Polisi yawagomea Lowassa, Sumaye, Mbowe Mwanza

Polisi yawagomea Lowassa, Sumaye, Mbowe Mwanza

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Posts
4,346
Reaction score
9,846
Mwanza. Shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Geita, Aphonce Mawazo aliyeuawa wiki iliyopita iko katika sintofahamu baada ya chama hicho kudai kuzuiwa na polisi kuuchukua mwili huo katika Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC) ulikohifadhiwa.

Viongozi wa kitaifa wa Ukawa na Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe akiambatana na aliyekuwa mgombea urais, Edward Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, wakurugenzi wa Chadema na wabunge wa upinzani waliwasili jijini Mwanza, lakini hadi tunakwenda mitamboni hawakuwa wamechukua mwili huo.

Taarifa ya Chadema iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari, Tumaini Makene baadaye jioni ilisema vikao vilikuwa vinaendelea na kuwa taarifa za kina zingetolewa baadaye.

Viongozi wa Chadema Kanda ya Ziwa, walifika BMC jana saa 5.35 asubuhi kuuchukua mwili, lakini hawakufanikiwa na wakaondoka wakieleza kuwa wanakwenda kufanya mazungumzo kujadili suala hilo.

Makene alisema: ?Baada ya viongozi hao kuwasili na kupewa taarifa za awali kuhusu maandalizi ya ratiba ya utoaji wa heshima za mwisho kwa Kamanda Mawazo, wamesikitishwa sana na kitendo cha Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kuzuia shughuli hiyo kufanyika jijini humo.?

Akizungumzia kwa nini Mawazo aagwe Mwanza na baadaye Geita, Makene alisema mbali ya kuwa mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Geita, pia alikuwa kiongozi wa Kanda ya Ziwa ambayo inajumuisha mikoa ya Kagera, Mwanza na Geita.

Msimamo wa polisi
Hata hivyo, polisi walikanusha madai ya kuwazuia Chadema kuchukua mwili huo lakini wakasisitiza kuwa wamezuia shughuli za kuaga mwili huo zilizopangwa kufanyika katika ofisi za Kanda ya Ziwa za chama hicho.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo alisema wamefanya mazungumzo na baba mdogo wa marehemu, Mchungaji Charles Lukiko kuwa mwili huo watauchukua kesho (leo) na kwenda kuzika mkoani Geita.

?Sisi hatujawazuia Chadema kuchukua mwili wa Mawazo, ila wao wameingiza mambo ya kisiasa, tunachosema polisi ni kwamba hatutaki shughuli za kuaga mwili huo zifanyike mkoani hapa, wala mkusanyiko wa aina yoyote.?

Mkumbo alisema wamezuia mikusanyiko ya aina yoyote kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.

Baadaye Mchungaji Lukiko alisema familia itauchukua mwili wa marehemu kati ya leo na kesho kutoka Bugando na kuupeleka moja kwa moja Geita kwa ajili ya mazishi.

Bado kuna mvutano, Chadema wapo kwenye vikao vyao, wanataka kuuaga mwili wa mwenzao, lakini na sisi kama familia tunatarajia kati ya Jumapili au Jumatatu tutauchukua. Kwa sasa siwezi kusema zaidi ya hapo,? alisema Mchungaji Lukiko.

Shughuli hizo za kuaga mwili zilitarajiwa kufanyika jana kwenye Viwanja vya Furahisha au Ofisi za Chadema Kanda ya Ziwa.

Awali, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Kigaila Benson alisema: ?Tunashangaa polisi kutuzia kuuga mwili wa Mawazo, tulikubaliana kwamba mwili utaagwa katika ofisi za Kanda, lakini wametugeuka na kutuzuia kufanya hivyo utadhani sisi ni wahalifu.

?Mawazo hajafa kwa kipindupindu, wala hatuendi kula chakula tunataka tumuage ndugu yetu, wanavyotumia nguvu kubwa sijui inaashiria kitu gani, ni jambo la kusikitisha kwani angekuwa kafa mtu wa upande wa pili angeagwa na ulinzi angepewa.?

Mkurugenzi wa Chadema Kanda ya Ziwa, Peter Makere alisema Chadema ni jeshi kubwa zaidi na kwamba kwa vyovyote lazima mwili wa mwenzao uagwe kabla ya kwenda kuzikwa Geita.

Ulinzi mkali kila kona
Jana, Jiji la Mwanza lilipambwa na askari polisi waliyokuwa na sare na waliokuwa wamevalia kiraia kila kona baadhi yao wakiwa wamebeba silaha za moto na wengine mabomu ya machozi na wengine wakiwa na mbwa.

