Asema POLISI wamekosa Hekima katika kusimamia mambo haya. CHADEMA wanamfahamu aliyerusha lile bomu ambalo limeleta maafa kwa watu wawili, Mh.TUNDU LISSU Mbunge wa Singida Mashariki na Mh. Akonai Mbunge wa Karatu wanashikiliwa kituo cha POLISI mpaka dakika hii. Na Mabomu bado yanapigwa mpaka sasa, Jambo lkujifunza POLISI wetu ni wachanga sana ktk kukabiliana na matukio kama haya, KWANZA wao ndio waliwaruhusu CHADEMA waondoe gari katikati ya uwanja wa Soweto,kuwasha Spika na kuhutubia WANANCHI,Kwanini POLISI tena waanzisha kulipua Mabomu?
Lingine ambalo nimeshuhudia kwa Macho na masikio yangu mwenyewe nikiwa stand ndogo ya daladala zinaenda USA, Ngaramtoni, Majengo na Njiro,POLISI waliingia mpaka ndani ya stand wakaanza kutembeza kisago kuna kijana mfanya biashara wamepigwa na POLISI mmoja huku anaambiwa kimbia (nilijiuliza akimbie aende wapi? Wamemkuta yuko kwenye biashara atamwachia NANI hizo bidhaa zake? Baada ya kumpiga akatugeukia sisi tulikuwa watatu akaagiza lete fimbo huko POLISI yeye mwenyewe akitetemeka chapa Hawa wazee LAKINI naona wenzake alipuuza amri yake hio.
Kisha sisi tulianza kuondoka mdogo mdogo bila kujali watatupiga ama waturushia mabomu ya machozi au risasi za moto. Askari wetu hawajatulia kisaikolojia.
Nilidhani baada ya kufanikiwa kuwasabaratisha watu kwenye uwanja wa Soweto, wangeanz kutumia gari lenye vipaza sauti kuwatangazia watu waliomitaa ya karibu na Soweto wasirudi tena uwanjani chakusikitisha wakaendeleza mabomu mpaka saa hizi wamesababisha na vijana nao wakaanza kuchoma matairi.
Mh. Lema amesema hawatautoa ushahidi kwa POLISI maaana wao ndio wahusika na watuhumiwa namba moja. .