Polycarp Cardinal Pengo azidi kutishiwa

Polycarp Cardinal Pengo azidi kutishiwa

Status
Not open for further replies.

Nikupateje

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2009
Posts
1,334
Reaction score
990
SOURCE: JIBU LA MAISHA
DATE: Sunday, May 12, 2013
ISSN: 1821-6463, No. 241
PAGE: 115
HEADLINE: ASKOFU PENGO AZIDI KUTISHIWA


- - - - - - - - -- - - - - - - - -- - - - - - - - -- - - - - - - - -- - - - - - - - -- - - - - - - - -- - - - - - - - -
Kwa matoleo kadhaa ya nyuma tumeripoti matukio ya kichochezi ya kusambazwa kwa CD na DVD zinazochochea utengano baina ya wakristo na waislamu nchini. Tumefanya hivyo kwa tahadhari kubwa na hata wakati mwingine kujitahidi kujiepusha na kuchapisha habari hizo.

Hata hivyo, tunalazimika kuripoti matukio haya ili kuzikumbusha mamlaka zenye dhamana zichukue hatua kali dhidi ya makundi haya ambayo yanaonekana moja kwa moja ni maadui wa umoja wa watanzania.

Katika kile kinachoonekana nia utaratibu maalumu, imetolewa CD mpya iliyopewa jina “Ndege wote walie akilia bundi uchuro” ambay pamoja na mambo mengine inaonyesha picha ya Askofu Kardinal Polycarp Pengo ikiwa na maandishi yanayosomeka WANTED ikiambatana na maneno makali ya kulaani Kanisa Katoliki na hata mengine, huku picha ya mtu anayechinjwa ikitumika kama logo inayojirejea kila wakati.

Juhudi za kumpata mtu anayeonekana katika DVD hiyo akitajwa kama Imam Hamza Omary, ili kufafanua ujumbe uliopo ndani ya mkanda huo hazikfanikiwa.

…

DVD hiyo ambayo JIBU LA MAISHA lina nakala yake inaonyesha mhadhiri akinukuu aya za Kuran na kuwaalika wenzake kwenye kile alichokiita Jihad (baadhi ya yale yanayosemwa hatuwezi kuyaandika kutokana na sababu za kimaadili)

Katika hilo Imam Omary anasema serikali imekuwa ikiegemea upande wa maaskofu na mabaraza yake, lakini si kwa waislamu.

Mkanda huo umeonyesha baadhi ya mazoezi makali ya vijana wa Kiislamu ingawa haionyeshi yanafanyika wapi.

Mhubiri huyo aliyashutumu pia mataifa ya kimagharibi akidai yamekuwa yakitoa silaha na kuwagombanisha wao kwa wao pasipo wenyewe kujua na hilo limeonekana kwa Saddam Hussein.

Aidha alionekana akidai kuwa jambo kubwa na la hatari kwa waislam wa sasa ni kutoongelea kabisa suala la Jihad, na hilo limekuwa donda ndugu.

Bila kupepesa maneno, Imam huyo alitaja viongozi ambao alidai eti wamekuwa wakibadili yale waliyokubaliana na waislam na wamekwenda kinyume kutokana na kutiwa msukosuko.

Vingozi na wasaniasa wanaotajwa katika DVD hiyo ni pamoja na Waziri wa mambo ya nje, Bernard Membe, Katibu Mstaafu wa CCM, Yusufu Makamba, na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Alipomaliza hilo alimgeukiwa Rais wa Uganda, Museveni na kudai yeye ni kiongozi wa Afrika Mashariki anayetaka kuhakikisha anaung’oa uislam kupitia mashehe kwa juhudi zote.

Aliyekuwa Kamanda wa Mkoa wa Mwanza, marehemu Liberatus Barlow, anatajwa kwenye mkanda huo, lakini JIBU LA MAISHA halitaongelea kilichoongelewa humo.

Yusuf Makamba ambaye ni muislam, wanadai naye mwaka 1998 akiwa Mkuu wa Mkoa Dar, wakati wao wakisema nchi inatawaliwa kwa mfumo Kristo, yeye alipinga na hilo likaonekana kuwa yuko kinyume na uislam.

Mwinjilisti Cecil Simbaulanga ambaye amekuwa akipita huku na kule kutetea wakristo ili wajue haki zao anatajwa kuwasisitiza wakristo kuchinja nyama wakati inajulikana siku zote kwamba waislamu ndiyo wenye kufanya jambo hilo hapa Tanzania.

….

Wakati hayo yakitokea, tukio la kurushwa bomu katika Kanisa la Parish of St. Joseph the Worker (Olasiti), mkoani Arusha, linarandana na maudhui ya kile kinachoelezwa kwenye mikanda kadhaa inayotolewa na watu wanaoaminika kuwa na imani kali ikionyesha chuki ya wazi dhidi na kanisa hilo.

Ndani ya DVD kadhaa zenye mlengo mmoja ambazo zimezagaa maeneo kadhaa jijini Dar, hasa maeneo ya Buguruni_Chama, inaelezwa kukamatwa kukamatwa kwa maaskofu ili kuwachinja ikiwa muislam atafanyiwa ubaya wowote au kuuliwa.
- - - - - - - - -- - - - - - - - -- - - - - - - - -- - - - - - - - -- - - - - - - - -- - - - - - - - -- - - - - - - - -
 
kazi kwa serikali ya kikwete.
Kama wanaonyesha na vijana wanafanya mazoezi basi tumekwisha.

Kwa mara nyingine namkumbuka mkapa, alikua na sauti ya kimamlaka.

Mungu tuepushe na hili janga.!
 
Mwinyi si muislam kasema kila mtu achinje na ale kile anachotaka ,tena lhaji kabisa!!sioni sababu yakugombea kuchinja wanalao jambo
 
naona Intelejensia halisi Mwalimu Julius Nyerere alikufa nayo....
wanasubiri watu wengine wafe tena ndio kamati ziuundwe watu wale pesa................. nchi si salama tena hiii.....
more worse to come....................
 
basi kama vipi itangazwe tu tulianzishe ya nini kuwindana?.........inavyoonesha huu moto hata aliyeuwasha anaogopa kuuzima!.....
 
huu ni upuuzi, watz ni watu wa aman

ni kweli mkuu yule shekhe zanzibar kumwagiwa tindikali kama saidi kubenea ni dalili za tz kuwa nchi ya amani, kuuwawa kwa padri mushi pia ni dalili ya tz kuwa nchi ya amani, hata mapigano na mauaji ya buseresere ni dalili ya amani, dalili za rasilimali kutoroshwa kama twiga pia ni dalili za tz kuwa nchi ya amani, ya mtwara na lindi pia ni dalili ya kuwepo amani, kuuwa mwangosi mbele ya polisi pia ni dalili ya tz kuwa nchi ya amani... hata cd na vile vipeperushi vya chuki kutoka kwa waislamu kuamuliwa kuwaua WAKRISTO zanzibar hata hapa dar ni dalili za nchi kuwa ya amani. asante sana mkuu una akili sana, Mungu akubariki sana.
 
basi kama vipi itangazwe tu tulianzishe ya nini kuwindana?.........inavyoonesha huu moto hata aliyeuwasha anaogopa kuuzima!.....

Kichaa umkabidhi RUNGU unategemea nini.

Nakumbuka siku moja Baba Mwadhama kadirnali PENGO alikuwa anatoa HOMILIA, akagusia amani kwa nchi za afrika alitolea mfano wa Ivory cost kwa kusema kwamba nchi hiyo zamani ilikuwa na amani ya ajabu hata tanzania haikuwahi kuifikia, lakini wale jamaa walipopata nafasi ya kupenyeza sera zao kama wanavyofanya TZ , matokeo yake ndiyo hayooooo. Sasa ni dhahiri tunaelekea huko na MELI imeshaondoka karibu inatia nanga.Hakika ni majonzi kwa ma-baba maaskofu pamoja na waumini, nawasihi tushikamane kwa kusali kufunga na kumkabidhi Mungu yote maana kwake yote YAWEZEKANA.
 
....Katika kile kinachoonekana nia utaratibu maalumu, imetolewa CD mpya
iliyopewa jina "Ndege wote walie akilia bundi
uchuro
" ambay ...... lakini si kwa waislamu.

Mkanda huo umeonyesha baadhi ya mazoezi makali ya
vijana wa Kiislamu ingawa haionyeshi yanafanyika wapi
.

Aidha alionekana akidai kuwa jambo kubwa na la hatari
kwa waislam wa sasa ni kutoongelea kabisa suala la Jihad, na hilo
limekuwa donda ndugu
.

