Polisi wapiga stop maandamano ya wanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wapiga stop maandamano ya wanafunzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpaka Kieleweke, Jan 23, 2009.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Jeshi la Polisi limeyapiga marufuku maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika ya wanafunzi wa vyuo vikuu DSM siku ya kesho jumamosi.

  Wametoa sababu eti kuwa maandamano hayo yatahatarisha amani ya nchi na hivyo wasithubutu kuandamana kama walivyokuwa wamepanga kuyafanya.

  uhuru wa kujieleza uko wapi?
  uhuru wa kutoa maoni uko wapi?
  Jeshi la Polisi kwa masilahi ya nani?
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  Wanaogopa nchi haitakalika? Too sad!
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Binafsi sikuwa na matarajio ya kwamba polisi watakubali kuwaachia wanafunzi wa vyuo vikuu waandamane.
  Kwanza polisi wenyewe wanafanya kazi kwa maelekezo ya CCM na jeshi lenyewe la polisi haliko huru katika kufikia maamuzi.Yangekuwa maandamano ya kuisifu serikali kwa kuwathibiti watanzania wasisome elimu ya juu ungemuona kova haraka haraka mbele ya waandishi wa habari.
  Kwasababu wakisema eti yatahatarisha amani ya nchi wanatakiwa waseme hiyo amani itahatarishwaje, nadhani wameshituka kuwa sasahivi watanzania wengi wamegundua hila za serikali kuivuruga elimu ya juu na watanzania wengi walikuwa tayari kuwaunga mkono kwenye maandamano na watu waliokuwa wameombwa/wamealikwa kuyapokea kila mmoja anafahamu uelewa wao na misimamao yao.Na ukijumlisha kuwa CHADEMA.net pamoja na kituo cha sheria na haki za binadamu(LHRC)wametangaza kuwatetea yaani hapo ndio kabisaaaa makamba ameshindwa kupata usingizi amemvutia waya tu JK kule pemba naye akamwambia kova zuia hao watu kuandamana.Kama raisi anakwenda ziara ya kiserikali pemba halafu anaanza kuwabeza wapinzani huoni kuwa hapo hakuna uhuru hata kidogo.Lazima wale wanaopingana na serikali yake watakandamizwa tu.Eti anasema wanaweza wasishike madaraka milele, hakianani kweli ulevi wa madaraka umemshika vibaya JK.
   
 4. G

  Ghwakukajha Senior Member

  #4
  Jan 23, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kwa nilivyomsikia kamanda Kova(kupitia TBC 1) amesema kuwa walioenda kuomba kibali/ulinzi ni kuwa walisema wao ni asasi(organization),lakini katika ufuatiliaji wao wamegundua kuwa sio asasi bali ilisajiliwa kama kampuni......Hvyo maandamano hayo ni batili.
   
 5. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Msinifanye nicheke. Kwani organization ni nini?

  Kama hao TSNP wamesajiliwa kama kampuni basi ni kampuni isiyotengeneza faida kwa hiyo ni organization.

  Hivi Tanzania si ina organization nyingi tu za namna hiyo zilizosajiliwa kama kampuni mathalani HAKI ELIMU, LEAT nk.

  Na nakumbuka HAKI ELIMU walisema wamesajiliwa kama kampuni kuepusha kufutwa na serikali ambayo imekuwa ikizufuta ovyo ovyo associations pale mambo ya ndani.

  Hebu mtoa habari tueleze undani wa kinachoendelea

  .....ndiyohiyo
   
 6. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Daily News; Friday,January 23, 2009 @20:06

  Habari nyingine
  Dk. Kashillilah ateuliwa Katibu wa Bunge
  TRA yaanza kuwabana wenye mizigo bandarini
  Sheria ya Mashirika ya Umma yaikwaza Bunge
  ATCL yaanza safari kwa abiria wa ‘kuridhisha’
  Makamba amlilia Mzee Waryuba
  CCM yaahidi Tsunami, CUF yalia faulo Mbeya
  Wanafunzi 75 kuburuzwa mahakamani
  Mabasi 15 yasimamishwa
  Mgawo wa umeme Dar haupo
  Wilaya 30 bado zakabiliwa na ukoma

  Wakati wanafunzi watano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani, ambao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shitaka la kufanya mkusanyiko usio halali, wameachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana, Polisi imezuia maandamano yao yaliyokuwa yafanyike leo.

