Elections 2010 Poll Watch: Malecela has not lost yet

Status
Not open for further replies.
Well latest ni kwamba Lusinde boy and the machine wana a big media team ambao wanatangaza ushindi wake toka jana bila kujali matokeo on the ground, jana usiku they almost changed matokeo ya kata moja ya Loje, lakini msimamizi akapigana to end, what Lusinde and the machine are doing ni kutengeneza mazingara ya kuibiwa ushindi, anyways this is my last comment maana nimesikitishwa sana na huu mchezo wa speculation of members ID, kwa hili JF utawala mmenisikitisha sana kumbe halijaeleweka bado!

Kwa herini ya kutoonana tena!

Es!

Du hii kali
 
Malecela won by 245 votes, Message delivered by Lusinde Boy no question about it na imefika, may be it is time to hang up now and pick up someone who will carry on the torch, just thinking loudly!

Well latest ni kwamba Lusinde boy and the machine wana a big media team ambao wanatangaza ushindi wake toka jana bila kujali matokeo on the ground, jana usiku they almost changed matokeo ya kata moja ya Loje, lakini msimamizi akapigana to end, what Lusinde and the machine are doing ni kutengeneza mazingara ya kuibiwa ushindi

Hii habari mbona haieleweki?????????
 
Breaking news: Lusind a.k.a The utamu amshinda Malecela a.k.a Tingatinga. " Hallow Anne! wameniibia kura mafisadi hah hah hah hah! but worry not wewe umeshinda hah hah hah!"
 
Hivi kuna aliyekuwa akicheza na ID za watu humu kama FMES hasa tuliowahi kutofatiana naye katika hoja mbalimbali humu? Tusijisahau, humu tunaandika na akina Invisible hawayafuti maandishi haya. Humu ni zaidi ya Hansard ya Bunge letu.
Turudi kwenye hoja. Mzee JSM sio mtu wa kukata tamaa na wala hii sio mara yake ya kwanza kuanguka. Atanyanyuka tu. Ikishindikana kabisa JK amkumbuke kwenye jimbo lake la IKULU endapo vikao vya juu vya CCM vitashindwa kumuengua dogo Lusinde.
 
Duh hii kali ya mwaka Tinga tinga alizoea kucheza rafu mara kibao dhidi ya wapinzani hadi akalikwaa jina la Tinga toinga.Ikiwa ni kweli kijana mdogo na mchanga kisiasa Bwana Lusinde kamchezea rafu kwangu mimi naona sawa mkuki mtamu kawa Nguruwe kwa binadamu mchungu.

Wapinzani jaribuni kujipanga sawa sawa uchaguzi mkuu 2010 utakuwa na rafu kibao sitapenda kusikia mkilia kama watoto wadogo jaribuni kuungana muunganishe nguvu zenu kuepuka kugawa kura,uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 majimbo ya uchaguzi ya Arusha na Moshi vijijini na mengine kibao wapinzani walishinda kilichotokea ni kugawana kura na kuruhusu CCM kuendelea kupeta.
 
Huyu mzee si apumuzike tu, nilishawahi kuandika kuwa atakuja kuondolewa kwa aibu. Ningekuwa mimi Malecela hata kama nitashinda kwa tofauti ya kura 100 ningeachia ngazi ni aibu kwa mtu aliyewahi kuwa PM kubishania tofauti ya kura 20, ilitakiwa kwa mtu kama yeye kama si kupita bila kupingwa amuache mpinzani wake kwa mbali sana.

Ila najua CCM hawatafanya kosa kumuacha huyu mzee kwenye mataa itafanya kila liwezekanalo apite hata kwa mbeleko, maana wanajua kupoteza tingatinga hili ni hatari hasa kwa uchaguzi wa mwaka huu. Ni bora wamumwage Lusinde kwa sababu wanaweza kumuahidi hata u-DC kuliko kummwaga Malecela kwa vile sijui kama malecela anaweza kuahidiwa u-DC au u-RC akakubali.
 
Siamini kwa nguvu aliyonayo Mzee Malecela ndani ya Chama na Serilkali kwa ujumla kama kweli angekuwa ameshinda...kuna mtu angethubutu kucheza rafu????

Kama ndivyo....je itakuwaje October 30 pale ambapo mgombea wa upinzani ataongoza dhidi ya Mzee Malecela????
Brooklyn, upinzani gani Dodoma?, samahani wana bodi, sio kuwa nataka kuleta hoja za ukabila, au umajimbo, lakini kuna baadhi ya maeneo, mwamko wa kisiasa bado ni mdogo sana, hivyo vugu vugu la upinzani liko chini sana, moja ya maeneo haya ni Dodoma na Singida, na baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kusini.

Nimefanya kautafiti kwa trend ya vuguvugu la upinzani, nikakuta ile mikoa iliokithiri kwa umasikini uliotopea, ndiko ambako huwaelewi chochote kuhusu siasa za ushindani, yoyote tuu yule atakayegawa fulana na kutoa shibe tuu japo ya siku moja kabla ya uchaguzi, huyo ndiye atakaye komba kura zote kesho yake. Dodoma ni moja ya maeneo yenye umasikini huu. Umasikini huu, haitokani na watu bali kukosekana kwa mazao ya biashara ambayo yangeinua hali za maisha ya watu. Ukiangalia wasomi wa Dodoma enzi hizo, lazima walisomeshwa na misheni vinginevyo wengelipa ada kwa fedha gani?.

Haya nimeyashuhudia Busanda, kiwango cha umasikini ni cha hali ya juu, Chadema wakafanya uhamasishaji wa hali ya juu, siku ya mwisho, wajumbe wa nyumba kumi kumi wa CCM walipeleka nusu kilo nusu kilo tuu ya sukari kwenye nyumba zao kumi kumi na kiasi kiasi cha mboga, jana yake walilalia pilau, wakaamkia kifungua kinywa hivyo wameshiba, kura wampe nani?!... na na matokeo yalibadilika.

Angalia mikoa yenye neema, Arusha, Moshi na Bukoba, walifanikiwa kutokana na kuwepo kwa zao la kahawa hivyo kuwa na fedha kusomesha watoto wao hadi kupelekea kasumba kuwa Wachagga na Wahaya wana akili sana, hapana ila tangu wazazi wao walipata hizo opportunities. maeneo haya vugu vugu la upinzani liko juu kwa sababu watu hawachukui uamuzi kufuatia shibe ya siku moja.

Kwa maeneo kama Tarime, huko ni makabila yenye msimamo usioyumba, kwa Dodoma upinzani safari bado ni ndefu, CCM itampitisha Mzee kuendelea na huyo kijana atapoozwa na ukuu wa Wilaya. Miaka mitano mingine mbona sio mbali, tatizo ni mwamko, by then mambo yaweza kuwa yameshabadilika.

NB: Hii tafiti yangu nimeifanya kwa kuangalia trend tuu, hivyo sio tafiti yakinifu yenye kufuata mising ya utafiti, no research methodoloy, I was just a 'manwatcher'
 
mambo ya ccm hayo.............wao tu wapo chungu kimoja na hawapikiki...je pale october si itakuwa vurugu?????????????????????
 
Hizi ID zaidi ya moja zinachekesha sana!!! Lakini kwa nini huyo babu hapumziki? Yaani wanataka wafe na tai ya ubunge au uongozi shingoni? Pumzikeni, uzeee huo!!! Kwa nini mnatafuta aibu kwa vijana??? Nimefurahi kuwa majimbo mengi yamebwaga wazee chini!
 
Well latest ni kwamba Lusinde boy and the machine wana a big media team ambao wanatangaza ushindi wake toka jana bila kujali matokeo on the ground, jana usiku they almost changed matokeo ya kata moja ya Loje, lakini msimamizi akapigana to end, what Lusinde and the machine are doing ni kutengeneza mazingara ya kuibiwa ushindi, anyways this is my last comment maana nimesikitishwa sana na huu mchezo wa speculation of members ID, kwa hili JF utawala mmenisikitisha sana kumbe halijaeleweka bado!

Kwa herini ya kutoonana tena!

