Polisi yawagomea Lowassa, Sumaye, Mbowe Mwanza

Ukiwa mmeishiwa pa kunadi sera naona yule pimbi wenu makanisa ayamtaki wa misikiti sasa kakimbilia misibani aaaaah mfa maji aishi kutapatapa
 
hii ndio tanzania ambayo wawepata uhuru kwa kupewa bila hata kuchomwa sindano wala kuwekwa mahabusu na wakoroni lakini wamekuwa wagumu manna hii cjuh wangepata uhuru kwa kukaa jela kama Mandela au kupigana kama mau mau Kenya cjuh watawala wetu wangekuwaje kama sasa wanaona kama nchi ni Mali yao ukitaka kufanya chochote lazima upige magoti kwao
 
Nilikuwa nimeanza kumkubali Magufuli japo sikumpa kura yangu lakini kwa udhalimu huu unaofanywa na vyombo vya serikali anayoiongoza nitaendelea kuichukia ccm na wote wanaoiunga mkono.Naililia nchi yangu naona giza huko tuendako.
 
CHADEMA mnapenda ligi za kipuuzi. Hivi kwanini msiache familia ya marehemu impumzishe mpendwa wao!? Yani hii mijitu sijui ni mishetani!

Mngesema chadema haikushiriki.

Tumeacha kuwapeleka akina Lowassa kwa akina Mtoi mkadai jamaa ametelekezwa.

Polisi waliuzuia Mwili wa Deo kuagwa kiccm ccm?
 
wauwaji wanashida hawa..
mmeshaua basi toeni huo mwili wa mwanaharakati mwenzetu..
pia hamtaki..
mh madhalimu hawa..
Zenji 2001 waliwatandika risasi wapemba na kuwafukia kama mbwa..
mwaka 2015 wakawafutia matokeo ya ushindi na kutamani tena damu zao..
Mungu akawapa subira..
atawajibu kwa namna nyengine.
 
Ukiwa mmeishiwa pa kunadi sera naona yule pimbi wenu makanisa ayamtaki wa misikiti sasa kakimbilia misibani aaaaah mfa maji aishi kutapatapa

Hivi wewe tako unatokea Moshi ipi maana moshi hamna watu wanaowashwa na mshono kama wewe!
 
Sijawahi kuona serikali halali inayojiamini inahangaika na mambo ya kitoto namna hii! Utakuta hao polisi wanalipwa mpaka posho kwa kukaa barabarani kuzuia watu kuaga mwili wa marehemu! Mbona Firikujombe ccm walimzika kwa heshima zote na haikuwa nongwa?

Nadhani kuna kitu hakiko sawa ndiyo maana mambo yako hivyo!

Kwa uonevu huu nitaendelea kuichukia ccm hata kama magufuli atabadilisha maisha ya watanzania mpaka ufika hata kununua ndege kwa kila mtanzania nikiwemo na mimi!
 
Hivi kamanda Mawazo hakua na ndugu????
Kwanini maiti yake iwe mtaji wa kisiasa?
 
Last edited by a moderator:
Mwanza. Shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Geita, Aphonce Mawazo aliyeuawa wiki iliyopita iko katika sintofahamu baada ya chama hicho kudai kuzuiwa na polisi kuuchukua mwili huo katika Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC) ulikohifadhiwa.

Viongozi wa kitaifa wa Ukawa na Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe akiambatana na aliyekuwa mgombea urais, Edward Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, wakurugenzi wa Chadema na wabunge wa upinzani waliwasili jijini Mwanza, lakini hadi tunakwenda mitamboni hawakuwa wamechukua mwili huo.

Taarifa ya Chadema iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari, Tumaini Makene baadaye jioni ilisema vikao vilikuwa vinaendelea na kuwa taarifa za kina zingetolewa baadaye.

Viongozi wa Chadema Kanda ya Ziwa, walifika BMC jana saa 5.35 asubuhi kuuchukua mwili, lakini hawakufanikiwa na wakaondoka wakieleza kuwa wanakwenda kufanya mazungumzo kujadili suala hilo.

Makene alisema: ?Baada ya viongozi hao kuwasili na kupewa taarifa za awali kuhusu maandalizi ya ratiba ya utoaji wa heshima za mwisho kwa Kamanda Mawazo, wamesikitishwa sana na kitendo cha Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kuzuia shughuli hiyo kufanyika jijini humo.?

Akizungumzia kwa nini Mawazo aagwe Mwanza na baadaye Geita, Makene alisema mbali ya kuwa mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Geita, pia alikuwa kiongozi wa Kanda ya Ziwa ambayo inajumuisha mikoa ya Kagera, Mwanza na Geita.

Msimamo wa polisi
Hata hivyo, polisi walikanusha madai ya kuwazuia Chadema kuchukua mwili huo lakini wakasisitiza kuwa wamezuia shughuli za kuaga mwili huo zilizopangwa kufanyika katika ofisi za Kanda ya Ziwa za chama hicho.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo alisema wamefanya mazungumzo na baba mdogo wa marehemu, Mchungaji Charles Lukiko kuwa mwili huo watauchukua kesho (leo) na kwenda kuzika mkoani Geita.

?Sisi hatujawazuia Chadema kuchukua mwili wa Mawazo, ila wao wameingiza mambo ya kisiasa, tunachosema polisi ni kwamba hatutaki shughuli za kuaga mwili huo zifanyike mkoani hapa, wala mkusanyiko wa aina yoyote.?

Mkumbo alisema wamezuia mikusanyiko ya aina yoyote kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.

Baadaye Mchungaji Lukiko alisema familia itauchukua mwili wa marehemu kati ya leo na kesho kutoka Bugando na kuupeleka moja kwa moja Geita kwa ajili ya mazishi.

Bado kuna mvutano, Chadema wapo kwenye vikao vyao, wanataka kuuaga mwili wa mwenzao, lakini na sisi kama familia tunatarajia kati ya Jumapili au Jumatatu tutauchukua. Kwa sasa siwezi kusema zaidi ya hapo,? alisema Mchungaji Lukiko.

Shughuli hizo za kuaga mwili zilitarajiwa kufanyika jana kwenye Viwanja vya Furahisha au Ofisi za Chadema Kanda ya Ziwa.

Awali, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Kigaila Benson alisema: ?Tunashangaa polisi kutuzia kuuga mwili wa Mawazo, tulikubaliana kwamba mwili utaagwa katika ofisi za Kanda, lakini wametugeuka na kutuzuia kufanya hivyo utadhani sisi ni wahalifu.

?Mawazo hajafa kwa kipindupindu, wala hatuendi kula chakula tunataka tumuage ndugu yetu, wanavyotumia nguvu kubwa sijui inaashiria kitu gani, ni jambo la kusikitisha kwani angekuwa kafa mtu wa upande wa pili angeagwa na ulinzi angepewa.?

Mkurugenzi wa Chadema Kanda ya Ziwa, Peter Makere alisema Chadema ni jeshi kubwa zaidi na kwamba kwa vyovyote lazima mwili wa mwenzao uagwe kabla ya kwenda kuzikwa Geita.

Ulinzi mkali kila kona
Jana, Jiji la Mwanza lilipambwa na askari polisi waliyokuwa na sare na waliokuwa wamevalia kiraia kila kona baadhi yao wakiwa wamebeba silaha za moto na wengine mabomu ya machozi na wengine wakiwa na mbwa.

Polisi walitanda katika Barabara Kuu inayoingia kutoka mikoa kati, Hospitali ya Rufaa Bugando na kwenye ofisi za Chadema Kanda ya Ziwa zilizopo kona ya Bwiru.

Mawazo aliuawa Novemba 14 baada ya kuvamiwa na kundi la watu wanaodaiwa ni wafuasi wa CCM na tayari watu watano wamefikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji.

Ss ni mashujaa ndio maana serekali inatumia polisi kuzua hata mazishi yetu.... Kila siku katiba inavunjwa nakuongezwa vipengele vyakubana demeckasia na hawa wanaotumika siku moja watajibu mmoja mmoja kwa majina yao hii c upande wao tu bali ni ywtu sote
 
Jeshi la polisi ni vilaza,hawatumii akili!Kuaga msiba na kipindupindu wapi na wapi?foolish
 
Vituko sana vya ukawa! Kwani Lowasa na Sumaye nao ni viongozi wa chadema!? Up.u.uzi mtupu mnatafuta umaarufu kupitia mwili wa marehemu.
 
Ipo siku hayo maneno yatakuwa juu yako!!!!!

Nashangaa hadi ss intelijensia yetu haijakubaini......huo ni uchochezi na kutugawa wa-tz kwa makabila yetu!au ndo niki nemu,uhalisia ni huyo mkuu wa ulinzi huko?
 
Back
Top Bottom