Polisi wamjibu ovyo Kardinali Pengo juu ya mauwaji ya Mapadri

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
  • Wadai wahalifu siyo kondoo wakamatike kirahisi
  • Wamtaka Pengo awaeleze aliko muuaji wa Padri

Jeshi la Polisi limemjibu kwa kejeli Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, kuhusu suala la kukamatwa kwa watu waliomuua Padri wa Kanisa Katoliki, Evaristus Mushi wa Parokia ya Minara Miwili kisiwani Zanzibar, likidai wahalifu siyo kondoo waliofungiwa kwenye mti.

Kutokana na hali hiyo, limemtaka Kardinali Pengo alielekeze jeshi hilo anakojua aliko mhusika wa mauaji hayo ili wakamkamate.

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Issaya Mngulu, alipozungumza na NIPASHE jana.

Padri Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi asubuhi ya Februari 18, mwaka huu akielekea kanisani kuendesha misa. Tukio lilitanguliwa na jingine la kujeruhiwa kwa risasi Padri Ambrose Mkenda wa parokia ya Mpendae, Zanzibar alipokuwa akiingia nyumbani kwake.

Katika matukio yote hakuna aliyekamatwa na kufikishwa mahakamani hadi sasa.

Aidha, wakati Mngulu akitoa kauli hiyo, Kamishna wa Jeshi hilo Zanzibar, Musa Ali Musa, alisema jana kuwa suala la mauaji ya Padri Mushi, liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Mngulu alisema aliyefanya mauaji hayo siyo mnyama ambaye ni rahisi kumkamata, bali ni binadamu anayetumia mbinu mbalimbali kujinusuru asikamatwe.

Alisema hayo kujibu shutuma zilizotolewa na Kardinali Pengo dhidi ya jeshi hilo kwamba, kinachoendelea tangu Padri Mushi auawe kikatili ni kama mbinu za kutaka suala hilo lisahaulike au liishe hivi hivi tu bila wahusika kukamatwa.

"Pengo aelewe kwamba, mtenda kosa, ambaye ni binadamu si sawa na kondoo aliyefungwa kwenye mti, unakwenda kumchukua kirahisi," alisema Mngulu.

Hata hivyo, alisema wanaendelea na upelelezi wa mauaji hayo na kwamba, timu maalum ya maofisa wapelelezi wa jeshi hilo wako visiwani Zanzibar kwa kazi hiyo kwa kushirikiana na askari wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI).

"Kama Kardinali Pengo anajua lolote, basi atuelekeze twende tukamkamate huyo kondoo aliyefungwa kwenye mti," alisema Mngulu.

Alipotakiwa kueleza hadi sasa ni watu wangapi waliokwisha kukamatwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo, Mngulu alisema hayuko katika nafasi nzuri ya kuelezea jambo hilo na kwamba, iwapo atawataja watuhumiwa hao anaweza kuharibu upelelezi.

Naye Kamishna Musa alipoulizwa na NIPASHE jana alisema mauaji ya Padri Mushi yalifanywa na mtu mmoja na kwamba, upelelezi wa shauri hilo unaendelea.

"Tunaendelea kuhangaika, kumtafuta, tukifanikiwa tutamfikisha mahakamani," alisema.

Hata hivyo, alisema katika upelelezi uliokwisha kufanyika, kuna watu kadhaa waliokamatwa, ambao alisema kutokana na mazingira aliyokuwapo jana hajui idadi yao.

"Mimi hata ukiniuliza wangapi nimekamata idadi yao hata siijui, kwa sababu ni kukamata, kuhoji, kukamata, kuhoji mpaka tufike pale tunapopataka," alisema Kamishna Musa na kuongeza:

"Mimi ukiniuliza wangapi nimewakamata ndiyo nitashindwa kujua. Kwa sababu kumbuka toka tarehe ile mpaka leo kuna watu chungu nzima tumewakamata na kuwahoji na kuwaachia.

"Wengine wamekamatwa, lakini wamepelekwa mahakamani kwa makosa mengine. Wale wengine katika kupeleleza tuliwakuta na risasi, noti bandia."

Hata hivyo, kuhusu wauaji, Kamishna Musa alisema bado hawajafikia hatua ya kuwapeleka mahakamani na kwamba, jalada la shauri lao limepelekwa kwa DPP.

"Ngoja nikuambie kitu. Faili (jalada) hilo la mauaji liko kwa DPP. Linasubiri maelekezo ya DPP. Wala hatunalo sasa hivi polisi. Polisi tumepeleleza, upelelezi tumeufikishia hapo. Lakini pahala pa kutaka kujua nini, tumempelekea DPP kupata maelekezo yake," alisema Kamishna Musa.

Hata hivyo, alipoulizwa kama wamekwisha kumkamata mtuhumiwa wa mauaji hayo, Kamishna Musa alisema: "mengine usiniulize, wewe jua kwamba, kuna faili liko kwa DPP."

Alipoulizwa kwanini mengine yasiulizwe, Kamishna Musa alisema: "Ala! Sasa wewe nitakwambia kila kitu? Kila kitu kina miiko yake. Hata wewe mambo mengine utaniambia? Hunambii ati. Kwa sababu yana miiko, yana muda. Ikishakuwa tayari nitakwambia."

Pia alipoulizwa kama idadi ya waliokamatwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo haijui, Kamishna Musa alisema: "Siwezi. Kwa mantiki ya kwamba, maana yake hili suala tunakamata na kuachia. Hao wengine tumewapeleka mahakamani baada ya kuona wana makosa mengine.

"Kwa hivyo, ukiniuliza toka siku ile nyie mmekamata wangapi, sasa hapa hivi nipo ndani ya gari nitashindwa kukwambia nilikamata watu ishirini, lakini kwa kukuhakikishia ni kwamba, kukamata, kupekua ndiyo kazi tuliyokuwa tunaifanya. Kwa hivyo, kuna watu wengi sisi tumewakamata na kuwapekua na kuwahoji."

Kamishna Musa aliongeza: "Mimi nafikiri tuachieni siku mbili tatu tutatoa taarifa tu. Hizo kelele za watu wanavyosema wewe achana nazo kwamba polisi hawafanyi kitu we achana nao. Kila mtu atasema atakavyo wakati hajui undani wa kitu."

Alisema kuna wahalifu walioua watu nchini Marekani wamekaa miaka 18 ndiyo wakakamatwa.

Tukio la kuuawa kwa Padri Mushi mbali na matukio hayo, pia kuna utata ndani ya jamii juu ya mashambulizi na mauaji ya viongozi wengine wa dini, akiwamo Mchungaji wa Kanisa la Pentecostal Assemblies of God, Mathayo Kachila mkoani Geita; Imamu wa Msikiti wa Mwakaje, Kitope Zanzibar, Sheikh Ali Khamis Ali, ambaye aliuawa kwa kuchomwa kisu shingoni shambani kwake.

Pia yuko Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fedhil Suleiman Soraga, ambaye alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.

Mwaka jana Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Stephen Ulimboka, alitekwa, akapigwa na kutupwa kwenye msitu wa Mabwepande akiwa haijambui.

Machi 5, mwaka huu, Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF) na Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006), Absalom Kibanda, alitekwa na kutendwa kama Ulimboka, watesi wake walimtoboa jicho, kuharibu meno yake ya mbele, kukata kidole na majeraha kadhaa kichwani.

Matukio haya yote yameacha jamii katika butwaa kubwa huku polisi wakivuta miguu bila kuwatia mbaroni wahusika wa unyama huo.
 
Inamaana hawajui ilunga yupo india? Watanzania ni mpaka mama zetu wapigwe risasi na watoto wetu ndo tutaamkani mpaka kiongozi mmoja akiuawa au watoto wao ndo wataamka... WALIO MUUA MTALII MBONA HAWAKUAMBIWA WALIPO..... KANISA MKILICHEZEA NIMESEMA LITATAFAKARI KUHUSU UHUSIANO NA SERIKALI..NDO HAPO MTAKAPO SHIKA ADABUMungu ibariki tanzania
 
Hii ishu police wanataka iishie hivihivi inaelekea wanajua undani wa mauaji ya Padri Mushi mbona kifo cha Rpc wa Mwanza Baro msako ulikuwa mkubwa mpaka wahalifu wakakamatwa hapa kunajambo kiburi hiki cha police wanakipata wapi,lile katuni lao walilo chora kudanganya toto niusanii mtupu.
 