Polisi walitanda katika Barabara Kuu inayoingia kutoka mikoa kati, Hospitali ya Rufaa Bugando na kwenye ofisi za Chadema Kanda ya Ziwa zilizopo kona ya Bwiru.

Mawazo aliuawa Novemba 14 baada ya kuvamiwa na kundi la watu wanaodaiwa ni wafuasi wa CCM na tayari watu watano wamefikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji.
 
....


......7 bila za Algeria zilikuwa halali yetu !!!!


na Bunge nalo lipigwe marufuku maana ni mkusanyiko...........
 
Siasa hadi kwenye misiba! CHADEMA bwana ndo maana hata mlizuiwa kumzika KISUMO na mabodaboda yenu
 
Je hapa mtasema Lema kahamishia vurugu Mwanza au mtawataka radhi watu wa arusha kipindi kile Mulongo Magesa alivyokua mkuu wa mkoa wa Arusha mlidhani vurugu zinaletwa na Lema na raiya wake wema.
Mmeshamjua mleta fujo ?
 
Naililia nchi yangu tz kwa haya yanayoendelea yanaashilia amani kutoweka.
 
Siasa hadi kwenye misiba! CHADEMA bwana ndo maana hata mlizuiwa kumzika KISUMO na mabodaboda yenu

Kwani aliekufa alikuwa askofu au mwanasiasa... kira roho itaonja mauti...
 
Siasa hadi kwenye misiba! CHADEMA bwana ndo maana hata mlizuiwa kumzika KISUMO na mabodaboda yenu


Mkuu..hivi hapa anayeleta siasa msibani ni nani kati ya polisi na chadema??
 
Wayapige tu hayo machaga,yameivuruga arusha,sasa yanataka kuivuruga na mwanza.
 
hapa kuna watu wanakwenda kupata aibu,familia itachukua mwili na utaenda moja kwa moja geita,hakuna mwanafamilia atavumilia mwili wa ndugu yake uendelee kuharibika,ili tu wanasiasa wapate kumtumia
 
CHADEMA mnapenda ligi za kipuuzi. Hivi kwanini msiache familia ya marehemu impumzishe mpendwa wao!? Yani hii mijitu sijui ni mishetani!
 
CHADEMA mnapenda ligi za kipuuzi. Hivi kwanini msiache familia ya marehemu impumzishe mpendwa wao!? Yani hii mijitu sijui ni mishetani!

Shetani sio nyie mliomuua?
 
Hamy-D machadema sera yao ni kujitafutia umaharufu wa kisiasa mpaka kwenye misiba umesahau yule pimbi wao lowasa alivyozuiwa kule mwanga
 
Taifa letu bana!! Hapo kina mbowe wasingeenda wangeitwa wanafiki..wameenda wanazuiwa kuzika eti ni siasa!! Kwani eliekufa ni paroko??? Msiba wa kombani dar hapakua na kipindupindu?????
 
CHADEMA mnapenda ligi za kipuuzi. Hivi kwanini msiache familia ya marehemu impumzishe mpendwa wao!? Yani hii mijitu sijui ni mishetani!

Hujui usemacho mpaka siku ukiona unaonewa au ndugu yako anaonewa.Kwa timamu zako kuna mtu anazuiliwa kuaga mwili au kuomboleza...labda nikwambie "fill the blanks....taja hali/vitu ambavyo husababisha mikusanyiko ya watui)........ii)..........jaza basi.We know the the so called RC na ubabe wake bt kama kila mtu ana dini basi tumwachie Mungu.Wako wap kina Saadam....
 
Hamy-D machadema sera yao ni kujitafutia umaharufu wa kisiasa mpaka kwenye misiba umesahau yule pimbi wao lowasa alivyozuiwa kule mwanga

Wewe chizi kweli umesahau msiba wa kigoda ee(alinitumia e-mail akiwa icu by magu)
 
Je hapa mtasema Lema kahamishia vurugu Mwanza au mtawataka radhi watu wa arusha kipindi kile Mulongo Magesa alivyokua mkuu wa mkoa wa Arusha mlidhani vurugu zinaletwa na Lema na raiya wake wema.
Mmeshamjua mleta fujo ?

yaani huyo mhogo huwa hawafai...ubabe ubabe tu na kujiona yeye ndo kila kitu.angalia mikoa anayoongoza lazima sintofahamu ziwepo.siku zote kiongozi akikosa busara na hekima mambo huwa tofauti.Polisi wenyewe na Maisha yao ya kuishi ndan ya kuta za bati hasira wanamalizia kwenye upinzani.kama wanapendwa sana wangeishi kifalme basi bongo hii,yanaishia kutumika vibaya na kujichumia dhambi tu
 
Back
Top Bottom