Polisi waminya kesi ya mwanafunzi aliyelawitiwa

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Polisi waminya kesi ya mwanafunzi aliyelawitiwa


Na Lilian Justice, Morogoro

MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Murad wilayani Mvomero mkoani Morogoro, amelawitiwa na kuibiwa sh 150,000 za ada na mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi wa Kituo cha Turiani na kuachiwa.Badala
yake mwanafunzi huyo anadai kugeuziwa kibao na kuwekwa rumande huku akitakiwa kupokea kati ya sh. 200,000 hadi 600,000 ili aachane na kesi hiyo.Mwanafunzi huyo wa kiume ambaye ni yatima, mwenye umri wa miaka 15, aliwaambia waandishi wa habari mjini Morogoro kuwa tukio hilo lilitokea Januari 5, mwaka huu.

Aliwalalamikia polisi wa Kituo cha Turiani, waliomkamata na kumuachia mtuhumiwa aliyemtaja kwa jina la utani la ‘Mpango mzima’ aliyemfanyia unyama huo usiku wa manane.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alimvizia baada ya kutoka kuoga na kuamua kujisomea kwenye kibaraza cha chumba anachoishi, wakati rafiki yake anayeishi naye katika chumba hicho jirani na shule, akiwa amesafiri.

Anasema alimshikia kisu na kumtishia ampatie fedha alizokuwa nazo ambazo zilitokana na biashara ya chipsi aliyokuwa akiifanya kwa nia ya kujikusanyia ada.

Mwanafunzi huyo kutokana na woga, alilazimika kumpatia sh. 150,000 ambazo hata hazikusaidia asifanyiwe unyama, ndipo mtuhumiwa huyo alimlawiti na kuondoka.

Baada ya kitendo hicho, mwanafunzi huyo alipiga kelele lakini hakuna watu waliojitokeza hadi alfajiri alipoamua kwenda Polisi Turiani kutoa taarifa.

Kijana huyo alisema pamoja na askari aliyepokea taarifa zake aliyemtaja kwa jina moja la Awadhi kwenda kumkamata mtuhumiwa na kumkuta na fedha hizo na pamoja na kisu kilichotumika, aliweka fedha hizo mfukoni mwake na kumuweka mtuhumiwa rumande.

Alimpa fomu ya kwenda kutibiwa na aliporudi alikuta mtuhumiwa ameachiwa huru na yule askari akamwambia achukue sh. laki mbili aachane na kesi hiyo, jambo alilikataa.

“Nilimuona Mkuu wa Kituo, akaniuliza tatizo langu, lakini Awadhi akawahi kumweleza, na mkuu yule akaniambia wanipe sh. laki mbili kesi iishe. nikakataa. Akasema wanipe laki sita nikakataa. Akaniuliza ninataka sh.ngapi ili niachane na ile kesi kwa vile ilikuwa ni kubwa, nikakataa, nikitaka twende mbele kwenye vyombo vya sheria.

Baada ya kukataa yule mkuu wa kituo alimwambia Awadhi aniweke ndani, akanipiga virungu na kuniweka ndani,� aliongeza kusema mtoto huyo.

Alisema baadaye rafiki zake na wananchi walioguswa na lile tukio walifika kituoni na kuhoji hali ile, hivyo polisi wakaamua kuandika maelezo na kumlazimisha asaini, lakini alikataa, kisha wakamuachia bila suala hilo kupelekwa mahakamani.

Dada wa mwanafunzi huyo, Bi. Zainab Athuman, mkazi wa Diongoya, Turiani alisema baada ya kupata taarifa za mdogo wake kufanyiwa unyama huo, alikwenda kituoni kuonana na mkuu wa kituo, lakini aliambiwa askari mwenye shauri hilo alikuwa mjini kwenye kikao na alipaswa kurudi saa 9 alasiri.

Baada ya kuona anazungushwa, wananchi walichanga sh. 30,000 zilizowafikisha kwenye vyombo vya habari na nia ikiwa ni kuonana na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Bi. Fatma Mwasa kumueleza hali hiyo.

“Tumeona tuliweke wazi kwa watu ili tujue namna tutakavyosaidiwa, kwani sisi ni yatima, na wote bado ni wadogo, hali yetu kiuchumi sio nzuri, huyu mdogo wangu bado anahitaji matibabu ya kina na pia aendelee na masomo,â€� alisema dada wa mwanafunzi huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Bi. Adolphina Chialo alisema ofisi yake haijapokea taarifa za tukio hilo, lakini akaahidi kulifanyia kazi ikiwemo kuhakikisha kijana aliyefanyiwa unyama huo anapatiwa huduma za matibabu na kama kuna askari waliokuwa na nia ya kuvuruga kesi hiyo wanachukuliwa hatua.




1 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Hao ndio polisi wa mheshimiwa Mwema.
Kashfa zote ni zao na hawatishiki! Hata wakiandikwa humu watadunda tu mtaani na kushirikiana na wahalifu.

Yooooooooooooooooooooooooooooooooooooooote yanasababishwa na viongozi mafisadi.

Kama mabosi wao wanaiba EPA kwa migongo ya makampuni hewa, wasio na uwezo wa kuifikia EPA watafanyaje! Watashirikiana na wahalifu wapate chochote.

Mtetezi wa yatima ni Mungu pekee!!! Wanaosimamia shiria wanasahau kuwa muda wote na mahali popote wanapomuonea mtu, Mungu huwa yupo akishuhudia. Sheria zetu zinapindishwa na wajanja. Usishangae ukiambiwa mtoto huyu ndiye mkosaji.
January 11, 2011 5:07 AM
 
Laana ya serikali ya kifisadi sasa imetapakaa nchi nzima.............................
 
Back
Top Bottom