Polisi wetu na huduma za makengeza

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
Ulishawahi kupata tatizo na ukahitaji msaada wa polisi? Au ulishwahi kufika kwenye kituo chochote cha polisi kwasababu zozote zile na ukaona jinsi huduma zinavyotolewa kwa matabaka na upendeleo wa wazu kabisa?

Kama huna hela kituo cha polisi huna thamani yeyote, lugha inayozungumzika pale ni lugha ya pesa, rushwa na hongo za wazi kabisa hakuna kificho, hasa kama kesi yako inahusiana na pesa nyingi aidha kuibiwa/ kutapeliwa au kutarajiwa kulipwa utaambiwa tu wazi kuwa kupata huduma ya namna hiyo ni lazima uwe na kiasi Fulani mfano halisi ni kupata nyaraka kwa ajili ya kwenda kulipwa bima ishu inayohusu ajali

Tunaweza kuwalaumu polisi wetu lakini tatizo ni la kimfumo zaidi, hatukuwa na matabaka zamani kila huduma ilikuwa inatolewa kwa jumuiya nzima, lakini siku hizi mambo ni tofauti huduma muhimu za kijamii zina matabaka hospital zipo za kulipia na zipo za serikali, shule na vyuo kuna matabaka mahoteli mpaka sehemu za starehe, japo si wazi sana lakini pesa yako ndio itakubagua tuu, utaenda unapomudu.

Bahati mbaya sana sana matabaka yote hayo yanakuja kukutana sehemu moja yanapotokea matatizo ya kipolisi na kisheria. Ni polisi pekee wameshindwa kuwa na vituo kulingana na bei ya mtu hivyo mtu wa being fulani aliyezoea kupata huduma ya daraja la kwanza alifika polisi hupata shida na hivyo kuamua kutumia pesa kupata huduma anayostahili.

Na polisi wetu kwakuwa nao ni binadamu na nje ya mavazi yao rasmi ya kazi wana changamoto za kawaida kabisa za kibinamu huangukia kwenye mtego huu kwa urahisi kabisa na kujikuta wanatoa huduma kwa macho ya makengeza, ni mfumo ndio umewajenga.
 
Nchi hii kama hauna pesa popote pale hautapata huduma sitahiki haijalishi kitengo gani au una haki na hiyo huduma.
Huu wote ni mfumo wa uongozi tulionao kuanzia kwenye familia hadi kwa mkuu wa nchi.
 
Tatizo mfumo,,, kila sector nowdays kuna corruption, nepotism and redtape na serikali inajifanya kipofu!
 
Umaskini, Mfumo mbovu wa uongozi, siasa chafu na rushwa ndio iliyotufikisha hapa.
 
nimekuelewa mkuu. sekta zote ni matatizo hasa za serikali

Tukifanikiwa kubadilisha uongozi wa kisiasa tukawa na kitu kipya kabisa mengi yatabadilika...! I mean kuiweka ccm pembeni kupitia sanduku la kura
 
Kuliwahi kuwa na Idea kuwa Polisi watumie Mashine za TRA wanapotoza faini, sijui kwanini haijafanyiwa kazi ,aama ingepunguza tatizo la kuandikiwa Notification bila risit, ukiomba risiti wanakua wakali balaaa.
 
Hapa kuna mtu kanitapeli laki 4 huu mwaka sasa sasa, nafikilia kwenda polisi ila kuna mtu kanipa onyo nisiende, maana hiyo hela nitagawana na polisi nusu kwa nusu, kumbe kweli jamani, sio siri niliogopa maana kutoa laki 2 kumpa polisi si mchezo, nimebaki nagombana nae tu, sijui hata nikamshtaki wapi, hebu nipeni ushauri katika hili ndugu zangu, ili nichukue hatua nyingine juu huyu mtu
 
Hapa kuna mtu kanitapeli laki 4 huu mwaka sasa sasa, nafikilia kwenda polisi ila kuna mtu kanipa onyo nisiende, maana hiyo hela nitagawana na polisi nusu kwa nusu, kumbe kweli jamani, sio siri niliogopa maana kutoa laki 2 kumpa polisi si mchezo, nimebaki nagombana nae tu, sijui hata nikamshtaki wapi, hebu nipeni ushauri katika hili ndugu zangu, ili nichukue hatua nyingine juu huyu mtu

Upo Dar? Maeneo gani? Hiyo pesa ina ushahidi wa maandishi? Kachukue RB kwanza
 
Back
Top Bottom