Polisi walalamikia uduni wa makazi yao

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
ASKARI Polisi mjini hapa wameiomba Serikali kuangalia jinsi ya kuboresha nyumba wanazoishi walinzi hao wa Usalama wa raia kutokana na kile walichodai zimechakaa kupita kiasi na kwamba hali ya sasa haioneshi kuwa zinafaa kukaliwa na binadamu.

Askari hao wanaoishi kambini walieleza kwamba nyumba hizo kwa sasa zilizo nyingi katika makazi yao kuta zake zimepasuka, vyoo vyake vimebomoka na hivyo kutishia usalama wa afya zao.

Wakizungumza na gazeti hili mjini hapa, baadhi ya askari ambao hawakutaka kuandikwa majina yao walisema kwamba wameamua kuzungumzia hilo kutokana na hali halisi ya mazingira wanayoishi kambini humo, kitendo ambacho wamekielezea kuwa kinawakosesha raha.

Walieleza kuwa, kutokana na uchakavu wa nyumba hizo zilizojengwa karibu miaka 80 iliyopita, enzi za ukoloni, kuna kila sababu ya kuzifanyia ukarabati mkubwa, au kuzibomoa na kujenga nyingine.

“Kama ulivyoshuhudia tu mwenyewe mwandishi wa habari, sisi ndo tunaishi katika mazingira haya, inasikitisha sana,” alisema mmoja wa askari hao aliyeongeza kuwa, kutokana na hali hiyo, baadhi ya askari wanalazimika kupanga uraiani ili kuepukana na adha ya mazingira ya sasa na pia udogo wa nyumba hizo.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Barlow amekiri kuwepo kwa makazi duni kwa askari wake na kuielezea hali hiyo kuwa ni moja ya changamoto zinazolikabili Jeshi hilo muhimu kwa usalama wa raia na mali zao.
 
wanavyoua raia wanafikiri ndio maisha yao yataboreshwa na serikali au
 
Wanawanyanyasa wananchi alafu hata hao mafisadi wanawafanyia kazi hawawajali!Na bado hali itaendelea kua mbaya mpaka hiyo mifisadi itakapoanguka!!
 
kwa nini wasilale kwenye magari ya kumwaga upupu wakiwa wamevaa nguo maalum za kutuliza ghasia wakiwa na ngao zao na virungu. Kiukweli Hela zilizowekezwa kwenye vitu hivyo vingetosha kabisa kuwapa makazi bora.

Wamekalia kukenua meno tu bila kujua kuwa wanaowatetea wala hawawajali, wanajali maslahi yao tu. Wanaowaua na kuwapiga virungu ndio wanaojali maslahi yao na wanaweza kuwa watetezi wao wazuri sana katika hili.
 
Sisi raia na polisi ndio hivo undugu umekwisha tangu January 05, 2011 na kinachobaki sasa hivi ni mazoea tu.

Waende wakawambie Baba zao mafisadi akina Rostam Aziz, Edward Lowasa na Jakaya Kikwete wanaowatumikia kutuua kinyama.
 
ASKARI Polisi mjini hapa wameiomba Serikali kuangalia jinsi ya kuboresha nyumba wanazoishi walinzi hao wa Usalama wa raia kutokana na kile walichodai zimechakaa kupita kiasi na kwamba hali ya sasa haioneshi kuwa zinafaa kukaliwa na binadamu.

Askari hao wanaoishi kambini walieleza kwamba nyumba hizo kwa sasa zilizo nyingi katika makazi yao kuta zake zimepasuka, vyoo vyake vimebomoka na hivyo kutishia usalama wa afya zao.

Wakizungumza na gazeti hili mjini hapa, baadhi ya askari ambao hawakutaka kuandikwa majina yao walisema kwamba wameamua kuzungumzia hilo kutokana na hali halisi ya mazingira wanayoishi kambini humo, kitendo ambacho wamekielezea kuwa kinawakosesha raha.

Walieleza kuwa, kutokana na uchakavu wa nyumba hizo zilizojengwa karibu miaka 80 iliyopita, enzi za ukoloni, kuna kila sababu ya kuzifanyia ukarabati mkubwa, au kuzibomoa na kujenga nyingine.

"Kama ulivyoshuhudia tu mwenyewe mwandishi wa habari, sisi ndo tunaishi katika mazingira haya, inasikitisha sana," alisema mmoja wa askari hao aliyeongeza kuwa, kutokana na hali hiyo, baadhi ya askari wanalazimika kupanga uraiani ili kuepukana na adha ya mazingira ya sasa na pia udogo wa nyumba hizo.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Barlow amekiri kuwepo kwa makazi duni kwa askari wake na kuielezea hali hiyo kuwa ni moja ya changamoto zinazolikabili Jeshi hilo muhimu kwa usalama wa raia na mali zao.

hawana sera hawa wanajua wazi wana maslahi duni lakini wanatesa wananchi mshahara wao kiduchu lakin bado hawataki mabadiliko. wakihamishwa hawalipwi stahili zao miaka na miaka bado tu wanatumikia mtwana,wacha wapate cha moto nlishatembelea makazi yao hapo dar nlishangaa kuona wanasumbuliwa na kunguni.viongozi wao wanakula kuku kwa mrija nk wao wanalia njaa.hawaoni wenzio wanajeshi wanatesa? mwosha huoshwa.

Hivi bado upolisi ni kwa watu waliokosa mueleko wa maisha au vigezo vinazingatiwa?? nina wasi wasi na polisi wa nchi hii coz wengi wao ni mapolisi baada ya channel zote kukataa na sio kwa ajili ya kutumikia raia na mali zao. Kuhusu makazi duni ni moja ya changamoto za maisha kama watanzania wengne tu vijijini kwenye nyumba za tembe.
 
Polisi wanachohitaji ni silaha zaidi ili kuendelea kuua Watanzania. Ninawasikitikia sana.
 
Polisi walalamikie uongozi wao au wajilaumu wenyewe. Wanaandaa bajeti yao kila mwaka na vipaumbele vyao ni magari ya maji ya kuwasha, virungu na risasi. Wangeweka makazi kama kipaumbele basi wasingekuwa na matatizo hayo!!

Malalamiko yao wameyapeleka kwa serikali lakini naona wazi wangeyapeleka kwa Said Mwema na kubainisha wazi kuwa kipaumbele chao ni hicho.:loco:
 
Waishi hata kwenye mapango na mende..who cares wauaji vibaraka wa ccm?
 
Walale hata nje hakuna atakayewajali kama kodi zetu ambazo ndo zingewaboreshea maisha yao wanazikingia kifua ziibiwe sa si tuwasaidiaje?kufeni kama mnavyowauwa raia wasio na hatia.mabosi wenu wala hata hawana time na nyie vibaraka msioelewa mbele wala nyuma ni wapi.
 
nadhani umefika wakati wa kuwa na jeshi la polisi lenye tija kwa taifa na sio kwa wanasiasa. how?(katiba mpya)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom