "kama u gekuwa unatunza hiyo pesa 10,000 kwa siku leo hii si ungekuwa na range rover!?

Mlevi; "samahani, naweza kukuuliza swali!?

Mchungaji; "uliza!

Mlevi; "unakunywa bia!?

Mchungaji; "hapana!

Mlevi; "nionyeshe range rover yako!

Mchungaji; "

ha ha ha ha
 
Ukishasema walevi,hakuna faida hapo kwani mpaka uitwe mlevi,maana yake pombe s e.thing to you,ua time,money and mahusiano yako ya kijamii inckuding family yamechukuliwa na pombe,ila mara nyingi inabidi wanywe tu,maana 'alosto' ya pombe ni mbaya unaweza ukafa......
 
Eni ninyi wanawake someni hizo biblia..
Tuacheni cc wanaume tunywe bia..
 
Wenyewe wanasema inawapoteza mawazo....ila mimi naona Pombe ni chanzo cha matatizo.
 
RAHA NA KARAHA BIA YA SITA!

Kwa wanywaji wazuri wa bia, chupa ya kwanza huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo. Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.

Baada ya kumaliza chupa ya pili kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi.

Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wagonjwa wa Ebola waliopona katika nchi ya Liberia. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.

Bia ya tatu huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza.

Bia ya nne huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia, bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.

Bia ya tano ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu, na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa au Mume wangu sijui yukoje hanijali

Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.

Kuanzia bia ya sita na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo ---- na hajui kuendesha kampuni.

Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjika.
Mkuu umechambua vizuri hasa ktk paragraph mbili za mwisho.
 
Walevi ndio wanaojenga hili Taifa! hamwoni kila mwaka wa bajet wanapandisha bei ya BIERRE na fegi tu! hawapandishi condom wala carolite na super black zenye watumiaji wengi Ke/me! sie kwa umoja wetu na uungwana wetu tunasema hata wakipandisha bia moja elfu 5000 tutapandanazo! Sema vichwa vitapata moto watu watatafuta hela kwa njia mbali mbali! Anko kova itabidi ajipange sawa sawa kama Rose Muhando!
Pendekezo: Kianzishwe chama cha kutetea haki za walevi
 
Back
Top Bottom