kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
ASKARI Polisi mjini hapa wameiomba Serikali kuangalia jinsi ya kuboresha nyumba wanazoishi walinzi hao wa Usalama wa raia kutokana na kile walichodai zimechakaa kupita kiasi na kwamba hali ya sasa haioneshi kuwa zinafaa kukaliwa na binadamu.
Askari hao wanaoishi kambini walieleza kwamba nyumba hizo kwa sasa zilizo nyingi katika makazi yao kuta zake zimepasuka, vyoo vyake vimebomoka na hivyo kutishia usalama wa afya zao.
Wakizungumza na gazeti hili mjini hapa, baadhi ya askari ambao hawakutaka kuandikwa majina yao walisema kwamba wameamua kuzungumzia hilo kutokana na hali halisi ya mazingira wanayoishi kambini humo, kitendo ambacho wamekielezea kuwa kinawakosesha raha.
Walieleza kuwa, kutokana na uchakavu wa nyumba hizo zilizojengwa karibu miaka 80 iliyopita, enzi za ukoloni, kuna kila sababu ya kuzifanyia ukarabati mkubwa, au kuzibomoa na kujenga nyingine.
Kama ulivyoshuhudia tu mwenyewe mwandishi wa habari, sisi ndo tunaishi katika mazingira haya, inasikitisha sana, alisema mmoja wa askari hao aliyeongeza kuwa, kutokana na hali hiyo, baadhi ya askari wanalazimika kupanga uraiani ili kuepukana na adha ya mazingira ya sasa na pia udogo wa nyumba hizo.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Barlow amekiri kuwepo kwa makazi duni kwa askari wake na kuielezea hali hiyo kuwa ni moja ya changamoto zinazolikabili Jeshi hilo muhimu kwa usalama wa raia na mali zao.