Polisi yakiri kupiga mtu risasi maandamano ya CHADEMA

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri mtu mmoja kupigwa risasi na polisi wakati wakiwatawanya wafuasi wa Chadema walioandama jana Februari 16, 2018.

Wafuasi hao wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe waliandamana kuelekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni, Aron Kagurumjuli kudai viapo vya mawakala wa chama hicho.

Maandamano hayo yalianzia viwanja vya Buibui Mwananyamala ulikokuwa ukifanyika mkutano wa kampeni wa Chadema na yalipofika eneo la Mkwajuni wafuasi hao walitawanywa na polisi, huku mtu mmoja aliyekuwa kwenye basi la daladala akidaiwa kupigwa risasi na kufariki dunia.

Akizungumza na MCL Digital, Februari 17 leo Jumamosi, Mambosasa amesema “Walizuia mwendo kasi, wakaanza kupiga mawe kwa hiyo kati ya risasi za hewani zilizopigwa kuwatawanya kuna iliyompata (mtu).”

Ufafanuzi huo wa Mambosasa licha ya kutoweka wazi kama mtu huyo amefariki dunia ama la, umekuja huku ikidaiwa kuwa aliyepigwa risasi na kupoteza maisha ni mwanafunzi wa elimu ya juu.

Taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo zilianza kusambaa tangu Ijumaa jioni katika mitandao ya kijamii sambamba na kuwekwa picha yake huku ikieleza kuwa amepigwa risasi wakati akiteremka katika basi.

Mambosasa alipoulizwa kama mtu huyo ni mwanafunzi wa elimu ya juu amesema, “Haijathibitishwa hiyo, nipo kwenye pilika za uchaguzi, nadhani nitajibu hilo nitakaporejea ofisini na kupata taarifa.”

Uchaguzi wa majimbo ya Kinondoni na Siha unaendelea leo Jumamosi na Mwananchi litakuwa linakuletea kila kinachoendelea.

PIA SOMA
- Maandamano ya CHADEMA: Aqulina Akwilini Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza NIT apigwa risasi na kufariki; Polisi wakiri kuhusika

Mwananchi
 
Siongei maneno mengi zaidi ya kuwambia uongozi wa serikali ya wanafunzi DARUSO kuwa mwenzenu kauwawa na aliyeuwa inajulikana ni askari maana risasi zilikuwa zinapigwa na askari polisi hivyo askari walioenda jana kinondoni wanajulikana kwaiyo ni muda huaafaka askari aliyehusika na mauji hayo akajulikana
 
Risasi ya hewani itapigaje kifuani mwa binadamu ndani ya daladala? Au risasi ya hewani ni kwa kuwa inapita kwenye hewa kabla ya kufikia target?
Tatizo sio Mambosasa,bali bosi anayewashwa na hataki kutubu

haya unayoandika umeyashuudia au kuna mtu aliyeshuudia kayasema? mnaamini uzushi wa watu waliopoteza dira
 
Vijana kuweni makini, polisi Ongezeni umakini. Kwasasa hatuitaji watu kupigana risasi tukauana kama wale polisi wa marekani wanao uwa watu kwa makusudi wakiwa kwenye maandamano.
 
Back
Top Bottom