Polisi watoa tamko kuelekea mechi ya Simba Vs USGN

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Kuelekea mchezo wa Simba dhidi ya USGN ya Niger, Jumapili Aprili 3 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, Jeshi la Polisi limesema liko tayari na limejipanga kwa ajili ya kulinda usalama siku hiyo ya mchezo huo ambao utaanza saa 4:00 Usiku.

Mchezo huo wa Kundi D katika Kombe la Shirikisho la Afrika utaweka rekodi ya kuwa mchezo wa kwanza ngazi ya klabu kuanza kuchezwa muda huo katika Uwanja wa Mkapa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro J. Muliro amesema wamejipanga kuhakikisha usalama unaimarishwa kwa kiwango cha juu kwa mashabiki na wachezaji, ulinzi ndani na nje ya uwanja utakuwa katika kiwango cha juu.

"Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam linatoa tahadhari kuwa mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vilivyo kinyume na sheria au taratibu ndani au nje ya uwanja atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria," - Kamanda Muliro.
 
Asante sana Muliro Muliro boy...!!!
Weka jiwe wapelekee moto
 
Back
Top Bottom