Hii picha ina majibu mengi sana;
Polisi wanaweza kutumia kila mbinu kujitetea lakini kwa hili wamecheza faulo mbaya...Jaribu kuiangalia kwa makini hii picha na kusoma kitendo cha kila askari. Utagundua kuwa wapo waliokuwa wanawazuia wenzao kuendeleza kipigo kwa mwandishi huyo(angalia movement za askari kanzu mwenye fulana ya bluu, pia kuna askari mwenye kofia nyekundu asiye na kikinga risasi, pia kuna askari upande wa pili mwenye kofia nyeusi)....
Hivyo huyo mwandishi alipigwa tena kipigo kibaya na ndio maana yupo chini akiwa hajiwezi.
Angalia pia mkono wa kulia wa huyo mwandishi, katika kiganja chake ameshika kamera, kwa hilo tu polisi walitakiwa watoe ulinzi maana kitendo cha kuwa na kifaa kama kamera ni ishara kuwa jamaa alikuwa ni mwanahabari naalikuwa katika harakati za kazi.
Halafu pia ukijaribu kuivuta picha kwa karibu utaona kuna kitu kama moshi kinafuka karibu kabisa na mwili wa marehemu na moshi huo unaelekea moja kwa moja katika mtutu ulioelekezwa kwake, moshi huo bilashaka ni matokeo ya bomu lililopigwa na huyo askari wa kushoto kabisa aliyeelekeza mtutu wake kwa marehemu.
Unaweza vipi kuua binadamu mwenzako halafu usiku ukapata usingizi? Jeshi la kishetani hili
Tume ya nini wakati polisi wenyewe wanaonekana wanampiga virungu marehemu hapo?
Kama polisi hawakukusudia kummwua Daudi Mwangosi (RIP) wanaonekana kwenye picha wachukuliwe hatua.
Yaani unaua halafu unajiundia tume ujichunguze...hawa jamaa ni minduku kweli...
Hapo kama IGP ana akili timamu alitakiwa huyo RPC mpaka saizi awe ananyea debe na kutaja vijana wake wengine hao walio mzunguka
Mafreemasons wanatoa watu kafaraTume ya nini wakati wanahabari wamemuonyesha muuaji ,picha zinajionyesha ,mahala walipomuulia panajulikana na aliyewatuma ni Jakaya Kikwete na shemeji yake IGP Saidi Mwema,mapepo na majini yao ni kwamba kable ya 2015 kwa kutumia polisi watakuwa wameua viongozi wote wa chadema na wananchi kama laki moja huo ndio ukweli manake dhamira yao inaonekana wazi sasa
Ni hao wateule wa RaisMimi sio mtaalam wa mabomu ila najua mabomu ya machozi huwa hayalipuki, hata likitua mbele yako!
Sasa hiyo live bomu nani alikuwa amebeba?
Huwezi Kuua mti kwa kukata majani au matawi Bali unaweza Kuua mti kwa kukata shina na mizizi yeye IGP angejiweka mwenyewe lockup Kama mshitakiwa namba moja na wengine wafuate