Polisi wapiga mabomu ya machozi kabla ya mkutano wa Chadema kufanyika

Status
Not open for further replies.

cjilo

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
884
444
taharuki ni kubwa, ntawajuza, ni bomu la machozi ni mbunge alienda kuwasalimia polisi kwenye gari lao, mara tukasikia kishindo cha bomu mtu mmoja amejuruhiwa
updates;
bomu la machozi limejeruhi mtu mmoja na amekimbizwa hospital
updates, mkutano huu wapigwa marufuku na polisi leo mchana kwa sababu kuna ugeni wa makamu wa rais, ila iliruhusu mkutano wa diwani wa chadema ubungo mataa, mnyika aamua twende ubungo kwenye mkutano ulioruhusiwa na polisi, sasa ndo tunatoka mabibo tunaenda ubungo
updates to come...
Nakutana na makundi mbali mbali wengine wakiwa ndo wanakuja uwanjani tukiwapa habari hizi wanalaani na tunageuza nao, pploce nao wameongeza magari yao, cna uha uhakika wa hali ya huko ubungo, watu wanajazba wanasema wakituzuia na ubungo kitawaka tu, hakuna kugeuza shavu la kushoto
updates;
tumefika ubungo na mbunge amepanda jukwaani ntawajuza
updates;
mtanisamehe kuhusu picha maana natumia kamchina ntakachoaanza kukalipia kila mwezi, shangwe zinaendelea hapa ubungo watu shazi kama kawaida, mnyika na madiwani wa chadema ubungo wapo jukwaani sasa, msanii maarufu wa cdm ameanza kutoa burudani
updates;
diwani ubungo anafungua mkutano, anasema mkutano huu ulibidi uwe mabibo ila tumewazidi polisi tulichukua vibali viwili vya mkutano kwa ajili ya tahadhari, anasema ahadi zake ameanza kutimiza kama za kujenga madaraja ya kuunganisha mitaa, asema polisi mwisho wao ubungo, mtetezi mkubwa wa machinga wenyewe wanamuita raisi wa machinga, anasema ubungo itakuwa wa mwisho kuondolewa kwa wamachinga,
diwani sinza; polisi walizamiria kumuua mnyika pale mabibo, asema tujifunze kufa tusiendelee kuuawacha upuuzi wa ccm
diwani kimara; mkuu wa wilaya amezuia mkutano wetu wa mabibo, anakataa kupokea cm za madiwani wa chadema muda huu

mnyika amesimama; anaanza kutambulisha viongozi wa chama na wale wanaojivua gamba leo, amesema kulikuwa na mlipuko mkubwa kwenye gari la polisi baada ya mlipuko polisi walimkimbilia majeruhi ili wamchukue, jitahada za mnyika zilifanikiwa kumuokoa na kumkimbiza hospitali, majeruhi mwenyewe ameongea huku akishikiliwa na watuhapa baada ya kutoka hospital, amejuruhiwa kati kati ya mapaja karibu na sehemu za siri,
anaanza kutoa mrejesho wa bungeni.....
Anasema kipengele cha kodi ya line kilirukwa wakati bajeti inasomwa walipohoji na kupiga kelele spika alise,a kinachoingia kwenye hansard ni kilichoongelewa c kilichoandikwa, anasema walienda kwenye mazishi ya mabomu arusha waliporudi walikuta bajeti inaendelea wakakata shauri wasiingie bungeni na kuikubali hiyo bajeti, ccm wanaogopa kuikataa bajeti kwa sababu wanaogopa uchaguzi

mnyika ameeleza historia ndefu sana kuhusu kodi ya cm ilivyokuwa

kamati ya chenge ilipendekeza kuanzishwa kodi mbali mbali ikiwemo za cm, lakini mpaka sasa wamekamilisha kodi moja na kodi zingine wameziacha kwa hiyo hayo cyo mawazo ya bunge wote

spika aliamua alivunja kanuni aliamua wote wenye marekebisho ya mswada wapeleke kwenye kamati na sio kurekebisha bungeni lengo kuzuia mswada huo usipingwe,

serikali imegundua kosa lake asema serikali itafuta tu hii kodi, asema yeye anataka gharama za maisha pia zipungue, ndo maana anaendelea kuchukua sign za watu apaeleke hoja binafsi