Siku chache mara baada ya askofu mkuu wa Dar es salaam kulalamikia jeshi la polisi juu ya usiri wa watuhumiwa wa wauwaji wa viongozi wa kidini.Jana polisi wamemjibu kuwa watuhumiwa sio kama kondoo kuwa wanakamatwa tuu kama anawajua watuhumiwa waliko awambie polisi wakawakamate
Mbona wamemjibu vizuri tu tena kiungwana kama kiongozi wa dini wewe ulitaka wamjibu vipi.
 
Polisi wetu nathubutu kusema HAWANA AKILI NZURI...Hapa polisi mmoja auwawe watawapata wauaji hata saa mbili hazipiti...Magamba wawatume kufanya upumbavu hata sekunde haipiti wameshashika watu na maelezo ya kutosha...Mauaji ya padri kuna vipeperushi vimeonekana na kuna sheikh aliwatuma waumini wao wakiua watupe na vipeperushi; sasa hapo nini tatizo huyo sheikh yupo india na hospitali aliyepo inajulikana wanashindwaje kwenda kumchukua tena zaidi ya kondoo...Ubabaishaji sana wa jeshi letu, linafanya kazi kwa RAMLI na SIASA za magamba. Acha nchi ichukuliwe ndio watajuaa
 
Nchi hii imeingiliwa na sijui tutatokaje hapa....
Polisi wanacho kificha ni kwamba..mauaji ya mapadri yametokana na uchochezi wa kidini ulioanzishwa na serikali ya CCM huku Mwenyekiti wake akipigia mstari jambo hili!!

Kama mpaka sasa polisi wameshindwa kutoa taarifa ya maana juu mauaji ya mapadri maana yake ni kwamba hata fununu hawana...!!

Hapa maana yake ni kwamba polisi imekuwa dhaifu...kama mkuu wa kaya!!
 
intelejensia ya ingeweza kuzuia kifo cha padri Mushi, ingetumika kumzuia cku ya tukio acende kuongoza misa au ingempa polic wa kumlinda au polisi wakikuwa hawatoshi?
 
Mbona wamemjibu vizuri tu tena kiungwana kama kiongozi wa dini wewe ulitaka wamjibu vipi.
WAHALIFU SIO KONDOO,hehehehe,sasa hilo jibu lina ubaya gani waungwana Ritz watu wanalaum kwakua amejibiwa KAMANDA WAO WA KIDINI,MBONA YEYE ALISEMA SERIKALI NI KAMA HAIPO,KWANI HIYO KAULI NI NJEMA,,,PENGO AMEKUA MWANASIASA WA MADHABAHUNI KUPITIA MEDIA,,,,NA NDO MAANA WAMEMJIBU KISIASA,MAANA AMEBWABWAJA TU,KWAKUA NI YUPO DAR AGOMBEE JIMBO KUU DAR ES SALAAM
 
Last edited by a moderator:
Kwa kifupi ni kwamba serikali ya huyu ------ ilishafail kuanzia alipoingia madaraka 2015. Yaani kila kitu ni Hopeless.
 
KWANZA SALAM

Nimeshangazwa sana na majibu ya polisi kuwa kama Pengo anajuwa waliko wauwaji wa padri mushi awaeleze wakawakamate. haya si majibu ya mtu mzima kumjibu kiongozi kama pengo na inaonyesha ni namna gani polisi wamesahau kuwa kazi wa kutafuta wahalifu ni kazi yao na sio ya pengo na endapo wanashindwa kumkamata mtuhumiwa wakulaumiwa ni wao na sio pengo maana waondio tunawalipa mishahara kwa kazi hiyo na wala pengo halipwi mshahara na serikali.

Polisi wamejisahau kuasi cha kusahau kuwa hata sisi watanzania tuna ufahamu wa kujua hapa kuna kinachofanyika au hakuna, kwamfano polisi wanaposema mhalifu sio kondoo akae mahali pamoja wanataka kutuambia wao hawajajifunza jinsi ya kumtafuta mhalifu na kama ndivyo watuambie wale waliomua kamanda Balo walikamatwaje?au yule dereva aliemgonga trafiki alipatikanaje au tuamina kuwa mhalifu akimuua askari anageuka kuwa kondoo ila akimuuwa kiongozi wa dini au akimteka mwana habari hapo anakuwa si kondoo.

Polisi wanaposema kama pengo anamjua mhalifu akawaambie yule aliemteka na kumtesa ulimboka na ulimboka akawaambia ni rama wa usalama wa taifa wamesha mkamata? polisi nawaomba fanyeni kazi acheni kujidhalilisha.
 
Back
Top Bottom