Polisi waendeleza mauaji holela - Kasulu

Polisi waendeleza mauaji holela - Kasulu

Sio wamesababisha kifo, hapana, bali wameua kwa kutumia "flying object"
Mkuu si unajua tena taarifa za kipolisi "UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA","INAHISIWA NDIYO ILISABABISHA KIFO CHAKE"
 
Hakuna haja ya kuwakamata polisi. Badala yake wangewaachia na kuwauliza wananchi nini adhabu ya wauaji hawa. Simpo. Wananchi sasa wamechoka.
Jeshi la polisi mkoani Kigoma,linawashikilia askari wake wawili kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mkazi mmoja wa kijiji cha Herushingo,tarafa ya Makere,wilaya ya Kasulu. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kamanda wa polisi mkoani humo,Fraisser Kashai,alisema tukio hilo lilitokea Decemba 25,mwaka huu,saa nne usiku katika kijiji hicho.

Aliwataja askari hao kuwa ni D.8622 CPL,Peter na G.1236 PC Sunday wa kituo kidogo cha Rerushingo ambapo wanadaiwa kumshambulia Bw.Gasper Mussa (36),ambaye ni mkulima katika baa waliyokuwa wanakunywa na baada ya kumpiga,walimfikisha kituoni hapo. Alisema Decemba 26 mwaka huu,mkuu wa kituo hicho alitoa taarifa kituo cha polisi kwa SP Sospeter kunguru kuwa mtuhumiwa alikuwa mgonjwa lakini alifariki muda mchache baada ya kufikishwa katika hospitali ya wilaya ya Kasulu.

"Chanzo cha ugomvi ni baada ya marehemu kushindwa kulipa vinywaji alivyokunywa ndipo askari walipoanza kumshambulia na kumsababishia maumivu yaliyosababisha kifo chake," Alisema kutokana na tukio hilo,askali hao wamekamatwa na wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo hasa cha ugomvi huo na kama itabainika walihusika moja kwa moja watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya mauaji.

Chanzo cha Habari:Gazeti la Majira la Desemba 28,2012,habari hii inapatikana ukurasa wa 3.

My Take Kadri siku zinavyozidi kwenda, mmomonyoko wa maadili kwa askari wetu unazidi kukuwa.Askari wetu wamejenga tabia ya kuchukua sheria mkononi (Instant justice).Hii pia imezoeleka hata kwa sisi raia,utasikia mtu anakwambia "unauliza makofi polisi" yaani anamaanisha askari ana haki na kuchukua sheria mikononi pale anapojisikia kufanya hivyo.Tabia hii ni mbaya na inaenda kinyume na kaki za binadamu.Kuna haja ya kufanya uchunguzi yakinifu, ili kujua kama askari wetu huwa wanafundishwa nini kwenye vyuo vya polisi,inawezekana huwa kuna mafunzo maalumu wanaopewa ambayo yanakinzana na haki za binadamu.
 
Kwa hali hii ya police kujichukulia sharia mkononi sasa imechukua kasi ndani ya Nchi yetu inayodai ya Amani na utulivu!

Na kwa jinsi ilivyo hautaacha kusikia kesho kutwa askari hao wako huru!
Mkuu hapo hakuna kitu ni sawa na kesi ya nyani apelekwe ngedere akaitolee maamuzi!
 
Marehemu kama ilivosemwa alikuwa anamdai mmoja wa askari polisi Tsh 5000 (Elfu tano) pasi shaka deni la siku nyingi. Siku ya tukio marehemu alikuwa kwenye grocery inayomilikiwa na askari anayedaiwa, akanywa pombe alipotakiwa kulipa pesa marehemu alimjibu yule polisi "tukatane kule kwenye deni". Basi askari huyo na mwenzie wakamshushia kichapo cha haja kisha wakamsweka rumande (cjui kwa kesi gani). Umbulula wa polisi na kujiona wako juu once again
 
Hakuna haja ya kuwakamata polisi. Badala yake wangewaachia na kuwauliza wananchi nini adhabu ya wauaji hawa. Simpo. Wananchi sasa wamechoka.
Ndiyo maana wale wananchi wa mkoa wa Kagera waliamua kumalizana na wale askari wawili,kwani walijua watapigwa danadana na maneno ya kipolisi "UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA".Kwa hali hii polisi hawaaminiki tena kwenye jamii yetu!
 
Mkuu si unajua tena taarifa za kipolisi "UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA","INAHISIWA NDIYO ILISABABISHA KIFO CHAKE"
Ingekuwa ni huku kila kitu kinachunguzwa...hata kama mtu alikufa miaka 50 iliyopita ili mradi kaburi lake linapatikana...ni mambo ya "Carbon Fourteen"
 
Ingekuwa ni huku kila kitu kinachunguzwa...hata kama mtu alikufa miaka 50 iliyopita ili mradi kaburi lake linapatikana...ni mambo ya "Carbon Fourteen"
Huko wapi mkuu?Sisi bado tunaendelea na mambo yetu ya kibongobongo ya "UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA HATA BAADA YA MIAKA KUMU BAADA YA TUKIO"Teh teh teh!
 
Huko wapi mkuu?Sisi bado tunaendelea na mambo yetu ya kibongobongo ya "UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA HATA BAADA YA MIAKA KUMU BAADA YA TUKIO"Teh teh teh!