Es!

FMES! Kubali kushindwa - Maisha ndivyo yalivyo!

Well 35 years nadhani ni muda muafaka wa Tingax2 to say Kwaheri ya kutoonana (Right?)

either ni " the machine" or "the conveyor belt" TingaX2 should go! (Aaargh)
 
Unataka kusema na Slaa naye aishie? Maana miaka kibao ananing'inia bungeni wakati kuna vijana kibao wenye damu changa na brain ya kasi wako nyuma yake!
 
Unataka kusema na Slaa naye aishie? Maana miaka kibao ananing'inia bungeni wakati kuna vijana kibao wenye damu changa na brain ya kasi wako nyuma yake!

Hapa naongelea umri na role played in politics so far

John S. Malecela (76) v/s Dr W. Slaa (68)?

Kama JSM alideclare umri wake vizuri anamzidi WS karibia miaka 10!
 
FMES! Kubali kushindwa - Maisha ndivyo yalivyo!

Well 35 years nadhani ni muda muafaka wa Tingax2 to say Kwaheri ya kutoonana (Right?)

either ni " the machine" or "the conveyor belt" TingaX2 should go! (Aaargh)
Baba_Enock, kukubali sio lazima kusema ndiyo, kitendo tuu cha kukaa kimya na kuaga kwa heri ya kutoonana, ni jibu tosha.
Ukweli ni kuwa Mzee wetu huyu ameshindwa. Matokeo yametangazwa sasa hivi kwenye taarifa ya habari ya SAA 7 mchana TBC.

Mjadala kama ameshindwa au hajashindwa, ufungwe kusubiri uamuzi wa NEC ya CCM kama utaridhia au utamjinjia baharini kijana Lusinde, akafie mbele!.
 
Huyu mzee si apumuzike tu, nilishawahi kuandika kuwa atakuja kuondolewa kwa aibu. Ningekuwa mimi Malecela hata kama nitashinda kwa tofauti ya kura 100 ningeachia ngazi ni aibu kwa mtu aliyewahi kuwa PM kubishania tofauti ya kura 20, ilitakiwa kwa mtu kama yeye kama si kupita bila kupingwa amuache mpinzani wake kwa mbali sana.

Ila najua CCM hawatafanya kosa kumuacha huyu mzee kwenye mataa itafanya kila liwezekanalo apite hata kwa mbeleko, maana wanajua kupoteza tingatinga hili ni hatari hasa kwa uchaguzi wa mwaka huu. Ni bora wamumwage Lusinde kwa sababu wanaweza kumuahidi hata u-DC kuliko kummwaga Malecela kwa vile sijui kama malecela anaweza kuahidiwa u-DC au u-RC akakubali.

Vya nini vyote hivyo kwa umri wake akae apumzike ale matunda ya pension yake na kushughulika na kilimo kwanza, haitajiki tena kwenye kipindi cha dot com
 
Its time to pack and go Mzee Malecela, aibu kubwa hii....angesoma alama za nyakati akaachana na siasa kwa heshima kubwa. Wezi wanapokutana huo ni mchezo wa hatari, kijana Lusinde anajua mbinu chafu na mzee JSM amepita humo humo mzee wa watu chali. Malecela legacy is in turmoil
 
I trust Issa Michuzi -- As per Issa Malecela kashindwa -- Ron-- US

MZEE MALECELA AKUBALI MATOKEO

HABARI TOKA JIMBO LA MTERA LINASEMA MGOMBEA LIVINGSTONE LUSINDE AMEMSHINDA MH. JOHN SAMWEL MALECELA KATIKA KURA ZA MAONI NA ANATEGEMEA KUWA NDIYE ATAYEPITISHWA KUGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CCM KWA JIMBO HILO, KWA MUJIBU WA MATOKEO YALIYOTANGAZWA SAA 4 LEO
 
Malecela won by 245 votes, Message delivered by Lusinde Boy no question about it na imefika, may be it is time to hang up now and pick up someone who will carry on the torch, just thinking loudly!

Kwa heri ya kuonana tena!

FMEs!

Enheee?????
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom