justus ndyanabo
JF-Expert Member
- Jun 2, 2015
- 444
- 379
Nitaingia kaburini bila kuipenda CCM na wanaccm yao mna roho mbaya kama mashetani
Umepanga kuingia Kaburini lini?Nitaingia kaburini bila kuipenda CCM na wanaccm yao mna roho mbaya kama mashetani
..hakuna biashara ya kudeki barabara na hakuna mtu anaekesha akinywa pombe nje ya hotel aliyofikia...
CHADEMA mnapenda ligi za kipuuzi. Hivi kwanini msiache familia ya marehemu impumzishe mpendwa wao!? Yani hii mijitu sijui ni mishetani!
Kwanza niungane na watanzania wote wapenda Amani kumuombea marehemu mawazo mungu amtangulie na kumlaza mahali pema peponi.
Na pia nalaani kwa nguvu zote mauaji ya Aina hii iwe kwa wanasiasa au kwa binadamu mwezetu yeyote, kwani ni haki ya kila binadamu kuishi duniani hadi mungu atakapoamua juu ya mauti yake.
Na ni hakika kila nafsi itaonja mauti hapa duniani.
My take :
Tatizo ninaloliona hapa ni jinsi ambavyo chadema na UKAWA Kwa pamoja wanapotaka kuugeuza msiba huu kama mtaji au turufu ya kisiasa.
Taifa letu ndio Kwanza tumemaliza zoezi la uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge..
Kuna makovu mengi na vidonda, kila sehemu ya nchi hii kisiasa (kwa walioshindwa na walioshinda) .
Rais bado hajateua hata baraza la mawaziri, kwa maana kwamba bado tuko katika kipindi cha mpito kuelekea uundaji wa serikali mpya chini ya Rais mteule mh. Dk JPM.
. Wakati Hali iko hivyo chadema kwa makusudi mnalazimisha kukusanya umati mkubwa wa watu, kwa kisingizio cha msiba huu, ilhali kila mtanzania anatambua jinsi mbowe na lowassa mlivyo na machungu ya kushindwa uchaguzi huu, mliotarajia kuingia ikulu ya magogoni kwa matarajio makubwa Bila mafanikio.
Juu ya Hilo pia kuyakosa na kuyapoteza majimbo ya nyamagana na ilemela imekuwa kama kumwagia kidonda kibichi chumvi.
Wakati haya yoote yakijiri bado ndani ya chadema kuna fukuto na malalamiko ambayo yametishia uhai wa BAWACHA kutokana na zoezi la uteuzi wa viti maalumu vya ubunge, kufanyika kwa upendeleo na sio siri kwamba uongozi wa cdm makao makuu bado unakwepa kuwaeleza wanachama wenu kuhusu malalamiko haya..
Kwa sababu watanzania tunaishi kwa matukio (sio wote) UKAWA na chadema mnataka kutumia msiba wa marehemu kamanda Mawazo kama nafasi ya kuusahaulisha umma juu ya machungu ya uchaguzi hususan ufukwazwaji kinyemela wa waasisi muhimu wa hoja zenye mashiko ndani ya Chama na umma kwa ujumla kama Dr slaa na kujiaminisha kuwa lowassa alikuwa ndio kila kitu katika kuingia ikulu kwa short cut, almaarufu Gia ya angani.
Maswali muhimu kwa UKAWA :
Wakati mnataka kuukusanya umma kwa kisingizio cha kumuaga marehemu, tuna uhakika gani na Aina ya maneno yatayotolewa katika hotuba za viongozi wenu kitaifa, kwamba hayataweza kuibua hisia za mihemko ya kisiasa na kuelekea uvunjifu wa Amani pale mamlaka husika zitakapojaribu kuwaeleza kuwa mnatoka nje ya Mada husika?
Mfano Hai tulishuhudia kupitia vyombo vya Habari nchi nzima wafuasi wa cdm wakidiriki kumpiga askari aliyekuwa kazini, huko katika hospitali ya Bugando, na tulishuhudia uhamasishaji wa Lema, sembuse huko furahisha?
Je kama marehemu alifikwa na mauti huko geita, ambako pia ni kwao, kuna Tatizo gani shughuli hii yote isifanyikie huko?
Kama mnamheshimu na mlimpenda marehemu, ni kwa nini msiitendee haki Familia yake kwa kuupeleka mwili wake kwa wanandugu wakatoe heshima zao za mwisho kwa mpendwa mwendazake.?
