Polisi yakana kumkamata Salum Mwalimu, yadai alijipeleka mwenyewe ili akamatwe

Maaskari wetu hawa wanafanya kazi kwenye mazingira magumu mno.

Kazi ya askari siyo hiyo; ni sawa na wewe uwe dereva wa familia ila mama kwenye nyumba muda mwingine akutume sokoni; ufue nguo za mtoto na kudeki..kazi utaiona ngumu ila hutakuwa na namna kwa kweli.
 
TBC : " ITV matatani baada ya mkurugenzi wa uchaguzi NEC kuhoji taarifa zilizorushwa na ITV za sanduku la kura kuporwa mtaa wa Idrissa kitongoji cha Magomeni jimbo la Kinondoni Dar-es-Salaam bila kupata idhidi ya NEC/TUME au msimamizi wa kituo husika"



Hili nililitarajia maana wamepanga kufanya wizi wa kura wa ajabu, hivyo hawataki matangazo yoyote ya mambo haya. Leo kuna kituoa huwa kinatangaza uchaguzi unapofanyika hapa nchi lakini wako kimya tu. Ninahakika wameambiwa wasithubutu kurusha haya matangazo.
 
Baadhi ya hawa mapoliccm suala la kutumia akili kwao halipo kabisa wanaongea kama ma zombie
 
Hili nililitarajia maana wamepanga kufanya wizi wa kura wa ajabu, hivyo hawataki matangazo yoyote ya mambo haya. Leo kuna kituoa huwa kinatangaza uchaguzi unapofanyika hapa nchi lakini wako kimya tu. Ninahakika wameambiwa wasithubutu kurusha haya matangazo.

Masuala ya kusikitisha sana, maana hata matokeo yanayobandikwa nje ya vituo vya kupigia kura nina mashaka kama yataruhusiwa hata kuoneshwa na TBC kabla ya NEC "kuhakiki" wakati msimamizi wa kituo kayaidhinisha majumuisho ya matokeo na yamesainiwa na wakala wa kila wagombea.
 
Kwenye gari la Polisi alipanda mwenyewe hawa watu wanatia hasira sana.
Hivi wanajimu humu si walituambia upi nzani utakufa kwa sababu awamu hii inachapa kazi hawana agenda?? Risasi za nini sasa?
Wanamaanisha kujipeleka kwake kukamatwa /kufanya kuanyiko lisilo halali hivyo ameyata mwenyewe
 
Hivi hii kitu inaingia akilini kweli, yaan hat kwa mtt wa miak 5 anawez kutambua hii sio sawa...!
 
87aa0f2e6ae05ba4eb9d6f5cdd0b977c.jpg
Kamanda wa Polisi wilaya ya Kinondoni, Jumanne Muliro amesema mgombea ubunge wa CHADEMA jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu hakukamatwa na Polisi, bali alijipeleka mwenyewe ili akamatwe wakati si mtuhumiwa.

Akizungumza na MCL Digital leo Frebuari 17, 2018, Kamanda Muliro amesema mgombea huyo alijipeleka mwenyewe kwenye gari la Polisi wakati si mtuhumiwa, akiamini kuwa kitendo hicho kitawafanya waandishi wa habari kumpiga picha ili ionekane kuwa amekamatwa.

"Hizi ni hadithi za abunuwasi. Haya mambo ya kufikirika hayatakiwi kabisa. Yeye ameshapiga kura akae asubiri matokeo", amasema Muliro.

"Amelazimisha kuchukuliwa na kuingia kwenye gari wakati si mtuhumiwa".

Timu ya waandishi wa habari ilishuhudia leo saa 6 mchana, Mwalimu akiondoka na Polisi katika Defender na kupelekwa katika kituo cha Magomeni ambapo alikaa kwa takribani robo saa na kuachiwa.

Mwalimu alifika katika kituo hicho baada ya kusikia taarifa za baadhi ya wananchi wa kata hiyo wakidai kuwa kuna mtu ameondoka na sanduku lenye kura, baadaye kukamatwa na Polisi akiwa na sanduku hilo.

Chanzo: Mwananchi
Du hii kalii aisee
 
Back
Top Bottom