Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,277
- 17,983
We are now living in a fully fledged Police State. Hatuna tofauti na Uganda Wakati wa Iddi Amin.Kamanda wa Polisi wilaya ya Kinondoni, Jumanne Muliro amesema mgombea ubunge wa CHADEMA jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu hakukamatwa na Polisi, bali alijipeleka mwenyewe ili akamatwe wakati si mtuhumiwa.
Akizungumza na MCL Digital leo Frebuari 17, 2018, Kamanda Muliro amesema mgombea huyo alijipeleka mwenyewe kwenye gari la Polisi wakati si mtuhumiwa, akiamini kuwa kitendo hicho kitawafanya waandishi wa habari kumpiga picha ili ionekane kuwa amekamatwa.
"Hizi ni hadithi za abunuwasi. Haya mambo ya kufikirika hayatakiwi kabisa. Yeye ameshapiga kura akae asubiri matokeo", amasema Muliro.
"Amelazimisha kuchukuliwa na kuingia kwenye gari wakati si mtuhumiwa".
Timu ya waandishi wa habari ilishuhudia leo saa 6 mchana, Mwalimu akiondoka na Polisi katika Defender na kupelekwa katika kituo cha Magomeni ambapo alikaa kwa takribani robo saa na kuachiwa.
Mwalimu alifika katika kituo hicho baada ya kusikia taarifa za baadhi ya wananchi wa kata hiyo wakidai kuwa kuna mtu ameondoka na sanduku lenye kura, baadaye kukamatwa na Polisi akiwa na sanduku hilo.
Chanzo: Mwananchi
Hata ushahidi wa video clips wanaona ni uongo.