Badala ya kutumia mwili huu kisiasa, ningewashauri mkaandaa mkutano maalum na siku maalum ya kuwashukuru wapiga kura wenu na wananchi kwa ujumla jijini mwanza. Na hapo ni rukhsa kuongea lolote ambalo mnalo na mngependa kuujulisha umma Bila kificho ilimradi hamvunji sheria kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu.
Nahitimisha kwa kulaani mauaji ya mtanzania mwenzetu na aliyekuwa hazina na Mfano wa kuigwa kwa wanasiasa wapenda democracy ya kweli nchini,
NI muhimu serikali ifanye uchunguzi wa kina na kuhakikisha waovu Hao wamefikishwa mbele ya sheria Ili haki itendeke na iwe fundisho kwa wengine wenye ufidhuli wa namna hii,
Hakika mawazo ametuacha kimwili lakini tutamuwaza daima.
Amen
HAMMY-D, ifikie wakati ubinadamu uwe zaidi ya siasa na maslahi yetu binafsi! Leo kuna msiba Dar es salaam wa katibu wa umoja wa wadreva. Niambie je! Dar hataagwa, na kama atazikwa kwao Mwanza, Mwanza hawatamuaga? Dar kipindupindu ndiko kimeanzia, Marehemu Kigoda,Kombani na Filikunjombe waliagwa tena kwa taratibu zetu za kiafrika kama ilivyo kawaida yetu. Hapa kafariki mtu wa CHADEMA mabomu yametanda, hivi napo hapa mnaongelea CHADEMA wanamatatizo? Ifikie wakati tuweke pembeni itikadi za vyama. Hivi mnataka ifikie wakati CCM akifariki azikwe na CCM na vyama vingine vivyo hivyo? Hii ni aibu, kama ndo mkuu wetu wa mkoa anaratibu hili kama inavyosemekana na wengi, basi mheshimiwa raisi hapa hana kiongozi. Kiongozi yeyote anaeonekana kutaka kuwagawa watanzania kwa jinsi yoyote na apingwe kwa nguvu zote! Hapa tumewaingiza ndugu zetu wa jeshi la polisi kwenye mgogoro usio wahusu hata kidogo! Hebu tusikie toka ofisi ya Afisa afya wa mkoa,Je! kipindupindu mkoani Mwanza kimefikai hatua ya kuzuia kuaga mwili wa marehemu alieuawa kwa mashoka na mapanga na si kwamba kafariki kwa kipindupindu? Kwa nini tamko hili lisitolewe na ofisi ya afisa afya wa mkoa? Nawapa pole sana polisi sababu wanajengewa chuki isiyowahusu. Mh raisi hesabu kwa Mwanza hauna kiongozi,unless kama hili lina baraka toka kwako kitu ambacho binafsi hakiingii akilini mwangu. Ninakufahamu na nmekufahamu siku nyingi.,hauko hivi labda ujifunze leo. Nakujua wewe si mwanza siasa bali ni mtu wa kazi. Wanasiasa watakuharibia nchi. Hapa kunajengwa chiki itakayozaa kuchukia serikali. Serikali iliyopita ilichukiwa kwa sababu ya kunyima watu haki zao.....tafadhari usijiingize kwenye huu upuuzi. Waachie waliozoea kunyanyasa wananchi kwa visingizo visivyokuwa na kichwa wala miguu. Hii double standard itaisha lini?CHADEMA mnapenda ligi za kipuuzi. Hivi kwanini msiache familia ya marehemu impumzishe mpendwa wao!? Yani hii mijitu sijui ni mishetani!
Nilikuwa nimeanza kumkubali Magufuli japo sikumpa kura yangu lakini kwa udhalimu huu unaofanywa na vyombo vya serikali anayoiongoza nitaendelea kuichukia ccm na wote wanaoiunga mkono.Naililia nchi yangu naona giza huko tuendako.
Mwanza. Shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Geita, Aphonce Mawazo aliyeuawa wiki iliyopita iko katika sintofahamu baada ya chama hicho kudai kuzuiwa na polisi kuuchukua mwili huo katika Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC) ulikohifadhiwa.
Viongozi wa kitaifa wa Ukawa na Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe akiambatana na aliyekuwa mgombea urais, Edward Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, wakurugenzi wa Chadema na wabunge wa upinzani waliwasili jijini Mwanza, lakini hadi tunakwenda mitamboni hawakuwa wamechukua mwili huo.
