Pilato 007
JF-Expert Member
- Sep 6, 2017
- 447
- 472
Na bado kuna wengine humu wana mtetea kamanda na kauli yakeHata Mimi nashangaa! Huyu ni wa kukamatwa na kuwekwa ndani
Na bado kuna wengine humu wana mtetea kamanda na kauli yakeHata Mimi nashangaa! Huyu ni wa kukamatwa na kuwekwa ndani
Mbowe kila siku anapenda kusababisha mauaji wa watu kwa maandamano yasiyo na tija
Hata hamuangalii hoja zenu zilivyo nyepesi?! Ukiwa mtu wa kusifu na kuabudu ni sheeeda sana.Huyu Mbowe ni mhuni tokea zamani. Anaanzisha vurugu halafu anaanza kuwalaumu polisi.
Umeambiwa risasi ya hewani siyo ya juu? Au hukusoma vizuri habari?Wataalamu mliosoma sijui MOTION, mara PROJECTILE na zifananazo, naomba kuuliza;
Kuna uwezekano RISASI iliyopigwa kuelekezwa juu ikafikia velocity yake ya mwisho kisha ikarudi na kuua/piercing human body???
Natanguliza shukrani zangu za dhati!
Magufuli haelewi kuwa damu ya huyu mtoto aliyeuawa na polisi wa chama chake yaweza kuwa na nguvu kuliko yeye, hao polisi na majeshi yake yote
Tafadhali tusifike kwenye imani za watu kwa huo ushabiki wa kipuuzi...wakiristo wanakunywa damu ya Yesu na mwili wake, iwe nongwa kwa ccm !?
Mbowe kila siku anapenda kusababisha mauaji wa watu kwa maandamano yasiyo na tija
shughuli za msiba na mazishi ya huyu mwanafunzi yanafanyikia wapi? pole kwa wazazi, ndugu na jamaa zake! pole kwa TZ!Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri mtu mmoja kupigwa risasi na polisi wakati wakiwatawanya wafuasi wa Chadema walioandama jana Februari 16, 2018.
....
Taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo zilianza kusambaa tangu Ijumaa jioni katika mitandao ya kijamii sambamba na kuwekwa picha yake huku ikieleza kuwa amepigwa risasi wakati akiteremka katika basi....
Mwananchi
Hoja nyepesi kivipi?Hata hamuangalii hoja zenu zilivyo nyepesi?! Ukiwa mtu wa kusifu na kuabudu ni sheeeda sana.
Labda siku hizi kuna technology ya kisasa daladala zinapaa angani..hongera kamanda!Risasi ya hewani itapigaje kifuani mwa binadamu ndani ya daladala? Au risasi ya hewani ni kwa kuwa inapita kwenye hewa kabla ya kufikia target?
Tatizo sio Mambosasa,bali bosi na hataki kutubu
Tuna Watawala wenye mentality za Kikoloni bado! Hata jeshi la Polisi limeundwa katika mfumo wa Kikoloni!Na bado kuna wengine humu wana mtetea kamanda na kauli yake
Jiulize mwenyewe, wafuasi wa u dictator mnachokisapoti ni nini?! Binti huyu kauwawa kwa mzuka tu bila sababu!!Hoja nyepesi kivipi?
Risasi iyopigwa hewani ikampatavmtu ardhini.Kadiri Sikh zinavyoenda teknologia ya kupiga risasi inakuwa kwa kasi.waweza lenga juu ikashoot chini asante.Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri mtu mmoja kupigwa risasi na polisi wakati wakiwatawanya wafuasi wa Chadema walioandama jana Februari 16, 2018.
Wafuasi hao wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe waliandamana kuelekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli kudai viapo vya mawakala wa chama hicho.
Maandamano hayo yalianzia viwanja vya Buibui Mwananyamala ulikokuwa ukifanyika mkutano wa kampeni wa Chadema na yalipofika eneo la Mkwajuni wafuasi hao walitawanywa na polisi, huku mtu mmoja aliyekuwa kwenye basi la daladala akidaiwa kupigwa risasi na kufariki dunia.
Akizungumza na MCL Digital, Februari 17 leo Jumamosi, Mambosasa amesema “Walizuia mwendo kasi, wakaanza kupiga mawe kwa hiyo kati ya risasi za hewani zilizopigwa kuwatawanya kuna iliyompata (mtu).”
Ufafanuzi huo wa Mambosasa licha ya kutoweka wazi kama mtu huyo amefariki dunia ama la, umekuja huku ikidaiwa kuwa aliyepigwa risasi na kupoteza maisha ni mwanafunzi wa elimu ya juu.
Taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo zilianza kusambaa tangu Ijumaa jioni katika mitandao ya kijamii sambamba na kuwekwa picha yake huku ikieleza kuwa amepigwa risasi wakati akiteremka katika basi.
Mambosasa alipoulizwa kama mtu huyo ni mwanafunzi wa elimu ya juu amesema, “Haijathibitishwa hiyo, nipo kwenye pilika za uchaguzi, nadhani nitajibu hilo nitakaporejea ofisini na kupata taarifa.”
Uchaguzi wa majimbo ya Kinondoni na Siha unaendelea leo Jumamosi na Mwananchi litakuwa linakuletea kila kinachoendelea.
Mwananchi
Mbowe asingeleta uhuni wake wa kuvunja sheria huyo binti angeuawa?...Binti huyu kauwawa kwa mzuka tu bila sababu!!...