Elections 2010 Poll Watch: Malecela has not lost yet

Status
Not open for further replies.
JF utawala mimi nilidhani niliwaonya sana kuhusu speculating ID za members hapa, nikadhani kwamba mmelidhibiti hilo kumbe bado lipo mpaka leo? Nyie endeleeni na huo mchezo ninaamini kwamba wengi wenu bado hamjaelewa madhara yake, tuulizeni tuwafahamishe maana kuna siku mtalia kilio cha mbwa humu mtakaporudi bongo!

FMEs!


I see.......noted!
 
Brooklyn, upinzani gani Dodoma?, samahani wana bodi, sio kuwa nataka kuleta hoja za ukabila, au umajimbo, lakini kuna baadhi ya maeneo, mwamko wa kisiasa bado ni mdogo sana, hivyo vugu vugu la upinzani liko chini sana, moja ya maeneo haya ni Dodoma na Singida, na baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kusini.

Nimefanya kautafiti kwa trend ya vuguvugu la upinzani, nikakuta ile mikoa iliokithiri kwa umasikini uliotopea, ndiko ambako huwaelewi chochote kuhusu siasa za ushindani, yoyote tuu yule atakayegawa fulana na kutoa shibe tuu japo ya siku moja kabla ya uchaguzi, huyo ndiye atakaye komba kura zote kesho yake. Dodoma ni moja ya maeneo yenye umasikini huu. Umasikini huu, haitokani na watu bali kukosekana kwa mazao ya biashara ambayo yangeinua hali za maisha ya watu. Ukiangalia wasomi wa Dodoma enzi hizo, lazima walisomeshwa na misheni vinginevyo wengelipa ada kwa fedha gani?.

Haya nimeyashuhudia Busanda, kiwango cha umasikini ni cha hali ya juu, Chadema wakafanya uhamasishaji wa hali ya juu, siku ya mwisho, wajumbe wa nyumba kumi kumi wa CCM walipeleka nusu kilo nusu kilo tuu ya sukari kwenye nyumba zao kumi kumi na kiasi kiasi cha mboga, jana yake walilalia pilau, wakaamkia kifungua kinywa hivyo wameshiba, kura wampe nani?!... na na matokeo yalibadilika.

Angalia mikoa yenye neema, Arusha, Moshi na Bukoba, walifanikiwa kutokana na kuwepo kwa zao la kahawa hivyo kuwa na fedha kusomesha watoto wao hadi kupelekea kasumba kuwa Wachagga na Wahaya wana akili sana, hapana ila tangu wazazi wao walipata hizo opportunities. maeneo haya vugu vugu la upinzani liko juu kwa sababu watu hawachukui uamuzi kufuatia shibe ya siku moja.

Kwa maeneo kama Tarime, huko ni makabila yenye msimamo usioyumba, kwa Dodoma upinzani safari bado ni ndefu, CCM itampitisha Mzee kuendelea na huyo kijana atapoozwa na ukuu wa Wilaya. Miaka mitano mingine mbona sio mbali, tatizo ni mwamko, by then mambo yaweza kuwa yameshabadilika.

NB: Hii tafiti yangu nimeifanya kwa kuangalia trend tuu, hivyo sio tafiti yakinifu yenye kufuata mising ya utafiti, no research methodoloy, I was just a 'manwatcher'


Kaka unaijua historia ya Lusinde lakini? Je makubaliano ya 2005? Je network yake sasa CCM? There is no way NEC ikambeba Mzee Malecela.

omarilyas
 
Mijitu bana.

Jana inamcheka Mwakalinga kuwa kashindwa vibaya sana na AIBU KUBWA. Leo hii mijitu iko hapa ikisema na kukiri kuwa CCM wanafanyiana Mchezo Mchafu sana. Na kesho itakuwa inalia kuwa huko Kyela, Dodoma, Dar etc CCM wamecheza mchezo mchafu.

Mkuki kwa nguruwe. Nchi inaendeshwa bila SHERIA yoyote. Rushwa kwa Wapendwa wa Chama tawala zilitawala na zilikuwa zikitolewa waziwazi. Kyela uchafu wa hali ya juu umefanywa na watu wameona waziwazi. Na baadhi yao ni hata member wa JF hapa na sasa wapo wakilaani RUSHWA ingawa na wao wamesaidia kwa hali na mali rushwa kama hizohizo kwenye majimbo ya wapendwa wao.

Bila sheria kali kuwepo na TAKURURU kulinda kwa hali ya juu na sheria kali sana na ikibidi HUKUMU YA KIFO kwa watoa na kupokea rushwa wakati wa uchaguzi, nchi yetu itaendelea KUUZWA na kununuliwa kwa watu wenye pesa zao. Kwa hali iliyopo sasa hivi Tanzania, kitamshinda nini tajiri wa Kimarekani, Kirusi, Kijep, Kichina etc kuja na kununua SERIKALI yetu nzima kwa kuweka wabunge wake? Kama Wananchi wanapenda Tshirt na Pilau, na viongozi ni mfano wetu wenyewe, basi nao wanapenda sana VYA BURE.

