Polisi yakiri kupiga mtu risasi maandamano ya CHADEMA

Polisi yakiri kupiga mtu risasi maandamano ya CHADEMA

Aliyepoteza dira ni Yule asiye weza kujisimamia mwenyewe katika ushindi Bali kutegeme mtutu wa bunduki na mapanga.
 
... Mambosasa amesema “Walizuia mwendo kasi, wakaanza kupiga mawe kwa hiyo kati ya risasi za hewani zilizopigwa kuwatawanya kuna iliyompata (mtu)...”
Eti risasi zipigwe hewani halafu zimpate mtu! Kwani huyo mtu alikuwa hewani? Hebu wasitufanye wajinga huko
 
Tatizo Magufuli anakuwa kama yuko mbinguni haoni kinachotokea katika nchi anayotawala!

Hivi kweli anashindwa kukemea unadhalimu huu unaoendelea nchini!?
Ukishakuwa kiongozi wa ccm unakuwa mungu ndani ya nchi .
 
Risasi zilipigwa hewani zikampata mtu..
Sijui kama ni mwanafunzi ntajua nikifika ofisini nipo kwenye pilika pilika za uchaguzi...
Inamaana hawa jamaa wanafanya kazi in series.. Heheheh
 
Huyo jamaa nadhani ni mwendawazimu. Hao binadamu waliopigwa risasi walikuwa ndege waliokuwa wanaruka angani mpaka wapigwe na risasi iliyoelekezwa angani?
 
Ila angeuwawa Tembo au Faru tungesikia mpaka Waziri Mkuu anataka aonyeshwe kaburi yake.

Amekufa binadamu tena mtoto aliye masomoni watawala wote kimya hata kwa kukemea. Hivi tukiitwa shithole countries tunataka ufafanuzi gani tena?
 
Leo nimetoa waraka kwa familia yangu yote , kama kuna MTU anajijua ni CCM nimempa Masaa 49 aje atubu mbele yangu kinyume na hapo nisimjue na yeye asinijue...



Kumbuka Mimi sina chama na sio mwanachama wa chama chochote ni Heri niwe na ndugu mchawi,shetani,ibilisi, jini mkata kamba au pepo la kuzimu kuliko kuwa na ndugu kutoka chama kinachodharau watanzania wengine wanaotekeleza haki zao kikatiba.


Kulikuwa na haja gani kuwanyina watu viapo vyao na baada ya vifo mkawapa hivyo viapo ( this is insanity)...



Na nimewaambia hata nikifa sitaki ndugu yangu,rafiki au jirani CCM asisogelee eneo la tukio. Na Mimi hivyo hivyo kuanzia Leo mpaka kifo changu Niko radhi kabisa nimsaidie Ibilisi wa mguu mmoja kuliko mwanaCCM iwe duniani au mbinguni.

Misiba ,harusi, birthday au magonjwa na majanga sitaki nisaidiwe na CCM yoyote na mini sitamsaidia mwanaCCM yoyote. Na kuanzia Leo sitatoa msaada bila kukuuliza chama chako.



Enough is Enough
Wewe ni USAid, JiCA, au KONICA au Caritas !?
 
Risasi hazikupigwa hewani! Risasi zililenga watu na waliopigwa risasi ni wengi ingawa mmoja alifariki. Wapo waliovunjwa miguu kwa risasi hivyo aache majibu ya kijinga!
Leta picha
 
Haya majibu yananifikirisha sana but nahisi si mtanzania na umetumwa kuja kuliangamiza taifa

Nina amini wewe ni mfuasi mzuri sana wa CCM coz nimekufuatilia kwa muda mrefu sana na upo hapo kulinda kitu flan

Mungu tetea taifa hili majibu ya hawa wafuasi ya CCM wanaashiria wamejipanga kuliangamiza hili taifa tenda miujiza sasa
Mkuu, umeeleza kitu cha maana sana ambacho wengi hawakijui. Magufuli kaleta Wanyarwanda wengi kwenye mitandao ya kijamii wakijiita majina ya kihaya na kisukuma. Chunguza Id feki za kihaya na kisukuma wanayoyasema ni ya kiuaji kabisa.
 
Mbona jibu jepesi sana kamanda ametoa!??? Amepigwa na risasi zilizokuwa zinapigwa hewani!?????
Huyo aliepigwa risasi nae alikuwa hewani!??
Hiyo sentensi ya mwisho ndio inayozua mjadala kwenye taarifa ya huyo polisi!
 
Katika Hali isiyo ya kawaida kwa kamanda mwenye uzoefu Na kazi yake..
Akizunguza Na MCL DIGITAL Leo trh 17.febr 2018 kamanda WA polisi,Mambosa [emoji117]amesema kuwa polisi walitumia risasi za moto katika kuwatawanya wanachama WA Upizani baada ya kuandamana.,[emoji117]amesema polisi walipiga risasi hewani,katika risasi hizi ilimpata mtu
[emoji117]Tena hajaeleza kama amekufa au LA!!
Sasa.
[emoji117]Swali langu kwa kamanda hiyo lisasi ya hewani iliyompata mtu je huyo mtu alikuwa angani???..nimepata ukakasi juu ya maelezo yako kamanda mzoefu!!!
=====#mambosasa weledi uko wapi??#====
 
Risasi ya hewani itapigaje kifuani mwa binadamu ndani ya daladala? Au risasi ya hewani ni kwa kuwa inapita kwenye hewa kabla ya kufikia target?
Tatizo sio Mambosasa,bali bosi na hataki kutubu
Hujui ami, hii ilitokeaga Zenjibar hii. Risasi ya hewani uliuawa wanenji kule miaka ileeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Back
Top Bottom