Polisi waendeleza mauaji

Saed Mwema katika hili nalo kazi itakua ni muomba radhi na watu kusahau sio? Tunajenga uhusiano wa aina gani kati ya polisi na raia hivi sasa???

Je wale vijana walioona kijana mwenzao akichukuliwa pale walikokua wanacheza pool na jinsi gani kupatwa na mauti kinyama kiasi hicho mbele ya macho yao hadi hapo Waziri Nahodha utakua unaona kitu gani kitakachofuatia hapo kote nchini??????

Wanaharakati nchini, enyi walinzi wa haki za binadamu mko wapi wakati haya yote yakiendelea kuwakumba wananchi kila kona ya nchi kila kukicha?


nafikiri wananchi tuchukue hatua sasa kama watu wa kutulinda ndo wanatuua . basi nasi tuunganishe nguvu kwa pamoja
 
Ukisikia visasi ndo kama hivi. Unakuta ni mwanao, au kaka/mdogo ako ndo ametendwa hivi.
Unambie unampojua askari aliyetenda hili unambie kama utasubiri hukumu ya mahakama.Hii nchi,kila mtu anajiona mbabe mahali alipo.

Siyo kila mtu ni mbabe bali mafisadi na timu yao wanayoshirikiana nayo ambayo ni police ndo wanaofanya ubabe wakiamini hela zao ni kila kitu
 
Sielewi utaratibu wa kuwa recruit polisi.
sidhani kama wanapima akili, wengine unakuta ni mataahira tu wanapewa jukumu la kulinda raia kumbe ni vibaka

Mkuu mbona police wapo wa kila aina? Kuna wezi, vichaa, matahahira, wasiojua wajibu wao na mengineyo mengi
 
siwalaumu sana askari ila nawalaumu zaidi raia waliokuwa wanaangalia hilo tukio na hata baadhi kudiriki kupiga picha. Kwa kitendo walichokuwa wanafanya hao askari,ilibidi raia wawa-treat kama majambazi/wahalifu wengine tu. Hii tabia itakoma pale tu...jini kwa jino itakapofanya kazi yake..F.U.C.K THE P.O.L.I.C.E

Isitoshe hawakuwa na jezi wangelabuliwa vizuri sana tu
 
Askari ndomana wengi wao ni njaa kali shida na dhiki zimewaandama utadhani hawana kazi, kwasababu ya dhurma na unyanyasaji!
 
kufatia hali hiyo askari huyo aliondoka na kuwafata wenzie ambao walikuwa na nguo za kirai na walimkuta hassani akicheza pull katika eneo la standi ya zamani wilayani humo ,mmmmh,wamshushia kipigo cha hali ya juu na kumvuta kwa moja kushika mguu wa kulia na mwingine mguu wa kushoto kichwa kikijibuluza chini umbali wa mita 2000
mpaka karibu na ofisi ya ushirika ya urambo na benki ya nmb
ambapo walimtupia katika bajaji hiyo ambayo unaiyona katika attach mmoja akiwa amemkanyaga kichwa chake,


Source: nimeichukua kama ilivyo kutoka mjengwa blog.

mytake:

Hivi serikali kwa nini inwatetea sana askari pindi wanapofanya makosa hata ya wale wanaofanya kwa uwazi kabisa, inaamaana askari wameruhusiwa kuvunja sheria, kwa maoni yangu naona askari ni watu wanaoongoza kwa kuvunja sheria nchini na hawachukuliwi hatua yoyote ile, hata kama ni kesi itaenda na kuisha kimyakimya au watuhumiwa kushinda, utawala wa sheria uko wapi hapakushinda, utawala wa sheria uko wapi hapa?

View attachment 48661
Kijana aliyepoteza maisha akiwa chini ya ulinzi wa askari waliompiga kwenye kigari hiki


Ni wiki chache tu zimepita toka mauaji ya kinyama yafanyike kule Songea.

Kisha IGP aliomba msamaha kwa maneno ya upole sana kama ilivyo hapa chini:

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema, amesema amesikitishwa na kusononeshwa sana na mauaji ya watu wanne yaliyofanywa hivi karibuni katika mji wa songea na vijana wake askari wa jeshi la polisi, ndiyo maana amepeleka kikosi maalum toka makao makuu ili kubaini ukweli wa hali halisi iliyojiri. Said Mwema, ameyasema hayo hivi punde, wakati alipokutana na kamati ya kudumu ya bunge inayoshughulika na maswala ya ukimwi, inayoongozwa na mhe. Lediana Mng'ong'o.

Akiongea kwa upole na unyenyekevu, hata kabla hajaulizwa, IGP, alifafanua kuwa yeye binafsi ameumizwa sana moyoni mwake na mauaji ya raia wasio na hatia. "hivi ninavyozungumza nina kidonda moyoni mwangu," alisema IGP akisisitiza kuwa, "mimi [said mwema] binafsi ninsingependa kuona hali hii inaendelea."

Kufuatia hali hiyo, mbunge wa Ludewa, mhe. Filikunjombe, alimtaka IGP aombe radhi, kuthibitisha kauli yake kwamba ni kweli ana 'kidonda moyoni' kinachosababishwa na mauaji ya watendaji wake wa chini.

Pamoja na kukubali rai ya Mhe. Filikunjombe, IGP Mwema, amesema askari waliofanya yale mauaji, ikibainika wametumia 'nguvu ya ziada', watachakuliwa hatua za kinidhamu. Na hivyo IGP amewataka wabunge wasubiri ripoti ya uchunguzi.

My take: Ni jambo la busara kwa IGP Mwema kuomba radhi kwa makosa yalosababishwa na askari wake. Huu ni uungwana. Hata hivyo, Mawaziri nao wajifunze kuwajibika kwa makosa ya walio chini yao.
(Maneno ya mmoja wa mchangiaji hapa JF)


JE, NA HILI IGP MWEMA ATAOMBA MSAMAHA AU ATACHUKUA UAMUZI MGUMU??



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
UONGOZI MZIMA WA HII WIZARA YA KI-POLISI HAKIKA WANANCHI HATUNA FURAHA TENA HATA CHEMBE NA UBABAISHAJI WENU KI-KAZI, KUKURUPUKA KILA LEO KAMA ZIMAMOTO HUKU WANANCHI TUKITEKETEA BILA HURUMA KATIKA MIKONO YA POLISI

Ni hatari sana raia polisi kuendelea kuua raia tena kinyama kila leo bila ya kuchukuliwa hatua zozote kisheria.

Kitendo cha hao polisi mwenzao kurudi kituoni kwenda kuwaita na kurudi nakuanza na shambulio kwa kijana Hassani na kisha kuendelea kumburuza chini wastani wa umbali wa kilometa 2, ni wazi kuwa mauaji haya yalikua ni mauaji ya KUDHAMIRI kwa kufuata mpango jinsi walivyojiwekea kabla ya kutoka kituoni.

Kwa jinsi hii si tu kwamba mahusiano kati ya polisi na umma utahama kuwa kama ule wa paka na chui tu bali sasa ni kwamba watu tunaanza kuhoji:

(1) Viwango vya uadilifi katika taratibu zote za kuwapata watu wanaojiunga na jeshi letu hili,

(2) aina na ubora wa mafunzo wanayopata kuwaandaa kweli kuwa WALINZI WA AMANI NA UTULIVU

(3) Mafunzo na uelewa wa polisi uhusiano wake na majukumu kwa raia , somo juu ya haki za binadamu na sheria za nchi

(4) Naam, hivi sasa tunatamani kuelewa hata viwango vya elimu kwa watu wanaojiunga na jeshi hili, viwango vya elimu vya wale wanaoitwa wakufunzi wa polisi pia,

(5) Kadiri matukio ya kustaajabisha yanavyoendelea kutokea nchini wananchi sasa tungependa pia tuelewe UBORA WA MAZINGIRA YA KAZI KWA POLISI kama vile aina ya ofisi wanazotumia, nyumba wnazoishi, mishahara na marupurupu wanayopata, na kadhalika

KWA UJUMLA WANANCHI HATUNA FURAHA HATA KIDOGO NA UONGOZI MZIMA WA VUAI NAHODHA, SAED MWEMA NA KATIBU MKUU WA HIYO WIZARA KWA JINSI WANANCHI TUNAVYOENDELEA KUUAUA KILA KONA YA NCHI KINYAMA NA POLISI NA WAO KUENDELEA KUONEKANA WAKO JUU YA SHERIA.



nafikiri wananchi tuchukue hatua sasa kama watu wa kutulinda ndo wanatuua . basi nasi tuunganishe nguvu kwa pamoja
 
Wabunge wa Tabora:

Rage - Tabora mjini:
Rage.jpg


Prof. Juma Kapuya:
Kapuya4.jpg


Kaka Samuel Sitta:
SIX.jpg

Wabunge wa vyama vyote mnaotoka Tabora na Songea tunaomba kusikia sauti zenu juu ya mauaji haya yanayoendelea kwa wananchi mikononi mwao polisi.

Mungu apokee roho yako upumzike kwa amani kijana mwenzetu Hassani na wafiwa wote huko Tabora.
 
Back
Top Bottom