  Maandamano hayo yaliyokuwa yameandaliwa na Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) kupinga sera ya uchangiaji elimu ya juu na kutaka wanafunzi wote warejee chuoni, yalikuwa yaanzie Ubungo Mataa hadi Jangwani.

  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema maandamano hayo yamezuiwa kwa sababu mtandao huo si halali, bali ni kampuni iliyosajiliwa kwa jina la Tanzania Student Network in Programme Limited.

  Alisema kampuni hiyo ilisajiliwa kwa cheti namba 4286, hivyo barua ya TSNP siyo sahihi na ilikuwa na lengo la kuipotosha Polisi kuwa mtandao wao umesajiliwa wakati walikuwa wakitumia namba hiyo ambayo imesajiliwa kama kampuni.

  Aidha, alisema kutokana na kasoro hizo, maandamano hayo kwa kutumia asasi hiyo yatakuwa ni kinyume cha sheria kwani asasi hiyo haipo kisheria mpaka yatakapofanyika marekebisho.

  Januari 19 mwaka huu, viongozi wa wanafunzi hao waliwasilisha polisi barua isiyo na kumbukumbu wakiomba waruhusiwe kufanyika kwa maandamano hayo. Kwa upande mwingine, wanafunzi walioachiwa jana walikaa rumande kwa siku mbili na walitimiza masharti yaliyowataka kuwa na mdhamini mmoja ambaye ni mwajiriwa serikalini na mwenye barua ambaye atasaini dhamana ya Sh 500,000.

  Wanafunzi hao walioshitakiwa kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isiyo halali huku wamebeba mabango yaliyoashiria uchochezi na uvunjifu wa amani ni Anthony Machibya (26), Owawa Juma (26), Sabinian Pius (25), Titus Ndula na Paul Issa (24).

  Pia walitakiwa kutokwenda maeneo ya chuo bila ruhusa ya mahakama pamoja na kuripoti katika Kituo cha Polisi Oysterbay kila Ijumaa na kusaini kwenye kitabu na washitakiwa hao kutokusanyika au kufanya mikutano bila kibali.
   
 7. G

  Ghwakukajha Senior Member

  #7
  Jan 23, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  I hope alichokuwa anataka kuimply ni kuwa kama wanataka kuandamana then waombe tena but this time waonyeshe kuwa wao ni kampuni na si organization.It might be a delay tactic,who knows??
   
 8. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Tunakokwenda siko kwani kama inafikia mahali hata polisi wenyewe hawajui maana ya organiozationi na kampuni basi wote tuu vipofu ama hatujui kusoma na kuelewa maana ya maneno .

  Ni wakati muafaka sasa Makamba kuja na kufafanua maana ya maneno hayo ndipo Kova ataweza kuelewa na akielew3a ataruhusu maandeamano hayo.
   
 9. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  -

  Hili ndio lilikuwa tamko lao walilotutumia News Room kwa email. Mbona hata Editors Forum imesajiliwa kama Kampuni?

  TSNP-

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  YAH: KUFUTIWA UDAHILI KWA WANAFUNZI WA ELIMU JUU TANZANIA NA KUFUTWA KWA UMOJA WA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (DARUSO)


  TSNP ni mtandao wa wanafunzi Tanzania ambayo ni asasi isiyo ya kiserikali na isiyo ya kibiashara iliyosajiliwa chini ya sheria ya makapuni tarehe 23 octoba 2001 na kupewa namba ya usajili (No.42386),kwa malengo ya kutetea wanafunzi Tanzania kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu na kuwaunganisha wanafunzi wote katika kudai haki zao ndani ya Tanzania.


  Katika kipindi cha miezi miwili kuanzia novemba 2008 mpaka januari 2009 baadhi ya vyuo vikuu vya umma nchini vilifungwa kutokana na madai ya wanafunzi ya kutaka serikali kuwalipia ada za masomo vyuoni kwa asilimia mia (100%),katika kufikisha madai yao ya kupinga sera ya elimu ya uchangiaji,wanafunzi waliingia kwenye migomo ili kushinikiza serikali kutambua madai yao baada ya kutosikilizwa kwa njia ya majadiliano kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi .

  Katika kujibu madai ya wanafunzi,serikali iliwafukuza wanafunzi wote vyuoni na kufunga vyuo kwa muda usiojulikana,pia serikali ilitangaza kuwafutia wanafunzi wote udahili kama njia ya kutatua madai ya wanafunzi ya kupinga sera ya uchangiaji ya elimu ya juu ,kama hilo haitoshi,serikali ilitoa fomu zenye masharti magumu ya kuwarejesha wanafunzi vyuoni,fomu zilizowataka wanafunzi wote kulipa pesa zote wanazodaiwa vyuoni bila kujali au kurejea kilichosababisha wanafunzi hawa kugoma,pia serikali kupitia viongozi wa vyuo wametangaza kufuta umoja wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam (DARUSO).

  Mtandao wa wanafunzi Tanzania umesikitishwa na ubabe unaoendelea wa kuwashurutisha wanafunzi kwa kutumia fomu zilizoandaliwa bila kujali nafasi ya masikini ndani ya Tanzania,pia tunalaani kiburi cha waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi,wakuu vyuo vya elimu ya juu hasa chuo kikuu cha Dar es salaam wa kutotumia elimu yao kutatua madai ya wanafunzi na kujigeuza miungu watu kwa nafasi walizonazo.Tunapinga ubaguzi uliowazi unaofanywa na serikali,hasa wa kuwabagua masikini wa nchi hii kwa kuwazuia kurudi vyuoni kwa kutumia njia chafu na ya kidhalimu kuwa hawakutimiza vigezo vya fomu.

  Sisi kama mtandao wa wanafunzi Tanzania,tunawaambia uongozi wa chuo kikuu cha Dar es salaam kuwa uwepo wa DARUSO siyo kwa huruma wao bali ni kwa matakwa ya sheria ya vyuo vikuu na “chater” ya chuo ya 2007 ibara ya 23 (1) inayotambua uwepo wa uongozi wa wanafunzi,ieleweka wazi kuwa bado tunatambua uwepo wa DARUSO na uanzishwaji wake ulifuata misingi ya sheria na kufutwa kwake lazima upitie mkondo huo wa sheria chini uongozi wa wanafunzi na siyo utawala wa chuo hicho.Tunalaani udikteta unaofanywa na utawala wa chuo kikuu cha Dares salaam wa kuingilia jumuia za wanafunzi kwa malengo ya kukidhi masilahiy yao.

  MSIMAMO WETU
  1. Kwa kuwa waziri wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi ameshindwa kushugulikia madai halali ya wanafunzi,na amezidi kuwa vyanzo vya matatizo na kushindwa kusimamia wizara hii kwa manufaa ya taifa,tunamtaka ajiuzulu nafasi yake na kuichia watanzania wanaoweza kusimamia elimu kwa mustakabali na uhai wa taifa.
  2. Serikali iwarudishe wanafunzi wote vyuoni bila kuwazuia baadhi ya wanafunzi wanaotoka katika familia masikini walioshindwa kukidhi vigezo vya fomu vya kurudi chouni.
  3. Uongozi wa chuo kikuu cha Dar es salaam ujiuzulu mara moja kunusuru mustakabali wa chuo hicho kwa kuwa wameshindwa kukiongoza. Ubabe wa uongozi wa chuo hicho wa kujipa mamlaka ya kutangaza hali ya hatari ndani ya chuo hicho ni ya hatari kwa maisha ya wanafunzi chuoni hapo na unakiuka katiba ya jamhuri ya muungano na kumnyang’anya Mh. Rais mamlaka ya kutangaza hali ya hatari,kuhujumiwa kwa demokrasia ya umoja wa wanafunzi unadhihirisha ulevi wa madaraka usioweza kuvumilika kwa wanafunzi wote Tanzania.
  4. Tunamkumbusha Mh.rais Kikwete kuingilia swala hili, ili kulinusuru taifa la Tanzania na kuwakomboa wanafunzi wanaotoka katika familia masikini ambao ni wahanga wa sera ya uchangiaji wa elimu ya juu.
  5. Tunawakumbusha wanafunzi wote kufika katika vyuo vyao tarehe iliyotangazwa rasmi kwa kuanza masomo.
  6. Tunaliomba bunge la Tanzania kuipitia upya sera ya elimu ya juu ya uchangiaji ili kuweza kutatua mapungufu yaliyopo,Na ili kuweza kupunguza migogoro ya sasa na kuinusuru sekta ya elimu ya taifa la Tanzania,pia kusimamia serikali ili kuhakikisha wanafunzi wote wanarudi vyuoni.
  7. Tunawakumbusha wanafunzi wote wa chuo kikuu cha Dar es salaam kuwa DARUSO ipo na itazidi kwepo kwa sababu ipo kisheria na siyo kwa huruma ya utawala wa chuo,wanafunzi wote wazidi kuwa wamoja mpaka hapo madai yao yatakapo shughulikiwa kwa manufaa ya watanzania wote na wasikubali kuhamishwa kwenye madai yao ya kupinga mapungufu yaliyopo kwenye sera ya elimu ya uchangiaji.  HITIMISHO.
  Tunaiomba jamii ya watanzania kulitazama swala la wanafunzi wa elimu ya juu kwa umakini zaidi na kuungana na wanafunzi katika kurekebisha mapungufu yaliyopo kwenye sera ya uchangiaji ya elimu ya juu Tanzania.Tunaikumbusha serikali kutambua uhitaji wa watalaamu katika taifa hili na kutokuwa tayari kufutia wanafunzi udahili kwa kigezo cha kutoka katika familia masikini.Sisi mtandao wa wanafunzi Tanzania tunatambua madai ya wanafunzi kuwa ni halali na yanahitaji kushughulikiwa kwa manufaa ya umma wa taifa letu

  Imesahiniwa na

  ………………………
  Owawa Stephen
  Katibu.
  17/1/2009

  Nakala kwa
  1. Waziri wa elimu na mafunzo ya Ufundi
  2. Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam
  3. Spika wa Bunge la Tanzania
  4. Rais wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam (DARUSO)
   
 10. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kichekesho, Kova hajui maana ya organization. Kwani kampuni haiwezi kuittwa organziation? Mbona HAKI ELIMU wanaitwa taasisi au asasi? Hivi TGNP nao kwanini hawakatazwi kujiita Mtandao wa Jinsia? Kwani nao si Tanzania Gender Networking Programme Limited(TGNP) au Tanzania Gender Networking Programme Trust Fund?

  From Wikipedia, the free encyclopedia
  Jump to: navigation, search
  For other uses, see Organization (disambiguation).
  An organization (or organisation — see spelling differences) is a social arrangement which pursues collective goals, which controls its own performance, and which has a boundary separating it from its environment. The word itself is derived from the Greek word ὄργανον (organon [itself derived from the better-known word ἔργον ergon - work; deed - > ergonomics, etc]) meaning tool. The term is used in both daily and scientific English in multiple ways.

  In the social sciences, organizations are studied by researchers from several disciplines, the most common of which are sociology, economics, political science, psychology, management, and organizational communication. The broad area is commonly referred to as organizational studies, organizational behavior or organization analysis. Therefore, a number of different theories and perspectives exist, some of which are compatible, and others that are competing.

  Organization – process-related: an entity is being (re-)organized (organization as task or action).
  Organization – functional: organization as a function of how entities like businesses or state authorities are used (organization as a permanent structure).
  Organization – institutional: an entity is an organization (organization as an actual purposeful structure within a social context)
   
 11. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kova na makada wenzake wanazidi kujiumbua na kuongeza presha kwani wanajiona kama wao ndio wenye haki miliki za watanzania wote kudai haki zao za kimsingi.......
   
 12. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii ni statement yao nyingine walitutumia mwaka 2007

  TANZANIA STUDENTS NETWORKING PROGRAMME
  (TSNP)

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  YAH: MATANGAZO YA HAKI ELIMU

  Vyombo mbalimbali vya habari Julai 10 mwaka 2007
  vilieleza kwamba katika Kikao cha Bunge cha tarehe
  9-Julai 2007 cha kuchangia mjadala wa hotuba ya Wizara
  ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyowasilishwa Bungeni
  na Waziri wa wizara husika Mh. Margareth Sitta
  kulizuka mjadala wa kuipinga shirika la Haki Elimu
  kutokana na matangazo yake yanayoikosoa Serikali.

  Mjadala huo uliibuliwa na Mbunge wa jimbo la Kongwa
  (CCM) Mh. Job Ndugai ambaye alidai kuwa Shirika hilo
  linatoa matangazo yenye picha mbaya kwa Serikali kwani
  hayaonyeshi mafanikio yoyote ya elimu ya Tanzania
  yaliyofikiwa na Serikali.

  Pia, Mbunge wa viti Maalum-CCM Mh Janet Masaburi
  alidai kuwa matangazo ya Haki Elimu hayafurahishi hata
  watoto kwani yanajenga matabaka miongoni mwa jamii ya
  Watanzania kati ya watoto wa matajiri na masikini.

  Wabunge hao wote kwa pamoja wameona kuwa ni bora
  Shirika hilo likajisajili ili kuwa chama cha kisiasa
  kwani imekuwa ikiishambulia vikali Serikali katika
  sekta nzima ya elimu ya Tanzania.

  Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) kama wadau wakuu
  wa elimu Tanzania, inasikitishwa na kauli za wabunge
  hao dhidi ya shirika mtetezi wa wanafunzi wanyonge wa
  Kitanzania tunaosoma katika mazingira magumu.

  Sisi kama wanafunzi tunaamini kuwa dhima kubwa ya
  shirika la Haki Elimu ni kuonyesha uhalisia wa
  mazingira ya elimu katika Tanzania. Yale yote
  yanaonyeshwa katika matangazo ya Haki Elimu si mapya
  bali ni hali halisi yanaoyotokea katika shule nyingi
  za Tanzania.

  Ugumu wa usafiri kwa wanafunzi masikini, ukosefu wa
  vitabu vya kusomea na kufundishia, uhaba wa walimu,
  ukosefu wa nyumba za walimu, mishahara midogo ya
  walimu, ukosefu wa vitendea kazi ni baadhi ya
  matangazo ya Haki Elimu yanaonyesha hali halisi ya
  elimu ya Tanzania jinsi ilivyojaa ubabaishaji.

  Ijulikane kuwa Haki Elimu imekuwa mstari wa mbele
  katika kufanya tafiti mbalimbali zenye lengo la kuinua
  ubora wa elimu Tanzania. Hivyo matangazo ya Shirika
  hilo ni tokeo la tafiti mbalimbali yakinifu za shirika
  hilo. Mfano Haki Elimu Annual reports zinazotolewa
  kila mwaka zinaonyesha mafanikio ya tafiti za shirika
  hilo zenye lengo la kuinua kiwango cha ubora wa elimu
  Tanzania.

  Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) unaamini kuwa
  Haki Elimu haina dhamira mbaya juu ya Elimu ya
  Tanzania bali ni kama kikumbukishi chenye kutoa
  taswira kwa Serikali juu ya hali halisi ya elimu
  Tanzania.

  Ni wazi kuwa, kauli za wabunge hao zinaweza zikawa
  chachu kwa Serikali kuamua kuweka kikwazo kama
  ilivyokuwa katika kipindi cha Utawala wa awamu ya tatu
  ya Mh. B. Mkapa Rais Mstaafu aliyeifungia Haki Elimu
  ambapo baadaye iliruhusiwa kuendelea na matangazo yake
  na utawala wa awamu ya nne ya Mh Rais Jakaya Kikwete.

  Tunaamini kuwa kauli za wabunge hao hasa Mbunge wa
  Viti Maalum Mh Janet Masaburi aliyesema kuwa,
  nanukuu“…tunaomba Taasisi hizi zifahamu kuwa hii nchi
  ina wenyewe na hatupendi kuchezewa”(Mwananchi
  10/07/2007) Kauli hiyo inaonyesha kuwa kuna utabaka
  kati ya wenye nchi na wasio na nchi! Tunaamini kuwa
  Haki Elimu ni sehemu ya wenye nchi, kwani tunaamini
  kuwa kila raia halali wa Kitanzania ana hisa ya uraia
  ya kuwa mwenye nchi.

  Hivyo kauli ya Mbunge huyo ya kuonyesha kuwa nchi hii
  ina wenyewe ni kauli iliyo tata na nzito na yenye
  kuonyesha kuwa baadhi ya watu ni wenye nchi na wengine
  hawana umiliki wa nchi. Kwa mantiki hiyo ni vyema
  kauli ya Mh. Janet Masaburi airekebishe au kuikanusha
  kabla ya haijaleta madhara na fikra mbaya miongoni mwa
  wananchi wa Tanzania.

  Tunaamini kuwa nchi hii ni nchi ya watu wote wenye
  uraia halali, walio huru wenye kulindwa na misingi ya
  Katiba na sheria za nchi. Hivyo kila raia wa Tanzania
  ni mwenye nchi kwani nchi inajengwa na kumilikiwa na
  wananchi na siyo vinginevyo.

  Misingi ya utawala bora wenye kuzingatia Katiba na
  Sheria za nchi zinampatia mtu, kikundi halali, au
  taasisi uhuru wa kupata habari, kutoa maoni kulingana
  na sheria na kanuni zilizopo, hivyo ni wajibu na Haki
  Elimu kutumia uhuru huo ipasavyo katika kuwapatia
  watanzania hali halisi ya sekta ya Elimu hapa nchini.

  Tunaamini kuwa baadhi ya watu wenye mawazo kama ya
  wabunge hao ni watu wenye kulenga kukaribisha mawazo
  na mfumo udikteta na kubomoa demokrasia iliyo ya
  kweli.

  Hivi karibuni kumezuka wimbi la watu au kikundi
  kinachozungumza ukweli wenye uhalisia katika jamii
  unaonekana ni upinzani. Mfano Mgomo wa wanafunzi wa
  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sokoine kwa kuipinga
  sera ya uchangiaji katika elimu ya juu walionekana ni
  wapinzani. Hivi haiwezekani kuwa kati na kuzungumza
  ukweli bila kupendelea upande wowote.

  Nchi nyingi zilizokuwa na misingi ya udikteta zilikuwa
  na kazi ya kuzifungia taasisi mbalimbali,
  kuzishinikiza wafate mawazo yao kwa manufaa yao
  binafsi na siyo kwa manufaa ya umma. Hivyo basi,
  mawazo ya wabunge hao yamelenga katika kuimarisha
  maslahi yao au ya chama chao pasipo kuangalia maslahi
  ya watanzania kwa ujumla, kwani Haki Elimu ipo kwa
  maslahi ya Watanzania wote pasipo kuangalia itikadi
  zao za kisiasa, kidini au kikabila.

  Hatuwezi kuendelea kuwa na asasi zisizo za kiserikali
  zenye midomo na fikra za kusemea vyama vya kisiasa,
  bali ni jukumu la asasi zote kama Haki Elimu kusimamia
  kweli kwa manufaa ya Watanzania wote kwa ujumla.
  Hatuwezi kuendelea kusema elimu ya Tanzania ni nyeupe
  wakati imejaa weusi, hatuwezi kusema kuwa Tanzania ni
  safi wakati imejaa uchafu. Sisi kama wanafunzi tunaona
  kuwa elimu ya Tanzania inaweza kuwa bora endapo
  mapungufu yatapatiwa ufumbuzi.

  Ni fikra potofu kwa utetezi wa hoja ya Mbunge Mh. Job
  Ndugai kwa kuonyesha ulinganisho wa Haki Elimu na
  matangazo ya yaliyokuwa yanatolewa nchini Zambia
  yalivyopelekea kuangaushwa kwa utawala wa
  Rais Keneth Kaunda na chama chake cha UNIP. Ijulikane
  kuwa Keneth Kaunda aliangushwa madarakani kutokana na
  utawala mbovu. Ni wazi kuwa Wabunge hao wametoa
  angalizo kwa Serikali ya CCM kuwa wanaweza kuangushwa
  na matangazo yanayotolewa na Haki Elimu kama
  ilivyokuwa nchini Zambia.

  Ni vyema Serikali, Wabunge na watu wenye fikra kama
  hizo waache mara moja kushindana na Haki Elimu badala
  yake wabuni njia chanya mbadala ya kupambana na
  mapungufu yanayotajwa katika matangazo ya Haki Elimu.

  Sisi kama Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP)
  tunapenda kuungana na Haki Elimu na tunaunga mkono
  matangazo yote yanayotolewa na Haki Elimu yenye lengo
  ya kukuza elimu ya Tanzania na siyo vinginevyo.
   
 13. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2009
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna mengi ya kujifunza kwenye hili kwani serikali kwa kushirikiana na polisi wanadhani kuwa wanaweza kuwanyamazisha watanzania wote kwa wakati mmoja , lazima wajifunze kuwa tz ya leo sio ile ya jana .

  Kuna mambo mengi sanha yanaendeloea kwenye Taifa hili na hakika yatakapotoka hadharani basi kuna mengi ya kujifunza.......
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Mkuu MK heshima mbele,

  - Hapa ungeifikisha ripoti kwanza kama ilivyo, halafu ndio utoe maoni yako maana ulivyoiweka hii kitu haijakaa sawa, tusingependa uhuru wa kujieleza ukandamizwe, lakini ni vyema pia tukaripoti ukweli exactly kama ulivyo kwanza, maana hapa inaonekana kuwa sheria inasema ili uandamane unahitaji kuomba kibali na watoaji vibali wana haki kisheria ya kukubali au kukataa kutoa kibali hili pia tumeliona dunia nzima.

  - Ninasema hivi kwa sababu ninaamini kuwa Tanzania tulishavuka haya ya kunyimana kibali bila sababu, tumeona maandamano mengi sana yakuruhusiwa kufanyika sasa Why this one? Hawa vijana heunda hawakutimiza masharti yanayotakwia kisheria ili kupewa kibali, sasa wayafanyie kazi na kuomba tena.
   
 15. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  NI wapi Tunakwenda mbele ni giza zito
   
 16. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu FMES,
  I absolutely agree with you kwamba kule kwa kunyimana vibali vya maadamano tulikwishapita muda mrefu. Tumeona maandamano mengi na mengine yalikuwa very sensitive.

  Mimi binafsi ni mmoja wa waumini wa mawazo huru bila ya kuzuiwa au kuingiliwa unnecessarily. Lakini pia ninapinga namna yeyote ile ya ubabe na ukaidi usiokuwa na maana badala ya kutimiza wajibu na kufuata sheria zilizopo kwa wakati huu.
  Hizi organization za wanafunzi zina nafasi nzuri sana katika nchi yetu ya kuweza kubadilisha mambo mbalimbali yanayowahusu wanafunzi hata yale makubwa ambayo wengine wanafikiria hayawezekani. Ila tatizo ambalo wanashindwa kulielewa ni kuwa kuna mamlaka halali (hata kama ni mbaya) ambazo zinasimamia shughuli zao au za kijamii kwa mujibu wa sheria za nchi hii.
  Sasa basi, sisi ambao tuko nje na wigo wa uendeshaji wa asasi zao hao wanafunzi hatujui wanaongea nini kwenye vikao na wanapanga vipi mikakati ya kutekeleza majukumu yao. Lakini unaposoma matamko kama ambalo limewekwa hapa kwenye thread hii utaona kuwa hizo asasi za wanafunzi zinaongea kana kwamba zenyewe ndiyo zenye mamlaka ya juu zaidi ya uongozi wa Chuo na Wizara husika kwa maana ya serikali. Kwa hali hii ni vigumu kabisa kwa taasisi zilizopewa jukumu la kusimamia utawala na uendeshaji wa Chuo kukaa pamoja au kuafiki madai kama yalivyotolewa hapu juu. Ni wazi kabisa asasi za wanafunzi zimekosa mikakati yenye kuubana uongozi na serikali katika meza ya majadiliano. Ikumbukwe kuwa si kila dai la wanafunzi linaweza kutekelezwa na Chuo au Serikali ni vema basi wanafunzi wangekuwa na mikakati ya kuhakikisha kuwa walau sehemu ya madai yao yawe yanafikiwa kiwango fulani cha utekelezaji kila mwaka.
  Maneno makali yenye kiburi na dharau kwa wenye kwa uongozi halali wenye dhamana yanatoa fursa kwa uongozi huo kutatua tatizo la chuo kwa kuzingatia upande mmoja bila ya kuwashirikisha wanafunzi.
  Mimi ningeshauri hawa viongozi wa wanafunzi kwanza washirikiane na uongozi wa chuo ili wahakikishe kuwa wanafunzi wengi wanarudi chuoni kwa utaratibu ambao umewekwa na uongozi wa chuo sasa hivi. Hii njia ni muhimu kwani itasaidia kuleta kuaminiana baina ya pande hizo mbili.
  Pili, asasi hiyo ya wanafunzi ijaribu kutatua kikwazo kitakachojitokeza kwa wale wanafunzi ambao hawatakuwa wamefikia taratibu za udahili. kwa kufanya hivi ni rahisi kuushawishi uongozi kuwakubalia hao wanafunzi pending kukamilisha taratibu mpya.
  Tatu, wanafunzi waanzishe association mpya badala ya Daruso kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na uongozi wa Chuo. Ikumbukwe kuwa hapo Chuoni Uongozi ni mmoja tu at a time inabidi wanafunzi watoe ushirikiano na wala si vinginevyo.
  Ninajua binadamu wa kawaida ambaye hana mapungufu anakuwa jazba, busara, hekima na kadhalika lakini utatofautiana vipi na wengine basi itategemea ni jinsi gani utaweza kuvitawala vitu hivyo. kazi kubwa ya wanafunzi ni kusoma kwa hiyo wanapaswa kuhakikisha kuwa pamoja na matatizo mengine, kazi yao ya msingi haiathiriki kwa kiwango kikubwa.
  Mwisho, ningeshauri vyama vya wanafunzi katika vyuo vyetu vikuu vijijenge na kuendesha mambo yao kwa kuzingatia maslahi zaidi ya wanafunzi katika kutimiza ndoto zao, yaani kukamilisha masomo yao. Mifumo mingi ya endeshaji wa vyama vyetu vya wanafunzi unakuwa kama ule wa vyama vya siasa hatimaye baadhi ya viongozi kwenye asasi hizo hujiona kuwa ni kama wanasiasa na kuanza kufanya mambo kisiasa zaidi. Tunahitaji kubadilika.
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Jan 24, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,703
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  1. Hivi kwa nini mdhamini lazima awe mwajiriwa serikalini?

