The King of Jews
JF-Expert Member
- Aug 11, 2013
- 478
- 109
leo mida ya saa nne posta dsm polisi wameendesha kamatakamata. ukionekana umekaa kama huna kazi umedandiwa, mara umevuliwa kofia yaani shida tupu wanachotafuta hakijulikani. nadhani imefika wakati kama hawataki wasio na kazi kuja mjini waseme tu maana watu kibao wamekamatwa na pesa kibao imetoka kama rushwa ya kuwaokoa jamaa. sio kila mtu ana kazi mjini jamani wengine tunakuja kuganga njaa hatuwezi kukaa majumbani tutakufa njaa.
angekuwa hana ningekuambia uangalie, unazidi kuthibitisha uboya wako. kusoma hujui hata picha huoni!? mimi ndio basha wake!
Enzi za mwalimu tulikuwa na vijiji vya gezaulole, wazurulaji wote wa dar walipelekwa huko wakalime viazi. Hakuna kukaa mjini bila kazi.
.......
Kamata Wote ....Kamata watembezi na wazururaji....nendeni mkalime masika ndo haya
Kwa mtindo huu utakamatwa sana.. Njoo huku mvuti tulime mihogo na mbaazi, vinalipa ukijituma.
tukianza na weweHumu jf mbona wazururaji wapo kibao?ful time wapo online,polis waje na huku
Unakamatwa kwasababu hujui sheria za nchi na hujui katiba hakuna sheria inayo mpamamlaka polisi kukamata wewe kama umekwenda mjini una haki ya msingi kwenda kokote kikatiba ilimradi tu usivunje sheria unatakiwa kumuhoji huyo polis anakushika kwa kosa gani?am sure wanoshikwa ni vibaka tu mtu na heshima yako hawawezi mbona mimi hawakunikamata na nilikuwepo mitaa ya posta kotokuwa na kazi sio kosa tatizo lenu shule mmekimbia
hayo mamlaka ya kuwalazimisha watu wafanye kazi wasiopata faida nazo yametoka wapi. kama kulima kunalipa, lima wewe lakini usilazimishe wengine!
kama nina makosa sioni hatari kukamatwa, lakini sio kukamatana kwa sababu zisizo msingi ni upumbavu wa hali ya juu wa hawa polisi. we komaa tu na kilomo chako.
leo mida ya saa nne posta dsm polisi wameendesha kamatakamata. ukionekana umekaa kama huna kazi umedandiwa, mara umevuliwa kofia yaani shida tupu wanachotafuta hakijulikani. nadhani imefika wakati kama hawataki wasio na kazi kuja mjini waseme tu maana watu kibao wamekamatwa na pesa kibao imetoka kama rushwa ya kuwaokoa jamaa. sio kila mtu ana kazi mjini jamani wengine tunakuja kuganga njaa hatuwezi kukaa majumbani tutakufa njaa.
You have improve your thinking capacity well done
umekusudia....you have TO improve your thinking capacity.....or you have improved your thinking capacity....??kwasababu kwenye hio lugha uliyotumia "You have improve your thinking capacity...."makes no sense.
Naona kama kizungu nitakuwa sijakutendea haki mkuu pole na shule yako ya kata
.......
Polisi aluta continue .........Kamata wazururaji Wote wanachafua Mji tu......na atakayejifanya mwamba apigwe tena apigwe maana tumechoka na hakuna jinsi.....mnaambiwa msije mjini bila kazi hamsikii.....please policemen arrest all who are meandering in the city with no specific job and if possible 'HIT' them at the right target using the right techniques ..
Thanks in advance.