"An imminent disaster"(We acha tu)Mkuu TUKUTUKU maisha ni kutafuta ila kesho nitatua JKIA, NBO Kenya, na baadaye Arusha na Dar before kuondoka. Anyway maisha ndivyo yalivyo..Nina wadau wa kuonana nao.
 
"An imminent disaster"(We acha tu)Mkuu TUKUTUKU maisha ni kutafuta ila kesho nitatua JKIA, NBO Kenya, na baadaye Arusha na Dar before kuondoka. Anyway maisha ndivyo yalivyo..Nina wadau wa kuonana nao.
Mkuu karibu sana tulikarabati linchi letu!
 
tutoe muda kanchi kanaelekea kuzuri huenda ..........nani alijua lema angeshinda rufaayake?:target:
 
[h=3][/h]




[TD="align: center"] [/TD]

[TD="align: center"] Kamanda Fraiser Kashai. [/TD]


Jeshi la Polisi mkoani Kigoma
linawashikilia askari wake wawili kwa tuhuma za kumpiga na kusababisha
kifo cha mkazi wa kijiji cha Herushingo, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma,
Gasper Mussa.


Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Fraiser Kashai,
aliwataja askari hao kwa waandishi wa habari mjini hapa kuwa ni mwenye
namba NCC 8622 Koplo Peter na G.1236 Konstebo Sunday. Alisema wawili hao
wanadaiwa kumpiga Mussa walipokuwa kwenye kilabu cha pombe usiku wa
Sikukuu ya Krismasi.


Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda Kashai, Mussa
alifariki siku moja baada ya kupata kipigo hicho alipokuwa akipelekwa
hospitalini baada ya kukaa mahabusu kwa siku moja.


Akisimulia tukio
hilo, Kamanda Kashai alisema siku ya tukio, Mussa na askari hao walikuwa
wakinywa pombe katika kilabu cha pombe na wakati wakinywa, ikatokea
vurugu ambapo inadaiwa kusababishwa na Mussa kukataa kulipa pombe
aliyokunywa.


Baada ya Mussa kukataa kulipa, Kamanda Kashai alisema
askari hao ambao kwa sasa wanahifadhiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi
wilayani Kasulu, walianza kumuadhibu kwa kumpiga na baadaye walienda
kumlaza mahabusu.


Hata hivyo, siku iliyofuata, Kamanda Kashai
alisema Mussa alizidiwa ndipo Mkuu wa Kituo cha Polisi Herushingo,
alianza jitihada za kumpeleka Mussa hospitali, lakini alifariki mikononi mwa polisi kabla ya kufikishwa hospitali. Alisema baada ya tukio hilo, alituma askari wake kufuatilia kwa undani kujua kile kilichotokea ili wachukue hatua.


Kwa sasa Kamanda Kashai alisema hatua za kijeshi kwa askari hao
zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuwavua hadhi ya kijeshi waliyonayo
kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.


Katika tukio lingine Polisi mkoani Kigoma inamshikilia Hassan Shija, mwalimu wa fani ya umeme katika Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (Veta)mkoani Kigoma kwa tuhuma za kumpiga mapanga na kumjeruhi mke wake sehemu mbalimbali za mwili wake.


Kamanda Kashai alimtaja mwanamke huyo kuwa ni Rida Mbili ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kigoma ya Maweni na kwamba chanzo cha mgogoro huo ni wivu wa mapenzi.



Chanzo : Zero 99
 
Tatizo askar wa kibongo wanajiona wapo juu ya sheria. Hili ni tatizo la jk na ccm yake. Kweli wananchi wako wanauliwa makusudi na jeshi we bado upo kimya sasa we ni raisi au?
 
Raia mmoja mwenyeji wa Kata ya Heru - Ushingo Wilayani kasulu, ameuwawa na Polisi kwa kupigwa risasi, baada ya fujo iliyotokana na tofauti za njia ya malipo ya huduma ya kinywaji katika kusherehekea Krismas.

Marehemu awali alikuwa anamdai Askari polisi. Marehemu huyo akaamua kwenda kupata kinywaji kwenye grocery inayomilikiwa na Askari polisi huyo.

Baada ya Kupata kinywaji, Askari huyo aliomba kulipwa, na kwa kuwa marehemu alikuwa anamdai Askari yule, Marehemu akamwambia Askari akate pesa yake kwenye Deni alilokuwa anamdai. Hapo ndipo mwanzo wa tatizo, lililopelekea kichapo, hadi matumizi ya silaha yaliyopelekea kifo.

Sakata hili analifuatilia kwa karibu Mbunge wa eneo hilo Mh. Agripina Buyogera (NCCR).

Chanzo:
Radio Kwizera
Policcm ni hatari, utaskia kesi inaisha kiaina, inabid tuwaroge tu.😛ainkiller:
 
Tusiwalaumu hawa jamaa,maana ndo wanachokijua hapa duniani,wanaenda kozi ya kupiga na kujificha ,sasa c ndo matumizi ya kozi waliosomea?kama vp mtaala wao ubadilishwe ulingane wa nchi zingine!!
 
Jamani tuache ushabiki je ni polisi wangapi wameuawa tujiulize hilo swali

Mfano ulio hai juzi kati hapa huko Iringa kuna Askari aliuwawa baada ya kupigwa na kupelekea mauti kumkuta.,,kwan polisi ndio wana roho za chuma...mbona hamjasema bana hamjakemea.

Au kwa mfano kamanda aondoe askar wake wote unafikir utakuwa na hali gani..'@
 
Back
Top Bottom