asema chenge alimwambia yeye anampotezea muda sasa tumuulize wenyewe kupitia 0754782577; bila kutukana matusi

viongozi wa chadema waalikwa majirani wa jimbo la ubungo ni wakati wao wanatambulishwaa

aliyekuwa wakili wa mnyika kwenye kesi ya ubunge ( edson mbogolo) anatambulishwa sasa
na anaanza kuiongelea katiba mpya, anasema yeye ni mjumbe wa kamati kuu cdm na wakili wa kujitegemea na pia ni mwanafunzi wa shahada ya falsafa ya udaktari hapo udsm

anasema ni majanga kwa ccm kujipinga yenyewe, vitu ipange yenyewe na ijipinge yenyewe, ajenda ya katiba ni ajenda ya chadema ccm walilzimishwa na wananchi na sas inafanya jitihada kuipinga, cdm kuzunguka mtaa kwa mtaa kuongoza mabaraza ya katiba
chadema inatiutiana kwenye mambo manne tu ni haya

(1) tunu ya taifa,
uwajibikaji uwazi,rushwa na kupinga ufisadi, ccm haiitaki hii kabisa, wanataka zitungiwe tu sheria zake na c kwenye katiba chadema inasema haiwezekani kwani katiba ni sheria mama

(2) haki za binadamu, ccm wanaponga pia wanataka zicwepo kwenye katiba

(3) Muungano, ccm haitaki serikali tatu, wanajua cuf wakichaguliwa zanz cdm tanganyika wao watakuwa wanalandalanda tu wasijue pakushika
amemaliza kwa kusema ccm na watu kuitikia majangaaaaa.....



Mnyika anaongea tena anasema kuwa mabaraza ya katiba yanaanza mwanzo wa mwezi wa nane, kwa ccm ilishachakachua mabaraza ya katiba sasa wananchi waunde mabaraza yao, mbowe alishasema wabunge waongeze wananchi na sasa kazi inayofanya chadema wabunge kuizunguka tz nzima, amepewa nakala 50 na serikali kwa ajili ya jimbo lake, kuwagawia wannchi baada ya mkutano, watu wakaijadili kwenye vijiwe,
chadema inapinga bunge la katiba kuwa lile lile la maccm na wake zao wa cuf na raisi atateua wajumbe wengine zaidi ya 176 kuwakilisha makundi maalumu hii nn

-------------------------------

[h=2]VIDEO: Aliyepigwa bomu na polisi Mabibo Dsm anena ya moyoni leo[/h]
[video=youtube_share;SBu5P8cG1gE]http://youtu.be/SBu5P8cG1gE[/video]
 
Dah aisee ngja basi tufanye nchi yote iwe na maandamano kama amani kwa njia za amani inashindikana

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Policcm wameamua kuwatisha akina sisi kuhudhuria mikutano ya CDM. Ridhiki yangu yategemea uzima wangu, kwa hili la mikutano CCM wameshinda, lakini hasira zangu ni 2015 katika BOX
 
mtu mmoja amekimbizwa hospitali, amejurehiwa vibaya na bomu
 
Hawa watu hawajakiona hiki kitabu
sisi tulioko nje tumeshakipata
inabidi kisambazwe nchi nzima kuonyesha polccm wanavyoua raia wasiokuwa na hatia

attachment.php
 
taharuki ni kubwa, ntawajuza,
ni bomu la machozi ni mbunge alienda kuwasalimia polisi kwenye gari
lao, mara tukasikia kishindo cha bomu mtu mmoja amejuruhiwa

mkuu, mbona haieleweki? heading na maelezo ya ndani mbona haviendani? huyo mbunge wa chadema aliyeenda kusalimia polisi ni nani? isije ikawa ndo wale red bridgade wamefanya vitu vyao
 
Na leo Jpili huendi kanisani?
au kusambaza magazeti na usafi hadi jpili?
Ninawaonea huruma maana watu kama nyie ndo mngetetea maliasili ya nchi
ili mrudi nyumbani ila nyie ndo mnashangilia wakati wakuu wenu wakikomba kila kitu




Tulijua kuwa mnatengeneza m,atukio ili mpate kitabu kama hiki
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom