Polisi waisoma namba; TANESCO wakata umeme kwenye maghorofa ya Polisi Kurasini

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,778
239,455
Yale maagizo ya Mh Rais wa Tanzania , Dr Magufuli , ya kuhakikisha TANESCO inawakatia umeme wadaiwa sugu yametua kwenye maghorofa ya polisi Kurasini ( maarufu kama Maghorofa ya Relwe ).

Ni siku ya tatu sasa giza totoro linawakabili wana usalama wetu

Haijafahamika kiasi cha fedha ambacho jeshi hilo linadaiwa , na pia haijajulikana sababu za viongozi wa polisi kushindwa kuomba muda kidogo wa kulipa deni hilo kama walivyofanya JWTZ , ili kunusuru askari wetu

Source ni mimi mwenyewe niliyemtembelea Inspector mmoja ambaye ni ndugu yangu .
 
Ukiona JESHI ''limepiga goti'' na kulipa kidogo huku lilisisitiza na wengine wote walipe, then ujue ''things are no longer at ease''. Jana ofisi nyingi za Serikali nao wamesomeshwa namba za kirumi kwa kukatiwa umeme, NIMR wakiwemo.
 
Yale maagizo ya Mh Rais wa Tanzania , Dr Magufuli , ya kuhakikisha TANESCO inawakatia umeme wadaiwa sugu imetua kwenye maghorofa ya polisi Kurasini ( maarufu kama Maghorofa ya Relwe ).

Ni siku ya tatu sasa giza totoro linawakabili wana usalama wetu

Haijafahamika kiasi cha fedha ambacho jeshi hilo linadaiwa , na pia haijajulikana sababu za viongozi wa polisi kushindwa kuomba muda kidogo wa kulipa deni hilo kama walivyofanya JWTZ , ili kunusuru askari wetu

Source ni mimi mwenyewe niliyemtembelea Inspector mmoja ambaye ni ndugu yangu .
Mtawalaumu tu pesa wizara ilizoomba haizipati zote unategemea nini hapo?! Mkulu ni kutaka kujikosha tu ili watu waonekane hawafai!! Hadibleo wizara umeipa 16%ya pesa iliyoomba unategemea nini??
 
Ni sawa kabisa kabisa, maana hiyo ndiyo faida ya kura uliyopiga 2015 mkuu
 
Hivi zile fine zinazokusanywa barabarani na kutangazwa kwa mbwembwe huwa zinatumika kufanyia nini!! Walipe deni au wafungiwe machine za LUKU ili watumie kwa adabu.
 
Yale maagizo ya Mh Rais wa Tanzania , Dr Magufuli , ya kuhakikisha TANESCO inawakatia umeme wadaiwa sugu yametua kwenye maghorofa ya polisi Kurasini ( maarufu kama Maghorofa ya Relwe ).

Ni siku ya tatu sasa giza totoro linawakabili wana usalama wetu

Haijafahamika kiasi cha fedha ambacho jeshi hilo linadaiwa , na pia haijajulikana sababu za viongozi wa polisi kushindwa kuomba muda kidogo wa kulipa deni hilo kama walivyofanya JWTZ , ili kunusuru askari wetu

Source ni mimi mwenyewe niliyemtembelea Inspector mmoja ambaye ni ndugu yangu .
Wakatiwe kila kitu na hata pumzi wapewe ya mgawo, siyapendi mimi kazi uonevu tu. Kwanza sio lazima wawe na mwanga hawa wakati akili na roho zao nyeusi tii.
 
Jamani hebu wahurumieni askari wetu , wanafanya kazi kubwa sana , makosa yao madogomadogo ya kibinadamu yasitufanye tusahau wema wao .
 
Back
Top Bottom