Politics of hate in Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Politics of hate in Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Nov 11, 2009.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Lets face it matajiri ndio walipa kodi wakubwa na kwa hali jinsi inavyoelekea inasemekana kuwa kule TRA japo kila kukicha tunapewa stats kuonyesha kuwa kodi zimeongezeka alakini ukweli ni kuwa hizi politics of HATE na VENDETTA zinazoendelea hapa zinatisha watu

  Najua kuna jamaa alifanya kazi yake nzuri akapa kamisheni kama dola milioni 5 lakini anaogopa hata kununua Yatch kisa ataambiwa FISADI, mtu haendeshi Vogue mjini ataambiwa ohhh PESA ZA EPA hizo!

  Na wanasiasa kama akina PINDA kuwaatisha wenzao wasivae suti ndio mbaya kabisa

  Tatizo langu ni la system ya wanasiasa iliyooza na wala si hawa matajiri maana kusema tutarudi enzi za UJAMAA tunajidanganya...na hawa ma investors hawaweza kuja Tanzania kama mnawapiga vita kila kukicha

  If anything walio mafisadi ni wanasiasa na vyombo vya kukusanya kodi kama TRA na si matajiri


  Tazameni hawa ma oil executives na watu walio na nafasi zao wanacvyojipumzisha kule ABUJA Nigeria..


  Hivi mnajua kama Mozambique inaongoza kwa kupoach investers waliokuja Tanzania?

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  [​IMG][​IMG]

  [​IMG][​IMG]
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu Ubuja hakuna mafuta... Ni mji uliojengwa kama Dodoma kwa ajili ya makao makuu na nilivyosiikia idea hiyo mwalimu aliitoa kwao.
  Si ajabu hao ngozi ya **** unaowaona hapo wakicheza ni wabunge, lakini wengine wote ni wabeba mizigo..Na kibaya zaidi moja ya picha yako inaonyesha wazungu wakipata kinywaji Miafrika ikitazama kwa uchu, hakuna karibu hapo!

  By the way tujikumbushe tu na ukweli bayana kuhusu Nigeria, kisha wapime nasi...(mbingu na ardhi)

  1. Nigeria is ranked 37th in the world in terms of GDP (PPP) as of 2007.
  2.Nigeria is the United States' largest trading partner in sub-Saharan Africa and supplies a fifth of its oil (11% of oil imports). It has the seventh-largest trade surplus with the U.S. of any country worldwide.
  3. Nigeria is currently the 50th-largest export market for U.S. goods and the 14th-largest exporter of goods to the U.S.
  4. The United States is the country's largest foreign investor.The bulk of economic activity is centred in 4 main cities: Lagos, Kaduna, Port Harcourt, and Abuja. Beyond these three economic centers, development is marginal
   
 3. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Game Theory,
  Matajiri ndio wakwepa kodi wakubwa hasa katika nchi zetu hizi ambazo uadilifu haupo! Investors wanaokuja Tanzania ni wale wanaojua kwamba huku kuna utajiri wa bwete. Wanakuja Tanzania kuchimba madini na mwisho wa siku watatuachia mashimo tutakuwa hatuna chochote cha maana tulichoambulia. Wengine wanakuja kujenga mahoteli ama kuanzisha biashara zenye muda wa msamaha wa kodi na muda huo ukiisha hubadilisha majina ili kukwepa kulipa kodi. Wengine ni wale wanaokwenda kwenye mbuga za wanyama na kuwinda ama kuchukua wanyama wazima wazima kuwapakia kwenye ndege kwa kificho usiku usiku na kuwapeleka kwao. Sasa wamefika mahali wameona ni bora wajenge mahoteli makubwa katikati ya mbuna na uwanja wa ndege kwenye mbuga za wanyama ili waweze kuwahamisha kwa urahisi zaidi! Na kutokana na ujenzi huo na madege yakianza kutua na kuruka, kwa vyovyote vile wanyapori watatishika na kukimbilia nchi jirani. Baada ya muda Tanzania tutakuwa hatuna tena mbuga za wanyama za kujivunia.

  Wawekezaji wanakimbilia Msumbiji bila shaka huko nako wameshanusa na kuona kuna ubwete fulani. Hakuna mwekezaji ambaye anakuja kuwekeza akiwaza maslahi ya nchi na wananchi katika nchi anayowekeza. Mwekezaji siku zote anawaza maslahi yake binafsi. Kwa ujinga wetu tunajidanganya na kudhani kwamba kuwa na Wawekezaji ndani ya nchi ndiyo dawa ya kukuza uchumi wetu.

  GT, Ujamaa unaosema hautarudi tena ulibeba msingi bora wa maendeleo - KUJITEGEMEA. Hao Wawekezaji tunaowalilia usiku na mchana kwamba ndio muarubaini wa maendeleo yetu kiuchumi wao kwao WANAJITEGEMEA. Siasa wanazofuata hata kama sio za Ujamaa lakini ni za KUJITEGEMEA na si kuwa tegemezi. Kwa nini sisi tulilie Wawekezaji badala ya kutafuta mbinu na njia zitakazotufikisha katika KUJITEGEMEA kama wao?

  Waziri Mkuu Pinda tunambeza kwa kusema watu wavae nguo zinazotengenezwa nchini badala ya kuvaa suti za bei mbaya kutoka nje. Lakini nchi za Asia ambao huko nyuma walikuwa maskini kama sisi leo hii uchumi wao umekuwa kwa sababu ya kutumia zaidi vitu vilivyotengenezwa ndani ya nchi badala ya kutumia fedha za kigeni kununua vitu hivyo kutoka nje. Ndilo darasa alilojaribu kulitoa Pinda lakini badala ya watu kuelewa mantiki yake wanamsakama kwamba anazuia bila sababu watu kuvaa suti!

  Mpaka hapo tutakapobadilika vichwani mwetu na kuamua kwa makusudi kutengeneza na kutumia vyetu hapo ndipo tutakapoyaona maendeleo ya kweli. Hizi takataka zinazotoka Uchina na kujazwa madukani kuanzia nguo hadi vifaa mbalimbali vya majumbani, maofisini na hata ma-toy ya kuchezea watoto, jhivi kweli vitu vya aina hiyo haviwezi kutengenezwa ndani ya nchi yetu?

  Yupo Mtanzania mwenye asili ya Kiasia aliwahi kuniambia kwamba Wahindi walioondoka Tanzania kukimbia purukushani za siasa ya Ujamaa na kuhamia Uingereza na Canada hivi sasa ndio wanaoshikilia uchumi wa nchi hizo! Tanzania hivi sasa tunao Wahindi matajiri ambao wanatengeneza fedha humu nchini na kuzipeleka kwenye makampuni yao nje ya nchi, wanaweza kuonyesha uzalendo kwa nchi kwa kujenga viwanda vya kutengeneza humuhumu nchini vitu vyote vinavyotoka Uchina. Naamini Wahindi hao na matajiri wengine 'wazawa' wakihamasishwa wakatakiwa kufanya hivyo wanaweza kufanya.

  Naipenda sana slogan ya Mwalimu Nyerere ya 'TANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO!' Wenye moyo wapo, wanahitaji kuhamasishwa. Watakapotokea wahamasishaji waadilifu na wakweli kwenye Siasa Tanzania inaweza kupiga u-turn ya nguvu na ya maana na hata ufisadi unaweza kutoweka na kuwa simulizi ya yaliyopita si ndwele.
   
 4. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  GT picha ni nzuri nakubali. Hasa hao warembo wa mwanzoni. Hivi nao ni oil executives? Mimi nadhani ni vimada tu. Je, kwa hao wazungu kucheza golf Abuja ni ushahid kuwa Nigeria inafaidika na uwekezaji? Picha yenyewe inaongea kinyume. Wapo wamatumbi wachache labda ndiyo hao wanaoiba mapato yanayotokana na mafuta na kuiacha nchi katika umaskini licha ya kuwa na mafuta. Nigeria ni kichekeshao ukiilinganisha na nchi za ghuba ya arabuni na nchi kama Libya. Ufisadi huo ndiyo umesababisha umaskini uliokithiri katika eneo la Kusini Mashariki wa Nigeria linalozalisha mafuta na kuwalazimisha vijana wa huko kuchukua silaha ili kutetea maslahi yao. Wawekezaji hasa wazungu si dawa ya umasikini wetu. Dawa ni uwekezaji wenye akili. Libya haina wawekezaji kutoka Magharibi lakini wamepiga hatua kutuzidi kupitia uwekezaji wa ndani (ukiacha mbali kelele na ulaghai unaondeshwa na vyombo vya habari vya Magharibi dhidi ya nchi hiyo). Wawekezaji ndiyo walipa kodi wakubwa? You are joking!
   
 5. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  GT,
  Nilikuwa sijaziona picha zote. Haya ndiyo maendeleo yanayoletwa na wawekezaji sambamba na watoto wa Kiafrika popote pale wanaokufa kila siku kwa utapia mlo na kukosa huduma za afya?!
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi Lowassa analipa kiasi gani cha kodi kwa mimali yote aliyo nayo Tanzania? Jeetu Patel analipa kiasi gani cha kodi? Manji, Rostum, na orodha ni ndefu tu hawa wanalipa kiasi gani cha kodi?
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,532
  Likes Received: 81,945
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jasusi, haya ndiyo yale tunayosema ukistaajabu ya Mussa...... Huyo fisadi Papa Rostam alikuwa hachelewi kwenda kukinga mkono pale hazina ili alipwe malipo yake kwa siku kutokana na mkataba wake Richmond/Dowans lakini wakati huo huo hakuona umuhimu wa kulipa kodi zake! halafu leo tunaambiwa matajiri ndiyo wanaolipa kodi kubwa Tanzania na wakati tunajua kwamba wanatafuta kila sababu na mianya iliyopo hata kuhonga ili kutolipa their fair share to our society
   
 8. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #8
  Nov 12, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Lazima iwepo punitive taxation system,I forget the technical name for it. Makampuni lazima yatozwe kodi mpaka mengine yaanze kufilisika,kwa ajili ya kodi,na yafunge kazi,ili Serkali iweze kufahamu kwamba kodi zinatozwa ambazo ni kwa faida ya wananchi.
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  GT Huyo rafiki yako aliyepata commission ya hayo mahela amefanya kazi gani kama sio kuinflate bei za hayo manyumba wanayojenga kutumia hela za pension za wafanyakazi; lazima aogope kuzitumia kwani ni mwizi!! Na sasa mnatumia udini kama kinga yenu ya kutuibia; ole wenu huyu jamaa yenu akiondoka mtajitambua!!
   
 10. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  huku hao oil executive waki enjoy their tax free status, delta watu wanalipua pipe kwa ajili hela ya mafuta haileti maendeleo. nigeria ni nchi inayoongoza kwa ku-kidnap oil workers duniani.
  na hao oil workers wakienda nigeria wanasema nigeria ni high risk kwa hiyo wana demand high pay ambayo licha ya kuwa juu kulikoni other oil producing countries pia ni tax free.

  hiyo oil inawafaidisha wachache
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Nov 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakacheze hiyo Golf huko Delta ndipo tutajua kweli huko hakuna hiyo HATE...Hizi picha kama zingekuwa zimelenga Utalii na kuonyesha jinsi wazungu wanavyokuja cheza Golf (mvuto wa golf ktk Utalii)..hapo ingekuwa deal lakini kujipumzisha baada ya wizi..
  GT, Mkuu wangu kama ni swala la kujirusha tu, Je, umewahi kwenda Mwadui Diamonds hata siku moja! jaribu fika pale na uone jinsi jamaa hao walivyojirusha toka enzi ya mwalimu..enzi zile team ya Mpira ya Mwadui walikuwa wakiruka na jet yao..
   
 12. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #12
  Nov 13, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Highly suggestive!
  to summarily brand 'Politics of Hate in Tanzania' to have anything to do with taxes- my brotha- is highly suggestive.

  There has been a few articles, posts, even threads that have the same mantra, the only difference they have dubbed "" divisive politics, class wars, mtandao etc... surely no taxes were involved!

  Watch what your planting, yanaweza kuota magugu.
   
 13. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #13
  Nov 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama kuna politics za hate and vendetta. Nachokiona ni kuwa kuna wafanyabiashara ambao wamekuwa ni wavunaji wakubwa wa yale wasiyopanda, kwa kutumia siasa, ndio wanaona wanapigwa vita baada ya watu kuanza kugundua hila zao. Na kama mpango ulikuwa ni kuiga mitindo ya kule Nigeria kama mtoa mada anavyoonyesha, where watu wachache wanakula karibu kila kitu wanaacha majority wanapata shida basi ajue lile tatizo la Niger Delta ambalo linakataa kufa kwa ujanja ujanja wa watu hao wachache , linaweza pia kutokea hata hapa kwetu.
  Mi naona dawa ni kuacha biashara za utapeli na wizi wa mali za walipa kodi ili heshima iwepo na inshallah watu wengi tuwe na uwezo wa kwenda kwenye hizo golf course.
  Mkubwa GT, sikio la kufa kumbe kweli halisikii dawa!!
   
 14. B

  Boca1 Member

  #14
  Nov 13, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ebwanayeeeeee umempa data
   
 15. B

  Boca1 Member

  #15
  Nov 13, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  GT
  Nina wasiwasi na ufahamu wako. You can not compare wakwepa kodi wa Bongo na wawekezaji wa kule Delta
   
 16. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #16
  Nov 13, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Noooooooooooooooo!!!! Pole sana. Nchi inajiendesha kwa kutoza kodi. Wafanyabiashara wakifilisika serikali itapata wapi kodi ya kuiendesha? Mawazo potofu kabisa. Hayafai. Pole sana
   
Loading...