Jeshi letu la polisi: Usalama wangu na Mali zangu

kiroka

JF-Expert Member
Feb 28, 2018
355
1,856
Kwa mujibu wa sheria kazi ya msingi ya jeshi la polisi ni kulinda raia na Mali zao, hii ni kazi inayohitaji wito Kama kua padri wa kirumi, inahitaji mtu muadilufu kama shehe wa kule makka, nikilala ndani kwangu najua polisi wapo kazi yao ni kunilinda Mimi raia wa nchi yao natakiwa nisiwe na hofu niwe na uhakika wa usalama wangu na Mali zangu kama mtoto mchanga alalavyo kwenye kifua cha baba yake.

LAKINI

Ninapowaza mambo kadhaa yaliyotendwa au yanayotendwa na watu waliomo kwenye hili jeshi nakosa amani

Nikiwaza kuhusu ile kesi ya kina Zombe kwamba askari wetu Hawa wenye dhamana ya kulinda raia na Mali zao waliwakamata raia wakiwa wazima wa afya wasiokua na hata chembe ya hatia wakawaua then wakaja kwenye kamera watuambia ni majambazi ilikua ni aibu ya karne. Hata kama haki imetendeka na watuhumiwa wamefungwa lakin bdo kuna mashaka makubwa kuhusu jeshi letu.

Kupigwa risasi kwa Lissu, mpaka Leo hakuna mtu hata mmoja aliekamatwa kuhusu kushambuliwa kwa lisu, tukio lililotokea makao makuu ya nchi yetu mchana wa jua Kali mchana kweupee, unawaza hivi kama mbunge ameshambuliwa saa nane mchana jua la utosi ndani ya majengo ya serikal katikati ya nchi yetu, Mimi ninae lala mbavu za mbwa huku mazinyungu kilosa morogoro itakuaje.

Wizi kwenye vituo vya polisi, kuna vitu ni aibu saana unapata ajali ya gari unavutwa kwenda police unaliacha gari police kesho unakuja baadhi ya spear hakuna zinaoteaje polisi sehemu salama jamn, au unakamatwa na ukiwa na boda boda ukiicha polisi asubuhi unakuta mafuta uliyaacha Jana hayapo, sehemu salama.
 
Back
Top Bottom