Polisi wamiminia risasi daladala

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
58
POLISI kanda maalumu Tarime/Rorya wanachunguza tukio la askari wake wawili kulimiminia risasi basi la abiria lenye namba za usajili T 928 BWK likiwa limeegeshwa baada ya wao kulisimamisha.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Sebastian Zakaria wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyetaka kujua sababu za milipuko ya risasi katika mtaa wa Mawasiliano, Tarime mjini jana asubuhi.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kwamba basi hilo ambalo hufanya kazi ya daladala lilisimamishwa na askari polisi wawili waliokuwa wakitaka dereva alipeleke basi hilo kituo cha polisi kwa ukaguzi.

Imeelezwa kuwa dereva huyo anayetambuliwa kwa jina la Robert Merengo (31) alipouliza sababu ya kupeleka basi lake hilo dogo la abiria aina ya Toyota Double Coaster polisi, askari mwenye bunduki alifika na kumtoa katika kiti chake cha udereva huku akiwa amemshikia mtutu shingoni.

Akisimulia mkasa huo, Merengo alisema akiwa nje ya sehemu ya kuuzia mbao mjini hapa Mtaa wa Mawasiliano alikopita baada ya kushuka abiria stendi ya mabasi Walimfuata askari wawili pale alipoegesha, mmoja trafiki na mwingine wa kawaida akiwa na bunduki na kuamuru aligeuze gari na kulipeleka Kituo cha Polisi.

Alisema alipowauliza gari hilo lina kosa gani, askari aliyekuwa na bunduki akamwambia ashuke kutoka ndani ya gari huku akimuelekeza bunduki.

“Nilitii amri kwa kuteremka, huku nikiacha gari ikiunguruma. Nilipoteremka chini walitaka kunipiga ndipo mama mwenye duka alipoingilia kati na kuhoji kwanini wanipige badala ya kuchukua namba za gari na kumtafuta mmiliki wake.

“Kabla mama yule hajamaliza kuwaeleza walifyatua risasi saba kwenye mlango wa kushoto na kusababisha watu pale mtaani kukimbia ovyo.”

Naye mmiliki wa basi hilo, Mohere alipoulizwa kuhusiana na basi lake kuwa huenda halina nyaraka muhimu zinazoliruhusu kutembea barabarani, alisema lina vibali vyote. "Gari langu lina vibali vyote, nasikitika kwa askari huyu kuniharibia gari na kutaka kuua dereva,” alilalamika.

Pamoja na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Sebastian Zakaria kusema kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa na kwamba uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea, ikiwa ni pamoja na kuwahoji askari waliohusika na tukio hilo, wananchi walisema kwamba lilileta kizaazaa kikubwa.

Mara baada ya tukio, mmiliki wake Boniface Mohere alifika eneo la tukio na kuamuru lipelekwe makao makuu ya polisi wilayani hapa akitaka aelezwe sababu za kuharibiwa kwa gari lake.
 
POLISI kanda maalumu Tarime/Rorya wanachunguza tukio la askari wake wawili kulimiminia risasi basi la abiria lenye namba za usajili T 928 BWK likiwa limeegeshwa baada ya wao kulisimamisha. Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Sebastian Zakaria wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyetaka kujua sababu za milipuko ya risasi katika mtaa wa Mawasiliano, Tarime mjini jana asubuhi.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kwamba basi hilo ambalo hufanya kazi ya daladala lilisimamishwa na askari polisi wawili waliokuwa wakitaka dereva alipeleke basi hilo kituo cha polisi kwa ukaguzi. Imeelezwa kuwa dereva huyo anayetambuliwa kwa jina la Robert Merengo (31) alipouliza sababu ya kupeleka basi lake hilo dogo la abiria aina ya Toyota Double Coaster polisi, askari mwenye bunduki alifika na kumtoa katika kiti chake cha udereva huku akiwa amemshikia mtutu shingoni.

Akisimulia mkasa huo, Merengo alisema akiwa nje ya sehemu ya kuuzia mbao mjini hapa Mtaa wa Mawasiliano alikopita baada ya kushuka abiria stendi ya mabasi Walimfuata askari wawili pale alipoegesha, mmoja trafiki na mwingine wa kawaida akiwa na bunduki na kuamuru aligeuze gari na kulipeleka Kituo cha Polisi. Alisema alipowauliza gari hilo lina kosa gani, askari aliyekuwa na bunduki akamwambia ashuke kutoka ndani ya gari huku akimuelekeza bunduki.

“Nilitii amri kwa kuteremka, huku nikiacha gari ikiunguruma. Nilipoteremka chini walitaka kunipiga ndipo mama mwenye duka alipoingilia kati na kuhoji kwanini wanipige badala ya kuchukua namba za gari na kumtafuta mmiliki wake. “Kabla mama yule hajamaliza kuwaeleza walifyatua risasi saba kwenye mlango wa kushoto na kusababisha watu pale mtaani kukimbia ovyo.”

Naye mmiliki wa basi hilo, Mohere alipoulizwa kuhusiana na basi lake kuwa huenda halina nyaraka muhimu zinazoliruhusu kutembea barabarani, alisema lina vibali vyote. "Gari langu lina vibali vyote, nasikitika kwa askari huyu kuniharibia gari na kutaka kuua dereva,” alilalamika.

Pamoja na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Sebastian Zakaria kusema kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa na kwamba uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea, ikiwa ni pamoja na kuwahoji askari waliohusika na tukio hilo, wananchi walisema kwamba lilileta kizaazaa kikubwa.

Mara baada ya tukio, mmiliki wake Boniface Mohere alifika eneo la tukio na kuamuru lipelekwe makao makuu ya polisi wilayani hapa akitaka aelezwe sababu za kuharibiwa kwa gari lake.

Habari Leo
 
Taarifa za kiintelijensia labda walipewa! Afu maajabu ya Tz, utashangaa hawachukuliwi hatua, na wakichukuliwa hatua mwenye gari wala walioathirika kisaikolojia hawasaidiwi chochote!
Tz nakupenda kwa moyo wooooote!
 
nitashangaa sana kusikia huyo askari hajachukuliwa hatua yoyote.....
 
Kweli tanzania imeoza kabisaaaaa.siku zote polis wanaamini wapo juu ya sheria.Nadhani ugumu wa maisha unamfanya kila mtu kuwa KATILI.
 
hata mbuyu nao ulianza kama mchicha.

Hawa polis naona taratibu wanajiamulia maamuzi yao walianza taratibu na sasa wanatisha kwa bunduki kwenye maandamano wanadungua watu na risasi kama ndege.

Badae watakazoea katabia hako na kuanza kukamata watu kwa kuwapiga watu kwanza risasi ndipo wawakamate.

Inabid wakae wakijua tz ya leo siyo ya miaka 50 iliyopita watu now wanazijua haki zao.
 
Kuna haja ya watz kujua thamani ya Risasi zinazotumiwa ovyo na hao askali polisi: inaonekana siku hizi matumizi ya risasi imekuwa fasheni kana kwamba zinapatikana bure, hakuna aja ya kuzinunua kama zinatumika ndivyo sivyo.
 
Nashauri hao askari wakapimwe akili.

Kama wana hamu ya kufyatua risasi tuwapeleke nchi zenye vita wakasaidie.

Watu kama hawa ni wa kuwanyonga hadharani ili fundisho kwa wajinga wengine.
 
Ona sasa tukisema police ni mambumbu watakataa?hizo risasi alizoharibu hapo nani atazilipa?hizo ni kodi zetu amezichezea bila huruma,ni bora angejimiminia mwenyewe kuliko kuziharibu.
 
Undugu mwingi bila elimu umezidi. Japo waziri Vuai alisema anataka ripoti fupi ya kurasa. 2 hakuna polisi niliyesikia amechukuliwa hatua. Wale polisi wauaji wa kasulu wapo mtaani tu wanatamba. Japo walishuhudiwa wakiua hakuna lolote lililofanyika. Wengine wameua tena kasulu mwezi wa kumi na mbili kwa kung'oa nywele zake hadi amekufa rasta polisi hao wapo nje tu japo inasenekana wapo lock up lakini sio ukweli. Nawaona mtaani. Kwa kuwa hawachukuliwi hatua ni bora wananchi wakaanza kutumia nguvu ya umma kuwapiga hadi nao wafe.
 
POLISI kanda maalumu Tarime/Rorya wanachunguza tukio la askari wake wawili kulimiminia risasi basi la abiria lenye namba za usajili T 928 BWK likiwa limeegeshwa baada ya wao kulisimamisha.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Sebastian Zakaria wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyetaka kujua sababu za milipuko ya risasi katika mtaa wa Mawasiliano, Tarime mjini jana asubuhi.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kwamba basi hilo ambalo hufanya kazi ya daladala lilisimamishwa na askari polisi wawili waliokuwa wakitaka dereva alipeleke basi hilo kituo cha polisi kwa ukaguzi.

Imeelezwa kuwa dereva huyo anayetambuliwa kwa jina la Robert Merengo (31) alipouliza sababu ya kupeleka basi lake hilo dogo la abiria aina ya Toyota Double Coaster polisi, askari mwenye bunduki alifika na kumtoa katika kiti chake cha udereva huku akiwa amemshikia mtutu shingoni.

Akisimulia mkasa huo, Merengo alisema akiwa nje ya sehemu ya kuuzia mbao mjini hapa Mtaa wa Mawasiliano alikopita baada ya kushuka abiria stendi ya mabasi Walimfuata askari wawili pale alipoegesha, mmoja trafiki na mwingine wa kawaida akiwa na bunduki na kuamuru aligeuze gari na kulipeleka Kituo cha Polisi.

Alisema alipowauliza gari hilo lina kosa gani, askari aliyekuwa na bunduki akamwambia ashuke kutoka ndani ya gari huku akimuelekeza bunduki.

“Nilitii amri kwa kuteremka, huku nikiacha gari ikiunguruma. Nilipoteremka chini walitaka kunipiga ndipo mama mwenye duka alipoingilia kati na kuhoji kwanini wanipige badala ya kuchukua namba za gari na kumtafuta mmiliki wake.

“Kabla mama yule hajamaliza kuwaeleza walifyatua risasi saba kwenye mlango wa kushoto na kusababisha watu pale mtaani kukimbia ovyo.”

Naye mmiliki wa basi hilo, Mohere alipoulizwa kuhusiana na basi lake kuwa huenda halina nyaraka muhimu zinazoliruhusu kutembea barabarani, alisema lina vibali vyote. "Gari langu lina vibali vyote, nasikitika kwa askari huyu kuniharibia gari na kutaka kuua dereva,” alilalamika.

Pamoja na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Sebastian Zakaria kusema kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa na kwamba uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea, ikiwa ni pamoja na kuwahoji askari waliohusika na tukio hilo, wananchi walisema kwamba lilileta kizaazaa kikubwa.

Mara baada ya tukio, mmiliki wake Boniface Mohere alifika eneo la tukio na kuamuru lipelekwe makao makuu ya polisi wilayani hapa akitaka aelezwe sababu za kuharibiwa kwa gari lake.

Source: Habari leo
 
Back
Top Bottom