Polisi yakana kumkamata Salum Mwalimu, yadai alijipeleka mwenyewe ili akamatwe

Huenda bangi inayokamatwa na maasikari huwa wanaiweka stoo kwa matumizi yao,maana kuna mambo mengine hata wao wanaona aibu kuyazungumza mbele za watu
Haa haa.. Kwani huoni wakienda kuchoma mashamba ya bangi ule mvuke wake inakuwaje
 
Upumbavu,upumbavu,upuuzi huu yafaa waelezwe vichaa.sasa polisi walikubali vipi kumchukuwa MTU ambaye hawana mpango nae?Tulishuhudia polisi wakimshusha MTU ndani ya gari na kusema huyu siyo muhusika.Hivi kwanini Watu wanakuwa waongo kiasi hiki? Kwanini mwalimu hawakumshusha?Inamaana mtu akipanda gari la polisi wanamwacha tu kisa ameamua mwenyewe kupanda?Acheni uongo.Nafikiri albadiri inafanya kazi.
 
87aa0f2e6ae05ba4eb9d6f5cdd0b977c.jpg
Kamanda wa Polisi wilaya ya Kinondoni, Jumanne Muliro amesema mgombea ubunge wa CHADEMA jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu hakukamatwa na Polisi, bali alijipeleka mwenyewe ili akamatwe wakati si mtuhumiwa.

Akizungumza na MCL Digital leo Frebuari 17, 2018, Kamanda Muliro amesema mgombea huyo alijipeleka mwenyewe kwenye gari la Polisi wakati si mtuhumiwa, akiamini kuwa kitendo hicho kitawafanya waandishi wa habari kumpiga picha ili ionekane kuwa amekamatwa.

"Hizi ni hadithi za abunuwasi. Haya mambo ya kufikirika hayatakiwi kabisa. Yeye ameshapiga kura akae asubiri matokeo", amasema Muliro.

"Amelazimisha kuchukuliwa na kuingia kwenye gari wakati si mtuhumiwa".

Timu ya waandishi wa habari ilishuhudia leo saa 6 mchana, Mwalimu akiondoka na Polisi katika Defender na kupelekwa katika kituo cha Magomeni ambapo alikaa kwa takribani robo saa na kuachiwa.

Mwalimu alifika katika kituo hicho baada ya kusikia taarifa za baadhi ya wananchi wa kata hiyo wakidai kuwa kuna mtu ameondoka na sanduku lenye kura, baadaye kukamatwa na Polisi akiwa na sanduku hilo.

Chanzo: Mwananchi[/QUOTE

Hayo maneno yamesemwa na kamanda "Zero"?
 
HAYA WENZETU WALISHAFANYA MWAKA 1500 CC WAAFRKA NDO TUNAONA WAJANJA.NAONA WALIPEWA MAAGZO KUTOKA JUU WAMWACHIE.
 
Kama huo utaratibu upo, itakua raha sana...

Unapiga mkono gari ya polisi, unapanda unaawambia nashukia kituo cha mbele hapo...


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom