Polisi waua Tabora

kayogo

Member
Sep 15, 2010
75
42
Kijana mwenzetu Amani Msimbe mfanyabiashara wa matunda soko kuu la Tabora, ameuwa na POLICE wakituo kikuu baada ya kumpa mateso makali Mithili ya jambazi sugu.

MSIMBE ambae alikamatwa tarehe 24 baada ya kumpiga mdeni wake , rafiki zake Wanasema Wakati anakamatwa aliwasumbua police kwavile alikuwa amelewa pengine ndio kisa cha Police hao kumshushia kipigo na mateso makali walipomfikisha central.

Chaajabu walipoona haliyake mbaya wakampigia mkewe simu aje amdhamini wakati mwanzo walisha mnyima dhamana. Alipofikishwa hospital hakuchukua muda akafariki, Jambo lililopelekea vurugu kubwa, baada ya wafanyabiashara wenzie wa sokoni kugoma mwili usitolewe wodini mpaka aje mkuu wa mkoa.

Baadhi ya viongozi walifika na kuokoa jahazi na kushusha jazba za vijana ss mwili uko chumba cha kuhifadhia maiti. Huku uvumi ukiwa umezagaa eti Police wameandika aligongwa na gari.
 
Polisi kuwa weredi kama wezenu wa nchi za Ulaya mmeshindwa...?
 
Kumbe mtuhumiwa alikuwa anawasumbua polisi.!
Halafu anasingizia pombe?
P.T (Piger too)
 
Kumbe pado wanatekeleza ile kauli "Wapigwe tu. Tumechoka!". Nilifikiri wamesahau kama wanavyosahau mafunzo.
 
Kijana mwenzetu Amani Msimbe mfanyabiashara wa matunda soko kuu la Tabora, ameuwa na POLICE wakituo kikuu baada ya kumpa mateso makali Mithili ya jambazi sugu.

MSIMBE ambae alikamatwa tarehe 24 baada ya kumpiga mdeni wake , rafiki zake Wanasema Wakati anakamatwa aliwasumbua police kwavile alikuwa amelewa pengine ndio kisa cha Police hao kumshushia kipigo na mateso makali walipomfikisha central.

Chaajabu walipoona haliyake mbaya wakampigia mkewe simu aje amdhamini wakati mwanzo walisha mnyima dhamana. Alipofikishwa hospital hakuchukua muda akafariki, Jambo lililopelekea vurugu kubwa, baada ya wafanyabiashara wenzie wa sokoni kugoma mwili usitolewe wodini mpaka aje mkuu wa mkoa.

Baadhi ya viongozi walifika na kuokoa jahazi na kushusha jazba za vijana ss mwili uko chumba cha kuhifadhia maiti. Huku uvumi ukiwa umezagaa eti Police wameandika aligongwa na gari.

Mkuu we mnafiki sana! Mbona majuzi hapa polisi wameuawa Newala hukukimbilia jamvini kuleta habari? Hii ya mbabe aliyepiga watu na kugoma kukamatwa umeiwahisha kishenzi! Bavicha kila tukio ni mtaji! Haya mtaji mwingine huo mpeni Slaa!
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Back
Top Bottom