Polisi wathibitisha kumkata Catherine Ruge wa CHADEMA

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
Jeshi la Polisi, Mkoa wa Mara limemkamata Katibu wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), Catherine Ruge.

Ruge amekamatwa leo Jumamosi, Septemba 24, 2022, muda mfupi baada ya kufika Mjini Musoma, Mkoa wa Mara kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari.

Lengo la mkutano huo ni kutoa msimamo wa familia za ndugu waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi Wilaya ya Serengeti, mkoani humo kwa tuhuma za ujambazi.

Waliouawa katika tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Septemba 23, 2022 ni Mairo Togoro (56), mkazi wa kijiji cha Majimoto, Mwise Simon (54) mkazi wa kijiji Nyamihuru na Mugare Mokiri mkazi wa kijiji cha Nyamikobiti wote wa wilaya ya Serengeti ambaye ni mjomba wake, Ruge.

Polisi walidai watu hao walikamatwa kwenye operesheni iliyofanywa kwa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara, Mwanza, Simiyu na Kanda maalumu ya Tarime/Rorya kufuatia matukio ya ujambazi wa kutumia silaha, matukio yanayodaiwa kufanywa na watuhumiwa hao wakishirikiana na wenzao.

Leo Jumamosi, Ruge alikuwa azungumze na waandishi ambapo baada ya kuwasili katika eneo hlio, aliwakuta askari wawili wa kike na wa kiume ambao baada tu ya gari lake kuwasili katika uwanja huo alitakiwa kupanda kwenye gari walilokuwa nalo askari hao agizo ambalo aligoma kulitii.

"Wananiambia nipande kwenye hilo gari kwanza gari lenyewe silijui na hao watu wenyewe siwajui, wananiambia wameagiza difenda ndio nasuburi hapa ili niondoke nao," amesema

Askari mmoja alisikika akimuelekeza dereva wa gari la polisi walipo ili waje kumkamata Ruge na baada ya muda mfupi gari la polisi lililoandikwa ubavuni OCD- Serengeti ilifika eneo hilo kisha askari wa kike aliyekuwepo eneo hili alikwenda kumgongea Ruge kwenye gari lake kumtaka ashuke.

Baada ya kushuka Ruge pamoja na askari huyo wa kike waliongozana hadi kwenye gari la polisi na kuondoka katika eneo hilo huku wakitanguliwa na gari lilikuja kumkamata awali lililokuwa na namba binafsi za usajili aina ya Toyota Kulger.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara (RPC), Longinus Tibishubwamu amesema Ruge amechukuliwa kwaajili ya mahojiano juu ya tuhuma alizozitoa dhidi ya jeshi la polisi na Serikali kuhusu mauaji hayo.

"Hatujamkamata, tumemchukua kwaajili ya mahojiano, tunataka athibitishe juu ya tuhuma alizozitoa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, hapo anakwenda kuhojiwa tu kisha tutamuachia na mtaendelea na mkutano wake na waandishi," amesema Tibishibwamu.
 
Nilijua tu, kumbe sio panyarodi lakini ni watuhumiwa wengine waliopotezea uhai wao mikononi mwa polisi, kama polisi wameacha kufuata sheria wasikasirike kuitwa majambazi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom