Mhadhiri UDOM akamatwa kisa Maandamano ya Sabasaba

lengi

Member
Joined
Nov 19, 2025
Posts
5
Reaction score
10
Chama cha Wafanyakazi wa Kitaaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) kimesema mmoja wa wanachama wake, mhadhiri Melkisedeki Kitunzi Kaijage, alikamatwa na kushikiliwa na Jeshi la Polisi kufuatia tuhuma zinazohusishwa na maandamano ya Julai 7, maarufu kama Sabasaba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na UDOMASA yenye tarehe 18 Julai 2026, Kaijage aliitwa katika Kituo cha Polisi UDOM tarehe 3 Julai 2026 kupitia mkuu wake wa idara. Baadaye, tarehe 8 Julai, alifika kituoni akiwa ameambatana na viongozi wa UDOMASA na mwanasheria wake, ambapo alielezwa kuwa anahitajika kwa mahojiano yanayohusiana na tuhuma za kuhamasisha maandamano ya Julai 7 kwa njia ya mitandao ya kijamii.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa baada ya kuhojiwa, Kaijage aliomba apewe dhamana, lakini ombi hilo lilikataliwa wakati tuhuma hizo zinadhaminika,na baadaye alihamishiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na kuwekwa mahabusu. Siku iliyofuata alipelekwa Kituo Kidogo cha Polisi Chang'ombe huku uongozi wa UDOMASA ukiendelea kufuatilia shauri hilo na kushirikiana na mwanasheria wake katika juhudi za kumuwezesha kupata dhamana.

UDOMASA imesema kuwa baada ya ombi la dhamana kukataliwa, iliamua kutuma nia ya kwenda mahakamani ili kutafuta haki ya mwanachama huyo. Kesi ilitajwa kwa mara ya kwanza Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Julai 17, 2026, lakini ikaahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena Julai 21, 2026.

Katika taarifa yake, UDOMASA ilisisitiza kuwa inasimamia haki za wafanyakazi na inapinga ukiukwaji wa taratibu za kisheria dhidi ya wafanyakazi wake. Chama hicho kimewahimiza wanataaluma kuwa watulivu huku kikiahidi kuendelea kutoa taarifa kuhusu mwenendo wa shauri hilo, ikiwemo hatua za dhamana na mwenendo wa kesi mahakamani.

Tukumbuke mtuhumiwa huyohuyo ndio alikamatwa mwaka jana mwezi disemba kuhusu maandamano yaliyokuwa yamepangwa, unaweza kuisoma habari hii kwa kubonyeza kiambatanisho kifuatacho: SOMA HAPA
​
1784486360259.png

1784486376809.png

-----------
Pia ieleweke kuwa Kaijage anafundisha masomo ya siasa, na moja ya somo analofundisha ni PO 123 (Government and Politics in Tanzania) inayoongelea serikali na siasa za Tanzania baada ya uhuru hadi sasa. katika somo hili hana uwezo wa kukwepa kuongelea siasa za tanzania baada ya uhuru hadi sasa. kumuingilia katika ufundishaji wake kunaweza kuathiri elimu anayoitoa au akubali kuingia katika tuhuma hizo mara kwa mara.

MY TAKE:Huyu Muadhiri anafundisha siasa,miongoni mwa module alizonazo ni Government and Politics in Tanzania,hivi atawezaje kuacha kuongelea siasa katika mfumo wa 3D kwa mifano hai?,msagaji kaamua kulisaga na taifa.

kukamatwa.jpg
 
View attachment 3632427
Kama hawataki Hilo somo SI walifute, kuliko hii kamata kamata,wanadhalilisha Taaluma!
 
Tukumbuke mtuhumiwa huyohuyo ndio alikamatwa mwaka jana mwezi disemba kuhusu maandamano yaliyokuwa yamepangwa,
Duh,
Kwa hiyo vyuoni hakuna tena uhuru wa kitaaluma, uhuru wa kuwa na mawazo/maoni ya kitaaluma?

Wanataka wahadhiri wawe machawa wa ccm?
 
Back
Top Bottom