Polisi waendeleza mauaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi waendeleza mauaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by cjilo, Mar 5, 2012.

 1. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  hivi karibuni nilikuwa katika wilaya ya urambo mkoani tabora ambapo kijana mmoja aitwae hassan mgalu akiwa katika soko la wilaya hiyo aligongwa na baiskeli na aliye mgonga alikuwa askari aliyevaa nguo zakiraia baada ya hassani kugongwa na askari huyo hali ilikuwa hivi


  hassani; kwanini umenigonga ?
  askari ;kwanini unataka nini?
  hassani;yani unanigonga na baiskeli na unasema nataka nini?


  hassani akampiga kibao askari huyo ambaye alikuwa amevaa nguo za kiraia


  kufatia hali hiyo askari huyo aliondoka na kuwafata wenzie ambao walikuwa na nguo za kirai na walimkuta hassani akicheza pull katika eneo la standi ya zamani wilayani humo ,mmmmh,wamshushia kipigo cha hali ya juu na kumvuta kwa moja kushika mguu wa kulia na mwingine mguu wa kushoto kichwa kikijibuluza chini umbali wa mita 2000
  mpaka karibu na ofisi ya ushirika ya urambo na benki ya nmb
  ambapo walimtupia katika bajaji hiyo ambayo unaiyona katika attach mmoja akiwa amemkanyaga kichwa chake,


  kutokana na mateso makali aliyoyapata hassani alipoteza maisha ,
  katika jalada lililofunguliwa kwenye kituo cha polisi urambo maelezo yaliandikwa amepigwa na wananchi wenye hasira jambo ambalo si kweli na lilileta utata kati ya wanafamila na wananchi wa eneo hilo ,ni meeandika haya ili upate picha
  je askari anahaki ya kumpiga raia ,manyanyaso haya ya raia kwa kutofahamu sheria mpaka lini,umegongwa na baiskeli,unapingwa na hata kutolewa uhai wako tutafika?
  Na Deborah Mpagama
  Source: nimeichukua kama ilivyo kutoka mjengwa blog.

  mytake:

  Hivi serikali kwa nini inwatetea sana askari pindi wanapofanya makosa hata ya wale wanaofanya kwa uwazi kabisa, inaamaana askari wameruhusiwa kuvunja sheria, kwa maoni yangu naona askari ni watu wanaoongoza kwa kuvunja sheria nchini na hawachukuliwi hatua yoyote ile, hata kama ni kesi itaenda na kuisha kimyakimya au watuhumiwa kushinda, utawala wa sheria uko wapi hapakushinda, utawala wa sheria uko wapi hapa?

  polisi.jpg
  Kijana aliyepoteza maisha akiwa chini ya ulinzi wa askari waliompiga kwenye kigari hiki
   
 2. v

  valid statement JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 160
  Ukisikia visasi ndo kama hivi. Unakuta ni mwanao, au kaka/mdogo ako ndo ametendwa hivi.
  Unambie unampojua askari aliyetenda hili unambie kama utasubiri hukumu ya mahakama.Hii nchi,kila mtu anajiona mbabe mahali alipo.
   
 3. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha sana.
   
 4. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  It is very sad

  Ni kumuomba mungu atuepushe na mitihani ya namna hii................maana come wat may yaweza kuwa applicable
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Sielewi utaratibu wa kuwa recruit polisi.
  sidhani kama wanapima akili, wengine unakuta ni mataahira tu wanapewa jukumu la kulinda raia kumbe ni vibaka
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Polisi its too much now kumbukeni mnaishi na wananchi wakiamua nao kuwageukia izo silaha hazitafua dafu
   
 7. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  siwalaumu sana askari ila nawalaumu zaidi raia waliokuwa wanaangalia hilo tukio na hata baadhi kudiriki kupiga picha. Kwa kitendo walichokuwa wanafanya hao askari,ilibidi raia wawa-treat kama majambazi/wahalifu wengine tu. Hii tabia itakoma pale tu...jini kwa jino itakapofanya kazi yake..F.U.C.K THE P.O.L.I.C.E
   
 8. obm

  obm Member

  #8
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mungu nisaidie nipate mazingira mazuri ya kulipiza hili kwa ajili ya hassan na wale wa songea na wengine wengi wanaouwawa bila taarifa kuwa hadharani. Huu ni unyama
   
 9. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  askari hao si wanafahamika,nadhani watu aliokuwa anacheza nao pool marehemu wapo na waliona tukio zima,waanzie kwa ocd kueleza ilivokuwa na askari hao watiwe ndani kwa mauaji
   
 10. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,401
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Kuripoti kwa ocd bado ni kuleta siasa kwenye kifo. Kilichopo hao walioshuhudia mwenzao akiuawa, nao wawavizie wauaji wote mmoja baada ya mwingine wawaue wote tu! Vinginevyo hakuna sababu ya kuwa na polisi wanaoua raia na kuwaacha majambazi wakiteka magari huko porini.
   
 11. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Miaka kadhaa nyuma, kuna jamaa alimkata dada yangu na kumfungia ndani ya darasa na kisa ni kuwa alimkataa.

  Kaka yangu mkubwa akapata habari na akaenda kumsaidia dada yangu kwa kumpiga jiwe huyo jamaa.

  Jamaa akaacha mlango na kumfuata kaka yangu na kumpa vibao. Kaka yangu hakukubali yaishe ila alienda na kumpa kichapo mdogo wake jamaa cha nguvu.

  Jamaa kusikia mdogo wake kapigwa, akaja na kumtembezea kipigo cha nguvu kaka yangu. Kaka yangu akasema mchezo unaendelea na akaenda kumkamata mdogo wake jamaa na kumpa kipigo tena cha nguvu. Ila siku hiyo hakuishia hapo. Akachukua nyasi na kumfunga kijana mikononi na akaanza kutafuta kibiriti/moto amchome.
  Mungu bariki watu pamoja na jamaa walimuona na wakamuwahi kabla hajamchoma. Yule jamaa kuona hivyo, ilibidi amchukue kaka yangu hadi nyumbani, akamchukua na Sister na kwenda kwa Wazee kuomba suluhu na kaka yangu. Jamaa akaahidi hatamsumbua tena dada yangu na wala kumpiga kaka yangu. Ilibidi wazee wamsihi sana kaka yangu asilipe kisasi tena kwa huyo mdogo mtu kwani walijua jamaa anaweza kumdhuru kikweli. Hadi leo, familia nzima tunaamini kuwa alikuwa hatanii na kama wasingelimkamata, angelimchoma moto mikono.

  THIS IS THE TRUE STORY.

  Puplic Enemy - Fight The Power.  Bahati mbaya wengine tumeshaanza kuzeeka. Siyo kama ile enzi tunamaliza JKT.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Ni heri ukutane na simba kuliko polisi.
   
 13. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kama ni ndugu yangu ndio aliyeuwawa na hao policcm ningelienda kuchoma kituo chao polisi au hilo Tawi la ccm, Ningehakikisha nawauwa hao polisi waliofanya hiko kitendo sitojali adhabu nitakayoipata baada ya kuua hao mbwa wa ccm:embarassed2:
   
 14. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hii sasa ni too much,imekua kawaida polisi kuua raia bila kuchukuliwa hatua,kwani hao askari hawafahamiki kwa sura mkuu?
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mhe Kikwete, kweli WaTanzania wanastahili vifo vya kinyama kiasi hiki kila kukicha mkononi mwao watu tuliowapa dhamana ya kutulinda ndani ya taifa hili ki-katiba kweli?
   
 16. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  umeona ee!!!!
   
 17. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  watu wanafahamika kabisa tena usishangae wanapewa kesi ya kuua bila kukusudia
   
 18. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #18
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  mkuu sina taarifa sana ila kwa maelezo niliyosoma hapa wanafahamika kabisa. naomba walio huko tabora watujuze zaidi
   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Saed Mwema katika hili nalo kazi itakua ni muomba radhi na watu kusahau sio? Tunajenga uhusiano wa aina gani kati ya polisi na raia hivi sasa???

  Je wale vijana walioona kijana mwenzao akichukuliwa pale walikokua wanacheza pool na jinsi gani kupatwa na mauti kinyama kiasi hicho mbele ya macho yao hadi hapo Waziri Nahodha utakua unaona kitu gani kitakachofuatia hapo kote nchini??????

  Wanaharakati nchini, enyi walinzi wa haki za binadamu mko wapi wakati haya yote yakiendelea kuwakumba wananchi kila kona ya nchi kila kukicha?
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wabunge wa vyama vyote mnaotoka Tabora na Songea tunaomba kusikia sauti zenu juu ya mauaji haya yanayoendelea kwa wananchi mikononi mwao polisi.

  Mungu apokee roho yako upumzike kwa amani kijana mwenzetu Hassani na wafiwa wote huko Tabora.
   
Loading...