Taarifa ya Chadema iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari, Tumaini Makene baadaye jioni ilisema vikao vilikuwa vinaendelea na kuwa taarifa za kina zingetolewa baadaye.
Viongozi wa Chadema Kanda ya Ziwa, walifika BMC jana saa 5.35 asubuhi kuuchukua mwili, lakini hawakufanikiwa na wakaondoka wakieleza kuwa wanakwenda kufanya mazungumzo kujadili suala hilo.
Makene alisema: ?Baada ya viongozi hao kuwasili na kupewa taarifa za awali kuhusu maandalizi ya ratiba ya utoaji wa heshima za mwisho kwa Kamanda Mawazo, wamesikitishwa sana na kitendo cha Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kuzuia shughuli hiyo kufanyika jijini humo.?
Akizungumzia kwa nini Mawazo aagwe Mwanza na baadaye Geita, Makene alisema mbali ya kuwa mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Geita, pia alikuwa kiongozi wa Kanda ya Ziwa ambayo inajumuisha mikoa ya Kagera, Mwanza na Geita.
Msimamo wa polisi
Hata hivyo, polisi walikanusha madai ya kuwazuia Chadema kuchukua mwili huo lakini wakasisitiza kuwa wamezuia shughuli za kuaga mwili huo zilizopangwa kufanyika katika ofisi za Kanda ya Ziwa za chama hicho.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo alisema wamefanya mazungumzo na baba mdogo wa marehemu, Mchungaji Charles Lukiko kuwa mwili huo watauchukua kesho (leo) na kwenda kuzika mkoani Geita.
?Sisi hatujawazuia Chadema kuchukua mwili wa Mawazo, ila wao wameingiza mambo ya kisiasa, tunachosema polisi ni kwamba hatutaki shughuli za kuaga mwili huo zifanyike mkoani hapa, wala mkusanyiko wa aina yoyote.?
Mkumbo alisema wamezuia mikusanyiko ya aina yoyote kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Baadaye Mchungaji Lukiko alisema familia itauchukua mwili wa marehemu kati ya leo na kesho kutoka Bugando na kuupeleka moja kwa moja Geita kwa ajili ya mazishi.
Bado kuna mvutano, Chadema wapo kwenye vikao vyao, wanataka kuuaga mwili wa mwenzao, lakini na sisi kama familia tunatarajia kati ya Jumapili au Jumatatu tutauchukua. Kwa sasa siwezi kusema zaidi ya hapo,? alisema Mchungaji Lukiko.
Shughuli hizo za kuaga mwili zilitarajiwa kufanyika jana kwenye Viwanja vya Furahisha au Ofisi za Chadema Kanda ya Ziwa.
Awali, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Kigaila Benson alisema: ?Tunashangaa polisi kutuzia kuuga mwili wa Mawazo, tulikubaliana kwamba mwili utaagwa katika ofisi za Kanda, lakini wametugeuka na kutuzuia kufanya hivyo utadhani sisi ni wahalifu.
?Mawazo hajafa kwa kipindupindu, wala hatuendi kula chakula tunataka tumuage ndugu yetu, wanavyotumia nguvu kubwa sijui inaashiria kitu gani, ni jambo la kusikitisha kwani angekuwa kafa mtu wa upande wa pili angeagwa na ulinzi angepewa.?
Mkurugenzi wa Chadema Kanda ya Ziwa, Peter Makere alisema Chadema ni jeshi kubwa zaidi na kwamba kwa vyovyote lazima mwili wa mwenzao uagwe kabla ya kwenda kuzikwa Geita.
Ulinzi mkali kila kona
Jana, Jiji la Mwanza lilipambwa na askari polisi waliyokuwa na sare na waliokuwa wamevalia kiraia kila kona baadhi yao wakiwa wamebeba silaha za moto na wengine mabomu ya machozi na wengine wakiwa na mbwa.
Polisi walitanda katika Barabara Kuu inayoingia kutoka mikoa kati, Hospitali ya Rufaa Bugando na kwenye ofisi za Chadema Kanda ya Ziwa zilizopo kona ya Bwiru.
Mawazo aliuawa Novemba 14 baada ya kuvamiwa na kundi la watu wanaodaiwa ni wafuasi wa CCM na tayari watu watano wamefikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji.
Inchi yako uchagani si kanda ya ziwa.