Polisi waendeleza mauaji holela - Kasulu

Polisi waendeleza mauaji holela - Kasulu

Mangaline

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2012
Posts
1,045
Reaction score
222
Raia mmoja mwenyeji wa Kata ya Heru - Ushingo Wilayani kasulu, ameuwawa na Polisi kwa kupigwa risasi, baada ya fujo iliyotokana na tofauti za njia ya malipo ya huduma ya kinywaji katika kusherehekea Krismas.

Marehemu awali alikuwa anamdai Askari polisi. Marehemu huyo akaamua kwenda kupata kinywaji kwenye grocery inayomilikiwa na Askari polisi huyo.

Baada ya Kupata kinywaji, Askari huyo aliomba kulipwa, na kwa kuwa marehemu alikuwa anamdai Askari yule, Marehemu akamwambia Askari akate pesa yake kwenye Deni alilokuwa anamdai. Hapo ndipo mwanzo wa tatizo, lililopelekea kichapo, hadi matumizi ya silaha yaliyopelekea kifo.

Sakata hili analifuatilia kwa karibu Mbunge wa eneo hilo Mh. Agripina Buyogera (NCCR).

Chanzo:
Radio Kwizera
 
CCM OYEEEEE
wanatimiza matakwa ya bosi wao CCM, anataka damu nyingi ya wanadamu wasio na hatia ili waweze kushinda uchaguzi mkuu ujao 2015
 
Marehemu alikua anafanya bonafide claim of right.
askari polisiwanajihisi wako juu ya sheria.
 
Hawa wamezidi sana tena wanatabia ya kujichukulia sheria mkononi,juzi polisi wakituo kidogo cha polisi kimara wametukuta saa 11:00 usiku bar wakaanza kutupiga bila kuuliza kwa nn tupo hapa wakatupora simu na pesa zetu yaani hawa ni majambazi badala ya kutulinda wanatuibia
 
Tatizo sahiz ktk jesh la polisi uzalendo umetoweka ndo maana askar kufanya ki2 kama hicho haoni tatizo.
 
mauaj ya kasuru wap na wap?ilo nikosa kama makosa mengne,uchunguz ukikamilika sheria itachukua mkondo wake tu.tutulie tu
 
Askari wa tanzania kuingia ufalme wa mbinguni ni ngumu kama ilivo kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano!
 
Ni mmiliki wa grocery ambaye ni askari polisi. ametenda kosa hilo akiwa ktk utekelezaji wa kazi za polisi au kama mmiliki wa grocery wakati anadai malipo yake.
 
Hivi hawo nao wa wapi, hawakuona mfano wa Ngara!!
 
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linawashikilia askari wake wawili kwa tuhuma za kumpiga na kusababisha kifo cha mkazi wa kijiji cha Herushingo, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, Gasper Mussa. Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Fraiser Kashai, aliwataja askari hao kwa waandishi wa habari mjini hapa kuwa ni mwenye namba NCC 8622 Koplo Peter na G.1236 Konstebo Sunday. Alisema wawili hao wanadaiwa kumpiga Mussa walipokuwa kwenye kilabu cha pombe usiku wa Sikukuu ya Krismasi.

Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda Kashai, Mussa alifariki siku moja baada ya kupata kipigo hicho alipokuwa akipelekwa hospitalini baada ya kukaa mahabusu kwa siku moja.Akisimulia tukio hilo, Kamanda Kashai alisema siku ya tukio, Mussa na askari hao walikuwa wakinywa pombe katika kilabu cha pombe na wakati wakinywa, ikatokea vurugu ambapo inadaiwa kusababishwa na Mussa kukataa kulipa pombe aliyokunywa.

Baada ya Mussa kukataa kulipa, Kamanda Kashai alisema askari hao ambao kwa sasa wanahifadhiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi wilayani Kasulu, walianza kumuadhibu kwa kumpiga na baadaye walienda kumlaza mahabusu. Hata hivyo, siku iliyofuata, Kamanda Kashai alisema Mussa alizidiwa ndipo Mkuu wa Kituo cha Polisi Herushingo, alianza jitihada za kumpeleka Mussa hospitali, lakini alifariki mikononi mwa polisi kabla ya kufikishwa hospitali.

Alisema baada ya tukio hilo, alituma askari wake kufuatilia kwa undani kujua kile kilichotokea ili wachukue hatua.Kwa sasa Kamanda Kashai alisema hatua za kijeshi kwa askari hao zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuwavua hadhi ya kijeshi waliyonayo kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Katika tukio lingine Polisi mkoani Kigoma inamshikilia Hassan Shija, mwalimu wa fani ya umeme katika Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) mkoani Kigoma kwa tuhuma za kumpiga mapanga na kumjeruhi mke wake sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda Kashai alimtaja mwanamke huyo kuwa ni Rida Mbili ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kigoma ya Maweni na kwamba chanzo cha mgogoro huo ni wivu wa mapenzi.
 
Dawa siku hizi tunaijua hivyo ikipatikana nafasi hatusubiri tena muanze kuficha ficha mambo nasi wananchi tunatoa adhabu hapo hapo.
 
polisi 2 wamemuua mtu 1,kisa polisi kudaiwa na marehemu!wa LHRC waongeze idadi kule the HAGUE,this too much!
 
BONGOLALA vp?Ameuliwa wapi na kisa kudaiwa nini mbona habari yako kama ya shigongo???
 
Last edited by a moderator:
Jeshi la polisi mkoani Kigoma,linawashikilia askari wake wawili kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mkazi mmoja wa kijiji cha Herushingo,tarafa ya Makere,wilaya ya Kasulu. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kamanda wa polisi mkoani humo,Fraisser Kashai,alisema tukio hilo lilitokea Decemba 25,mwaka huu,saa nne usiku katika kijiji hicho.

Aliwataja askari hao kuwa ni D.8622 CPL,Peter na G.1236 PC Sunday wa kituo kidogo cha Rerushingo ambapo wanadaiwa kumshambulia Bw.Gasper Mussa (36),ambaye ni mkulima katika baa waliyokuwa wanakunywa na baada ya kumpiga,walimfikisha kituoni hapo. Alisema Decemba 26 mwaka huu,mkuu wa kituo hicho alitoa taarifa kituo cha polisi kwa SP Sospeter kunguru kuwa mtuhumiwa alikuwa mgonjwa lakini alifariki muda mchache baada ya kufikishwa katika hospitali ya wilaya ya Kasulu.

"Chanzo cha ugomvi ni baada ya marehemu kushindwa kulipa vinywaji alivyokunywa ndipo askari walipoanza kumshambulia na kumsababishia maumivu yaliyosababisha kifo chake," Alisema kutokana na tukio hilo,askali hao wamekamatwa na wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo hasa cha ugomvi huo na kama itabainika walihusika moja kwa moja watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya mauaji.

Chanzo cha Habari:Gazeti la Majira la Desemba 28,2012,habari hii inapatikana ukurasa wa 3.

My Take Kadri siku zinavyozidi kwenda, mmomonyoko wa maadili kwa askari wetu unazidi kukuwa.Askari wetu wamejenga tabia ya kuchukua sheria mkononi (Instant justice).Hii pia imezoeleka hata kwa sisi raia,utasikia mtu anakwambia "unauliza makofi polisi" yaani anamaanisha askari ana haki na kuchukua sheria mikononi pale anapojisikia kufanya hivyo.Tabia hii ni mbaya na inaenda kinyume na kaki za binadamu.Kuna haja ya kufanya uchunguzi yakinifu, ili kujua kama askari wetu huwa wanafundishwa nini kwenye vyuo vya polisi,inawezekana huwa kuna mafunzo maalumu wanaopewa ambayo yanakinzana na haki za binadamu.
 
Kwenye taarifa ya habari ya ITV saa mbili usiku huu,wame-ripoti kifo cha raia mmoja huko kasulu kilichosababishwa na polisi kwa jeuri yao.
kisa cha kifo hicho,inasemekana raia huyo asiekua na hatia alikua akimdai mmoja wa polisi huyo fedha,polisi badala ya kulipa deni wakamshushia kipigo na kumsweka rumande hadi mauti yalipomkuta

NB:i ssue kama hizo za askari kujiona ni miungu watu zinazidi kuenea kila kukicha wakijiona kua wao ni wao wakitakacho lazima kiwe,wanaudhi.juzi tu kwenye X-mas mitaa ya segerea nimekwaruzana na magereza mmoja kisa aligoma kunipisha njiani eti anaongea na simu wakati nampigia honi ya gari,badae akadai eti ataniweka ndani.mpuuzi huyo!
 
Sio wamesababisha kifo, hapana, bali wameua kwa kutumia "flying object"

Wananchi wa Kasulu wanapaswa kulaumiwa kwa kujiruhusu kuwa waathirika wa unyama wa polisi. Kwanini wasifanye kamajirani zao wa Ngara waliowaua polisi wawili hivi karibuni baada ya kumuonea mwenzao? Kwa vile polisi wetu wameamua kuwa wauaji badala ya walinzi wa wananchi, ni haki na wajibu kwa wananchi kujilinda kwa kuhakikisha anayewaua nao wanamuua. Mwisho wa mchezo na ngoma droo.
Kwenye taarifa ya habari ya ITV saa mbili usiku huu,wame-ripoti kifo cha raia mmoja huko kasulu kilichosababishwa na polisi kwa jeuri yao.
kisa cha kifo hicho,inasemekana raia huyo asiekua na hatia alikua akimdai mmoja wa polisi huyo fedha,polisi badala ya kulipa deni wakamshushia kipigo na kumsweka rumande hadi mauti yalipomkuta

NB:i ssue kama hizo za askari kujiona ni miungu watu zinazidi kuenea kila kukicha wakijiona kua wao ni wao wakitakacho lazima kiwe,wanaudhi.juzi tu kwenye X-mas mitaa ya segerea nimekwaruzana na magereza mmoja kisa aligoma kunipisha njiani eti anaongea na simu wakati nampigia honi ya gari,badae akadai eti ataniweka ndani.mpuuzi huyo!
 
Meku ungeweka ufafanuzi kidogo hivi ingependeza zaidi.

Sio vizuri kutumia madaraka vibaya, Polisi safari bado ndefu ndugu zangu.

Pole kwa wanafamilia, ndugu na jamaa kwa jumla.
Rest In Peace
 
Kwa hali hii ya police kujichukulia sharia mkononi sasa imechukua kasi ndani ya Nchi yetu inayodai ya Amani na utulivu!

Na kwa jinsi ilivyo hautaacha kusikia kesho kutwa askari hao wako huru!
 
Back
Top Bottom