Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire amekiri kupata taarifa za awali za tukio la kuuawa na Polisi kwa abiria aliyekuwa katika Gari lililokaidi Amri ya Polisi ya kusimama. Kamanda Bwire ameeleza kufuatilia tukio hilo ili apate taarifa kamili. Alisema kuwa: "Ni kweli nimepata taarifa hizo lakini nazifuatilia ili nijue kwa undani kwa sababu tukio lenyewe lina utata."
Shuhuda wa ajali hiyo ameeleza kuwa, dereva wa Gari aina ya Canter aliyekuwa akiendesha kwa zaidi ya spidi 50 kutokea Iringa, alisimamishwa na Polisi lakini alikaidi Amri ya kusimama ndipo askari hao wa usalama barabarani wakaanza kulifukuza. Alieleza kuwa, Polisi walipokuwa wakilifukuza Gari hilo walipiga risasi kwenye kioo cha ubavuni upande aliokaa abiria na inadaiwa ilimjeruhi kichwani na kufariki dunia.
Hata hivyo, Polisi walipifika maeneo ya Kinyanambo C walipiga risasi katika gurudumu la gari na kumlazimu dereva kusimama.
Baada ya marehemu na dereva kupakiwa kwenye gari la Polisi, dereva alikuwa akiwalalamikia askari polisi: kwa nini mmemuua ndugu yangu, kwa nini mmemuua ndugu yangu?
Wajuvi wa mambo ya ajali, hebu angalieni Picha ya gari na eneo lililoharibiwa kioo halafu ufikirie kuwa, risasi ilipigwa wakati wanakimbizana. Akili za kuambiwa?