Polisi wafanya mazoezi ya kwata mitaani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wafanya mazoezi ya kwata mitaani

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by johnmashilatu, Oct 27, 2010.

 1. j

  johnmashilatu JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Wakati tukiambiwa kuwa Vyombo vya ulinzi na usalama vitatumika kusimami zoezi la kupiga kura, Vitisho vimeanza kuonekana waziwazi wilayani Kibondo, mkoani kigoma.

  Juzi, 26.10.2010, askari Polisi wa wilaya hiyo iliyoko mpakani na Burundi na ambayo inasifika kwa vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha, walikuwa wakifanya mazoezi katika mitaa ya mji huo

  Mkuu wao, OCD, Innocent Rweramila ameelezea hali hiyo kuwa ni jambo la kawaida kwa walinda usalama hao kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu!

  wananchi wa Kawaida wanajiuliza, kwanini mazoezi haya yafanyike hivi sasa na si kabla na mbaya zaidi ni kufanyika mitaani

  wengi wanaeleza kwamba kw auelewa wao hawajawahi kuwaona askari hao wakifanya mazoezi mitaaani
  wanataka kuwatisha wananchi?

  kumbuka katika wilaya hiyo Mgombea wa CCM (muhambwe) ambaye anakabiliwa na tuhuma kadhaa, anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wagombea wa NCCR mageuzi na CHADEMA, ambapo jitihada za Makamba na mama salma kufika wilayani humo zimeshindwa kuzima kiu ya mabadiliko ya wananchi
   
 2. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Msiogope Mkwala huo,kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji!!hakuna kulala mwaka huu mbaka kieleweke!!!
   
 3. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Wasihi wananchi watulie kimyakimya jumapili kwenye sanduku la kura wakaonyeshe "umwamba" wao..
  Zingatia mabadiliko ni muhimu...tukianza na Rais makini wabunge na madiwani...
   
 4. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata polisi nao wanajua, hakuna bomu linaloua kama kura, tukutane Oct 31
   
 5. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni yupi, yule mwuji wa albino? Angalizo langu ni yupi anakubalika zaidi, NCCR or Chadema? wasije wakagawana kura za upinzani ccm akapeta!!!!
   
 6. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  msiogope hao polisi wote ni chadema..! wanatii amri tu kuogopa kupoteza ajira...!

  mshahara wao ni laki moja hao...! so pia wana uchungu na uongozi mbovu wa sisieme na kiwete
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Ni kweli, karibia vituo kibao vya daladala hapa dar kuna defender mpya zimepakiwa, yaani imewekwa kituoni imezima hakuna dereva hakuna mtu, hapo nimeiona kuanzia kituo cha kanisani- kinondoni hadi hapa gongo la mboto, malori ya jeshi ndo usiseme, thatha jamani thatha kwa thlaa kupita ndio iwe ugomvi?? mathkini thithiemu
   
 8. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Kwani lazima wafanye mazoezi ili kulinda siku ya uchaguzi?
  Ni vitisho ambavyo havina maana kabisa na huenda lengo ni kuwaogopesha wananchi. Lengo la demokrasia yoyote ya kweli lazima iwe kuwapa wananchi matumaini na sio kuwatisha.

  Ukifanya kwata barabarani inatoa ishara kuna vurugu zitatokea au kuna kuna kitu cha ajabu wanapanga kufanya. Muhimu ni kuelemisha wananchi na sio kuwatisha.
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Jana kwenye mkutano wa F. Mbowe uliofanyika NMC Arusha...Mgombea ubunge Bw Godbless Lema aliwaomba polisi hata wakiambiwa kupiga risasi raia, wamjibu risasi hazitoshi ukilinganisha na umati wa watu wanotaka mabadiliko kwani mabadiliko ni ya watanzania na siyo ya wanachadema peke yake, CHADEMA inapigania watanzania hata hao CCM/POLISI tuna wapigania maana ugumu wa maisha ni kwa wote , polisi wengi walioletwa hapa Arusha mjini zaidi ya 90% ni vijana naamini na huko ni hivyo hivyo, kama ndiyo basi vijana watakuwa na uchungu Taifa lao hiyo wana kigoma msiongope...
   
 10. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mbona sehemu zingine polisi wanacheza kwata kwa juma mara tatu!! Inaonesha polisi wa huko ni wazembe mpaka uchaguzi uje ndiyo wanafanya kwata? Mi nafikiri kwata ni zoezi la kawaida na lazima kwa polisi wetu. We kama ulitaka kuleta fujo siku ya uchaguzi acha, kapige kura kwa amani, hutafanya kitu. Nyuki haumi tu hovyo mpaka achokozwe!
   
Loading...