figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Polisi wa India walikuwepo eneo la tukio wakati Mwanafunzi wa kike wa Kitanzania anapigwa na kudhalilishwa. Walishindwa hata kupiga risasi hewani.
Hata kabla ya kudhalilishwa, Mwanafunzi huyo ambaye ni Mtanzania, alipanda gari la abiria akijiokoa toka kwa wale vijana waliokuwa wanampiga, lakini abiria nao waliokua ndani ya gari wakamsukumia nje tena. Poleni ndugu zetu Mlioko India.
Hata Wanafunzi wengine walipoenda kutoa Taarifa Polisi, hawakusikilizwa wala kupewa msaada wowote. Huu ubaguzi inatakiwa kama taifa tuukemee kwa nguvu zote.
Sitaki kuamini kama haya ndo maisha wenzetu wanaishi nje ya nchi.
Serikali itumie mkasa huu kukomesha tabia ya wanafunzi wa kigeni kutoka bara la Afrika kudhalilishwa nchini India.
Mtanzania anayesoma India amepigwa, kuvuliwa nguo na kisha kulazimishwa kutembea akiwa uchi na kundi la watu nchini humo India.
Habari zaidi soma=>Tanzanian girl (21-year-old) stripped, assaulted by locals in Bengaluru, India.