Tufurahie tu ndugu zetu wanaposhinda kwa kutumia UMAFIA ila siku tukija kuona nchi inaliwa na Rostam Azziz, basi nisisikie jitu la CCM likilalamika. Mlitoka kwa RUSHWA, mtarudi kwa Rushwa, jina la CCM litukuzwe, Anem.

Kwa sababu CCM imeshindwa kutibu hili GONJWA na watu mwamko bado uko chini, inabidi kupeleka mtu MAGOGONI ili afanye kusafisha kwa kiasi kikubwa RUSHWA. Mtu huyu tujiandikishe na tumsaidie kwa hali na mali na bila kutumia RUSHWA ambayo itakuja kutula tena.

WOTE TUJIANDIKISHE na kuwakumbushe ndugu, jamaa na marafiki ili TUMCHAGUE Dr. Slaa.

UKO NA MAFISADI AU UKO NA Dr. SLAA.
 
I trust Issa Michuzi -- As per Issa Malecela kashindwa -- Ron-- US

MZEE MALECELA AKUBALI MATOKEO

HABARI TOKA JIMBO LA MTERA LINASEMA MGOMBEA LIVINGSTONE LUSINDE AMEMSHINDA MH. JOHN SAMWEL MALECELA KATIKA KURA ZA MAONI NA ANATEGEMEA KUWA NDIYE ATAYEPITISHWA KUGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CCM KWA JIMBO HILO, KWA MUJIBU WA MATOKEO YALIYOTANGAZWA SAA 4 LEO


hehe heheeee!!! babu kaula wachuya! kwishney asubiri mbeleko ya Mafisadi wa NEC sasa
 
Hapana Mkuu. Uchaguzi ndiyo MSINGI wa kila nchi. Unafahamu kwenye nyumba au kila JENGO, msingi ndiyo kitu kikubwa sana na muhimu.

Ukishajenga jengo kwenye MSINGI mbovu, basi kila kitu kitaharibika. Rushwa Tanzania zinaanzia kwenye UCHAGUZI. Ukishapata viongozi walioingia kwa rushwa, basi rushwa itaenda hadi kwa karani wa ofisini. Ukiweza kuvunja RUSHWA wakati wa Uchaguzi, basi kwanza unaanza na BUNGE safi na viongozi wanaofuata sheria. Na kwa sababu wao ndiyo watunga sheria, na baadaye kuja kuwa mawaziri na hata Rais wetu ambaye ndiye huwa kuwa mteuzi wa hawa maboss wa TISS, PCCB, POLICE etc inakuwa ni wazi kuwa atachagua viongozi walio safi. Sasa kama yeye kaingia kwa Hongo na anafahamu kuwa miaka 5 ijayo itakuwa rahisi kwake kuingia kwa Hongo, unafikiri atangaika kufanya kazi? Unafikiri atatunga sheria zitakazombana yeye? Unafikiri atasimama na kukamata wala Rushwa?

Uchaguzi ni MWISHO kabisa wa MNYORORO wa ile hadithi ya KARUMEKENGE. Tukichagua viongozi bila ya rushwa kwa watu kuogopa hukumu ya kifo, basi tutaendela kuwa na Rais asiyependa hongo, Bunge lisilopenda hongo, sheria zisizopendelea rushwa, Mawaziri wasiopenda rushwa, ma DC, Polisi, Takururu, maofisa wa serikali nk nk wasiopenda/wanaoogopa rushwa kwa kufahamu HUKUMU YAKE NI MBAYA SANA.

Kama wewe hilo hulioni na unaona kuwa nimeandika kwa sababu MWAKALINGA kashindwa, nazidi tu kuamini kuwa Tanzania tuna safari ndefu sana kuondoa RUSHWA. Na nitakumbuka hayo maneno yako kila siku. Nikija kuona sehemu unalaani RUSHWA, ntakupa swali kama hilohilo. Nikiona mtu analaani RUSHWA, itabidi nikupe swali kama jamaa na yeye anaandika kwa sababu Mwakalinga kashindwa.

Kesi ya Mwakalinga hapa si muhimu sana. Soma sahihi yangu ndiyo utafahamu lengo langu la mwaka huu ni nini.

UKO na SLAA AU UKO NA MAFISADI. Nyambala, uko wapi??????

Mkuu haya maneno ni baada ya Mwakalinga kushindwa au?
 