  2. Uhuru wa mwananchi kutofautiana au kutotofautiana na serikali yake au chombo kingine chochote hautakiwi kuwekewa mipaka. Uhuru huu unahusu hata kuonyesha hisia zao kwa namna yeyote. Wajibu wa serikali ni kuhakikisha kuwa kwa kufanya hivyo hakuathiri wananchi wengine. Katika mfumo huu wa kuonyesha hisia kwa njia ya maandamano, wajibu wa serikali ni kuweka ulinzi kuhakikisha waandamanaji hawadhuru mtu na wenyewe hawadhuriwi na wanaotofautiana nao. Ukiangalia kwa wenzetu wakati wa mikutano ya WTO, pamoja na kujua kuna anarchists ambao wao starehe yao kubwa ni kupambana na polisi, hawazuii maandamano dhidi ya Globalization. Wanachofanya ni kuyapatia nafasi na kuweka ulinzi wa kuhakikisha hakuna atakayeumia au kuharibu mali za wenzao. Kwa wenzetu hata Neo Nazis wanapewa nafasi ya kuandamana ingawa hakuna serikali iliyo makini inayokubaliana na sera zao! Hii ni pamoja na kujua kuwa kuna watu wa mlengo wa kushoto ambao nao wako tayari kupambana na hao Neo Nazis. Ulinzi unatolewa kuhakikisha usalama wa hao Neo Nazis na vile vile kuwazuia wasifanye fujo.

  Kama kweli tunataka demokrasia ya dhati ni lazima tukubali kukosolewa, kutofautiana na zaidi ya yote kulinda kwa nguvu zote haki za wale wanaotofautiana nasi. Haya ya kunyima vibali kwa flimsy excuses hayana nafasi katika demokrasia. Kama mwana wa Afrika Obama alivyowaambia watendaji wake wakuu, " tusisahau hata siku moja kuwa sisi ni watumishi wa wananchi na si vinginevyo", au maneno kama haya. Itakuwa vyema kama na sisi tukimsikiliza. Mara nyingi tunatumia taratibu kuwanyima haki wananchi. Hii si haki maana mara nyingi wafuatao hizo taratibu hatuwasikilizi.

  Amandla......
   
 18. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Hata US huwezi andamana bila kibali cha polisi, Sharpton na wenzake walipotaka kuandamana kupinga hukumu ya polisi kwenye kifo cha Sean Bell polisi walikataa, na alipoandamana anyways akapigwa pingu na majuzi tu amelipa fine mahakamani for that, tunawaomba vijana wetu watimize masharti ya sheria ya uandamanaji kwanza kama sheria ina kasoro basi wabunge wetu wa CCM na upinzani waivalie njuga ibadilishwe.

  Sheria ni sheria, wa kulaumiwa sio mtekelezajiwa sheria ila mtungaji, hapa in this case polisi ni watekelezaji tu wa sheria.
   
 19. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #19
  Jan 24, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawa Wanafunzi hata wangeandamama still it wouldnt help.Kama waligoma wakarudishwa nyumbani na bado nothing has changed I suggest they use forms like sending petitions to the parliament to help through wiht htese and they settle for more diplomatic methods!
   
 20. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #20
  Jan 24, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  FMES,

  Endelea kutoa somo hadi lieleweke ...
   
Loading...