Polisi waua tena

Kama kawaida, vyombo vya dola vikiongozwa na polisi huko Geita vimeripotiwa kumuua mtu mmoja na kuwajarehi wengine kwa risasi za moto wakati raia hao wa kata moja ya Geita kuandamana kwa amani wakishinikiza diwani wao ajiuzuru baada ya diwani wao huyo kushiriki katika baraza la madiwani kumwondoa kiongozi aliyesadikiwa kutetea maslahi ya wananchi. Wananchi wanauliza, sisi ndio tuliomchagua diwani wetu na tuna haki ya kumwondoa tumepigwa na polisi kwa nini?
Source; ITV saa 8 usiku

Kwa hali hii sina sababu ya kutoamini kwamba polisi wetu hawafundishwi namna ya kukabiliana na waandamanaji.

Bila shaka wao wanafundishwa kuua tu. Inawezekana vipi watu wanaandamana kwa amani halafu polisi wanafika tu na kuanza kuwashambulia kwa risasi? mtu mwenyewe aliyeuawa ameripotiwa kupigwa risasi kichwani, sasa hapa kwanini tusiamini kwamba hawa mapolisi wamefundishwa kuua raia?

Shame on you police force, you are just too unprofessional!!
 
watanzania tuunganishe nguvu lakini tukiendelea kutengana ooh, arusha ni wahuni haya leo geita, juzi ili kuwa tabora na nyamongo tukawaita majambazi lakini tulikuwa tayalikutoa zaidi ya mil 3 kwa kila jambazi iliziwasaidi kwenye mazishi sijui huruma hii imeanza lini..je kesho wataua wapi wasingizia nini..?

mkuu hapo kwenye red itawezekana endapo tutajiuliza na kujibu swali la hapo kwenye blue....tatizo letu tunaangalia leo tu, hatujiulizi kesho na keshokutwa itakuwaje kwenye maeneo mengine ya nchi!!tatizo lingine tulilonao tunaona ni illegal kudai haki zetu, hii inachangiwa na ignorance yetu!!
 
Jamani hivi hawasomi Police general order (PGO) zao zinazowaongoza katika kazi zinasemaje? au ndio bora liende.

Poleni sana
 
Kwenye UKWELI uongo ujitenga serikali ya magamba kila siku imekua ikisingizia Chadema ndio wavunjifu wa aman , tumeona arusha, mbozi, tunduma,nyamongo, tabora nk haya leo Geita,aingiii akilini kabisa Kikongwe wa miaka 90 unampiga heti analeta vujo tena umemwingilia kwake kwa kuvunja mlango , simply amefuatwa kwake na polic ndio waalifu hata kama aliandamana, ndio maana watu wengi awalipendi jeshi la police ila basi tu awana la kufanya . Siku mmmoja ikatokea bahati mbaya mvamizi akavamia nchi hii aki ya nani watu wanaweza shirikiana na mvamizi kutoa tahalifa na hata kuwasaidianki mbinu
 
Mimi sasa naona serikali legelege ndiyo shida kubwa iliyonayo ni kushindwa kujitambua ya kwamba imeshindwa uongozi. Lakini hebu tuombeni MUNGU atupe uzima na tuone mwisho wao ni wapi.:whoo::whoo::whoo::whoo:
 
Yap..niiona hiyo kwenye taarifa ya habari. Licha ya huyo aliyeuwawa kijana mwingine alichapwa risasi ya mkononi amelazwa hospitali, bibi mmoja alikula kisago na nyumba yake ikavunjwa mlango eti kuna watu wamejificha ndani ya hiyo nyumba ya huyo bibi.
 
tusiwachekee hawa polisi wengi vihiyo tunaishi nao hata shoka la kichwa mpe tu msg itafika kwa dkt masuti alaf nao wataandamana kwa kutaka makazi bora tuone nani atawapiga risasi? Masaburi ya nguruwe hawa
 
Back
Top Bottom