Hivi kuna aliyekuwa akicheza na ID za watu humu kama FMES hasa tuliowahi kutofatiana naye katika hoja mbalimbali humu? Tusijisahau, humu tunaandika na akina Invisible hawayafuti maandishi haya. Humu ni zaidi ya Hansard ya Bunge letu.
Turudi kwenye hoja. Mzee JSM sio mtu wa kukata tamaa na wala hii sio mara yake ya kwanza kuanguka. Atanyanyuka tu. Ikishindikana kabisa JK amkumbuke kwenye jimbo lake la IKULU endapo vikao vya juu vya CCM vitashindwa kumuengua dogo Lusinde.
Mkuu vipi bana! after october mwenye kuteua wabunge wa jimbo la Ikulu ni Dr, umesahau nini! tehe tehe tehe! Jamaa si apumzike tuu, maana nasikia jamaa hata mshiko anao wa kutosha.
 
FMES;

Lkn hii ya Mzee maarufu kisiasa kama Malecela kusubiri hadi kura ya mwisho ihesabiwe ndiyo atangazwe mshindi,wewe kama mtu wa karibu wa Mzee huyu hali hii unaichukuliaje kwake kisiasa?

Kama kafanya vyema kwa wapiga kura wake wa Mtera wakiwemo wana CCM wenzake why isiwe kama wenzake akina Sitta,Sendeka,Mama Kilango au Lembeli ambao mara tu baada ya"exit polls"wafuasi wao walijimwaga barabarani kushangalia ushindi wao?

Mzee Malecela kawakosea nini wana CCM-Mtera hadi wakamsulubu kiasi hiki,pengine vibaya zaidi hata kuliko ya mwaka 1985 alipoangushwa na "mzee mwenzake"fundi bomba Yohana Mazengo kwenye ubunge jimbo la Chilonwa?

Why mwanasiasa Chipukizi kama Lusinde amsumbue Mzee Tingatinga kiasi hiki?Kakosea wapi Mzee wetu Cigweyemis?

.........hayo hapo juu ndio maswali muhimu ya kujiuliza.........na wajuvi wa nyakati huyaona haya hata kabla hayajatokea..........?
 
UKO na SLAA AU UKO NA MAFISADI. Nyambala, uko wapi??????

Msimamo wangu siku zote uko pale pale.............................. i have neva voted for CCM and neva will.
 
'Kenyewe' kamesema bajaji kaangusha tingatinga!

Kwa umahiri wa rafu za kisiasa za Mzee JSM isingewesekana ashindwe kimizengwe; he's so smart for that. Mzee akubali tu kwamba ndiyo hivyo tena. Ambacho anatakiwa ajutie ni kushindwa kusoma alama za nyakati. Angefuata ushauri wa Mzindakaya, haya yasingemkuta. Sasa anaondoka katika siasa disgracefully! Poleni sana wahusika wote
 
Lusinde and the "Machine" at this point wanajaribu sana kubadili kura za kata mbili, nazo ni LOJE na CHINOBOLI ili watangaze rasmi ushindi wa dogo, lakini kuna watoto wa Malecela on the scene na hasa katika kuhesabu kura hizo who are making it difficult, bado kuna kamchezo kanaendelea what a rollercoster! Haters poleni sana, ila JF haiamui nani awe mshindi.

JF utawala mimi nilidhani niliwaonya sana kuhusu speculating ID za members hapa, nikadhani kwamba mmelidhibiti hilo kumbe bado lipo mpaka leo? Nyie endeleeni na huo mchezo ninaamini kwamba wengi wenu bado hamjaelewa madhara yake, tuulizeni tuwafahamishe maana kuna siku mtalia kilio cha mbwa humu mtakaporudi bongo!

FMEs!
Mkuu Fmes, Posts zako zimekuwa zinaleta mwamko mkubwa wa watu kuja hapa jamvini mara kwa mara na hilo lita thihirishwa na siku za karibuni ulipokuwa haupo hapa kumekuwa na mpoozo wa aina fulani.

Naomba usitukimbie hata kama kuna mambo ambayo haya kufuhishi ni vizuri ukayaweka bayana hapa tujaribu kuyatafutia uvumbuzi

Mods, kwenye hile thread ya wana jamiiforum kutinga bunge kuna watu waliongelea kuna mtu alikuwa ana reveal ID za members, majibu yenu hayakuwa NDIYO au HAPANA-kama kuna mtu kafanya hivyo au hakuna kitu kama hicho.Sasa Mkuu wetu naye anaongelea speculating ID za members ingawa kwa upande wangu nimwelewa tofauti alipoendelea "maana kuna siku mtalia kilio cha mbwa mtakaporudi bongo" hii ni zaidi ya kukisia ID z za members.

Ni vizuri kuweka ugonjwa wazi ukatibiwa hata kama utakimbiwa na baadhi ya marafiki kuliko kuficha na bila kusahau "Where We Dare To Talk Openly" au hii dhana inatumika pale tunapojadili watu wengine.

Chonde chonde Mods wekeni hili jambo wazi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom