Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Muammar Gaddafi vs Nelson Mandela? Nani shujaa/mwamba wa Afrika?


  • Total voters
    237
Mandela nasikia wazungu walimnyongonyesha kwa kumuonesha gerezani kila aliyekuwa nae bega kwa bega kuwa amewafuata wazungu walimfanyia hivyo mpaka anatoka alikuwa anaona hakuna mtu wa kuitetea afrika ,
alipopata madaraka akaamua kuwashirikisha hao hao wazungu bila kinyongo.
gadafi alitumia sehemu ya utajiru wake kuikomboa afrika(alijaribu lkn hakuweza)
 
junky,

..mchango wa Gaddafi kwa vyama vya ukombozi vya kusini mwa afrika unaweza kuulinganisha na mchango uliotolewa na nchi kama Nigeria na Algeria?

..nimewahi kusoma kwamba Nigeria inapewa heshima kama nchi za mstari wa mbele kutokana na msaada mkubwa walikuwa wakiutoa kwa vyama vya ukombozi.

..binafsi nikikwama ktk habari kama hizi huwa nawatafuta Shwari, Companero, au nguruvi kwa msaada.
 
..Gadaffi huyu aliyeua askari wetu wakati wa vita vya Uganda?!

..vijana wa siku hizi hebu someni kidogo.

..manaake mnaaibisha kwa kuanzisha thread kama hizi.
Hata Mwalimu alikuwa na mapungufu yake, hakuna asiyekuwa na mapungufu. Mbona huyohuyo Gadafi alikuwa akishutumiwa kuwaunga mkono makundi ya kigaidi mengi tu?

Binafsi kati ya Mandela na gadaffi naona Gadaffi ni shuja kabisa.
 
Baba Madiba hana wakufananishwa naye hapa duniani.
Madiba na Hayati Nyerere naona ni kama mbingu na ardhi. Watu naona hamjui kuwa mpaka leo SA kuna ubaguzi, bado kuna mitaa ya ngozi nyeupe na nyeusi, nchi bado inatawaliwa na wazungu.

Madiba alivyotoka jera biashara yake iliishia hapo hapo, waliamua kumzawadia heshima tu ili atulia lakini kiutendaji, achana na Nyerere na Gadaffi.
 
Gaddafi alijitahidi sana kusaidia Africa, sema ndio hivyo baadae wakubwa waliona ni kikwazo kwa maslai yao! Mandela alipata zaidi umaarufu hasa kwa msamaha wake kwa makaburu licha ya kuwekwa jela kwa miaka kibao! Kwangu mimi Gaddafi ni zaidi ya Mandela
 
Wote in mashujaa kwa kazi walizozifanya.
Huwezi kusema kati ya aliyepata A ya Biology na aliyepata A ya Hisabati ni nani msomi zaidi?
 
1) gaddafi ni shujaa anaejielewa na alikuwa na msimamo mmoja juu ya wanyonyaji wake,anaongea anachohisi na ukweli mtupu.alikuwa analijua tatizo la afrika na akadhamiria kuikomboa africa yote kwa vitendo. alikuwa hatoi kauli dhaifu za hekma kwenye kupambana na unyonyaji wa afrika yetu.
2) mandela alikuja kufanywa mwanasiasa akawa anaongea kisanii na kisiasa kama anavyotarajiwa kuongea ili apendeze kwa wanyonyaji wake kama kawaida yetu waafrica,hotuba za busara na hekma zilizompa u-star alikuwa akiandikiwa na makaburu ili kulevya watu wake na waafrika kwa jumla, ndio mana afrika ni shamba la bibi, wamiliki wake hawapo africa
 
Pamoja na hayo, huwezi kufuta historia aliyoiandika. Ww hupaswi kumchukia, kila vita ina upande c.o lazima akae upande wako.
 
Madiba na Hayati Nyerere naona ni kama mbingu na ardhi. Watu naona hamjui kuwa mpaka leo SA kuna ubaguzi, bado kuna mitaa ya ngozi nyeupe na nyeusi, nchi bado inatawaliwa na wazungu.

Madiba alivyotoka jera biashara yake iliishia hapo hapo, waliamua kumzawadia heshima tu ili atulia lakini kiutendaji, achana na Nyerere na Gadaffi.
Mkuu kwa Madiba hata kwa fimbo huwezi kunitoa yule mzee Mungu alimleta duniani kuja kuikomboa S.A, hata wakimbizi wakati anaumwa walikuwa wanalia sana, kazi yake alishamaliza wakina Zuma ndiyo wanaiharibu S.A.
 
Back
Top Bottom