Mwinjilisti Cecil Simbaulanga ambaye amekuwa akipita huku na kule
kutetea wakristo ili wajue haki zao anatajwa
kuwasisitiza wakristo kuchinja nyama wakati inajulikana siku zote kwamba
waislamu ndiyo wenye kufanya jambo hilo hapa Tanzania
.

…. hasa maeneo ya Buguruni_Chama,
inaelezwa kukamatwa kukamatwa kwa maaskofu ili
kuwachinja ikiwa muislam atafanyiwa ubaya wowote au kuuliwa
.
- - - - - - - - -- - - - - - - - -- - - - - - - - -- - - - - - - - -- - -
- - - - - -- - - - - - - - -- - - - - - - - -

mkuu, naona wewe unaendeleza zile sanaa zilizokataliwa na Watz wengi. tittle yako wala haijafanana na ulichoandika. huo ni uchochezi unaofanywa na watu wasiolitakia mema taifa hili kwa kuwazulia uongo waislam na kuwatengenezea cd za kizushi. alianza mbunge selasini akaja lema na sasa hizo ulizosema
 
basi kama vipi itangazwe tu
tulianzishe ya nini kuwindana?.........inavyoonesha huu moto hata
aliyeuwasha anaogopa kuuzima!.....

mkuu, hilo si jibu la matatizo yaliyopo hapa nchini. serikali ibaki kati na isiegemee upande wowote
 
Kichaa umkabidhi RUNGU unategemea nini.

Nakumbuka siku moja Baba Mwadhama kadirnali PENGO alikuwa anatoa HOMILIA, akagusia amani kwa nchi za afrika alitolea mfano wa Ivory cost kwa kusema kwamba nchi hiyo zamani ilikuwa na amani ya ajabu hata tanzania haikuwahi kuifikia, lakini wale jamaa walipopata nafasi ya kupenyeza sera zao kama wanavyofanya TZ , matokeo yake ndiyo hayooooo. Sasa ni dhahiri tunaelekea huko na MELI imeshaondoka karibu inatia nanga.Hakika ni majonzi kwa ma-baba maaskofu pamoja na waumini, nawasihi tushikamane kwa kusali kufunga na kumkabidhi Mungu yote maana kwake yote YAWEZEKANA.

Pengo ile kichwa ina akili. Ulimuelewa hapo kwenye RED. Kwani hujui Ivory Coast ndiko kule Laurent Gbagbo alipojaribu kuiba kura ikashindikana.

Kilichowezekana kule ni kwamba wapinzani walikuwa na matokeo yao kwa kila kituo, hawakusubiri kujumlishiwa na tume. NNchi yenye wapinzani ambao siku ya kupiga kura wanasubiri eti tume iwajumlishie matokeo wasahau kuiona ikulu.

Hilo ndilo fundisho tok Ivory Coast.
 
mkuu, naona wewe unaendeleza zile sanaa zilizokataliwa na watz wengi. tittle yako wala haijafanana na ulichoandika. huo ni uchochezi unaofanywa na watu wasiolitakia mema taifa hili kwa kuwazulia uongo waislam na kuwatengenezea cd za kizushi. alianza mbunge selasini akaja lema na sasa hizo ulizosema

tatizo lako unataka kukifanya CCM chama cha Waislam wakati washatukataaa zamani acha upuuzi
 
wanotoa kashfa na vitisho kwa dini nyingine serikali hii inawafahamu hakuna siri yoyote swala je ni kwa nini wachochezi hao wanaokashifu dini nyingine na kufanya wanavyotaka hawashughulikiwi?
 
mkuu, hilo si jibu la matatizo yaliyopo hapa nchini. serikali ibaki kati na isiegemee upande wowote

unajifanya unaponda selikari leo umechelewa.. .wakati kila siku unamsifu kikwete na ccm kwenye kila upumbavu
 
Natamani uchaguzi uwe kesho coz sioni kama CCM na serekali yake haya matukio kama yanawagusa moyoni na wanania ya dhati kuyakomesha zaidi ya unafki,kama unakufa(CCM) kufa mwenyewe kwa nini unataka kuangamiza taifa zima.,hii dhambi kila moja ataitolea maelezo siku ya mwisho,ni masihara kwa sababu u mzima ila siku ya kufa ndio utalia na kusaga meno..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom