Polisi VS Majambazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi VS Majambazi

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mkaa Mweupe, Jan 20, 2010.

 1. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Katika siku za karibuni kumekuwa na habari mbalimbali zikiripotiwa kuwa Polisi wamefanikiwa kuyaua Majambazi kadhaa katika matukio ambayo yalisababisha kurushiana risasi.

  Jambo linalonishangaza ni kuwa,
  "Je, kunakuwa na ni nani hasa anatakiwa kuthibitisha maelezo yanayotolewa na Polisi?"

  "Hivi inakuwaje ni Majambazi tu ndio wanauwawa na sio Polisi katika matukio ya kurushiana risasi?"

  Nawasilisha.
   
 2. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kwahiyo ungependa Polisi wauwawe na majambazi sio?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Polisi ni Proffessionals wa kutumia silaha unlike majambazi, ambao mostly hawana hata mahala pa kujaribishia silaha zao, ndio sababu wanashindwa kupambana na polisi. Hakuna jibu zaidi ya hilo.
   
 4. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kwa kuwa polisi wanakuwa wamejiandaa vema kwa tukio inakuwa rahisi kuwakabili majambazi. Wakishtukizwa mbona huwa wanakula kona mbaya?
   
 5. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Nadhani mshkaji swali lake ni la kimsingi. Ni kwamba in most cases(mara nyingi) unakuta polisi ndo majambazi wenyewe....kwa mfano muulize Zombe na wafanyabiashara wake wa madini alivyowauwa na kuwapora na akashinda kesi kisanii na kifisadi.

  Kinachotokea ni kuwa wakishakosa kuleta 10% mara baada ya kupiga issue, au ikitokea wamepiga kwa kigogo kimakosa, au polisi wamelaumiwa sana na vyombo vya habari, hapo ndipo baadhi yao hutolewa muhanga.

  Kwa hiyo wanapoandaa kupiga kwa kuwa ni timu ileile, wanazungukana kimtindo, sasa wale wasiokuwa na upolisi halali ndo huwa matatani kwa hiyo wanapigwa shaba kwa mfano wakiwa ndo wanajiandaa pengine Buguruni, unakuta kama watano hivi wanauawa, halafu maiti zinapelekwa Amana Ilala ili kuzuga kuwa wanahitaji matibabu kwa watuhumiwa wa ujambazi ambao wako mahututi. Inakuwa confirmed kuwa wamekufa.

  Taarifa ya habari sasa......Watuhumiwa wa Ujambazi watano wameuawa na polisi baada ya kurushiana risasi na polisi huko eneo la kimara baruti. Kamanda wa Polisi kanda maalumu amethibitisha tukio hilo..............

  Lakini yako matukio mengine huwa hayatengenezwi na katika haya pande zote mbili huwa zinapata madhara. Majambazi, wengi wao wana mafunzo ya kijeshi kwa hiyo si rahisi watano wakauawa bila madhara hata kidogo kwa askari watatu waliopambana nao...ebo!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 6. Kionambele

  Kionambele JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh! Mbona naona maruweruwe. Naomba urudie hii kwa Lugha rahisi.
   
 7. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Sorry. I'm not from Kigoma.
   
 8. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  sasa ulitaka police wauawe? au nawewe ni ja....i? am sory
   
 9. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hili suala hata mimi linanipa wasiwasi,majambazi wanafanya vibaya kuua watu,lakini polisi wasijisifie kuyaua majambazi kwani wanahalalisha sheria mkononi. Kama kuna uwezekano wa kuyakamata yakamatwe.
   
 10. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Jambazi ambaye kuna uhakika pasi shaka kuwa ni jambazi akikutwa kwenye tukio auawe tu, hakuna sababu ya kutupotezea muda wa wanasheria wetu kubishana bure mahakamani na jambo lililoko wazi. Shida ya hizi sheria ni kuwa hazitoi ile haki halisi, zinatoa hukumu kulingana na mabishano ya wanasheria, ambapo wakati mwingine jambazi huonekana hana hatia na kuachiwa huru, ilhali anayebambikiziwa kesi ya ubakaji hufungwa kifungo cha maisha!
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  polisi hawana haki ya kuua mtu wanayendhania ni majambazi , naomba tuelewe hili. Polisi wana uhakika gani 100% kuwa wanaowauwa ni majambazi? Kuuwa iwe ni in very exceptional cases isiwe ni kawaida na kama inatokea polisi inbidi wasikitikie kitendo hicho na sio kushangilia jamani.

  Na kama watauwa basi wajisubmit wenyewe kwenye inquest ili ionekane kuwa polisi walikuwa justified kufanya hivyo na sio vinginevyo.
   
 12. bona

  bona JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  well the answer is simple, mapolisi most of the time wana wa outnumber majambazi na kama majambazi wakiwa wengi kuliko polisi, polisi hua hawa wa engage ktk fire fight, pili mapolisi wanakua wamejiposition vizuri kuliko majambazi na majambazi wanakua anxious kwani jinsi mda unavyoenda chance za wao kukamatwa zinaongezeka so wanamake ridicoulous move then they end up dead!
   
 13. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ukiwa polisi kwenye doria ukapata habari kuna ujambazi unatendeka, na ukifika kwenye tukio unakutana na watu wenye bunduki wanapambana na wewe, unahitaji uhakika gani tena kuwa hawa ni majambazi? Au benki inavamiwa majambazi wanaonekana kabisa wakirusha risasi hovyo kusambaratisha watu, unataka polisi watafute uhakika gani kwenye hali kama hii? Jambazi yuko mbele yako na SMG mtutu unatema kama mvua unataka polisi akamkamate, atamkamataje? Unacheza wewe! Jambazi auawe tu, hakuna kubembelezana. Watu wenye mawazo kama haya ya kwako mi nawaona mdebwedo tu.
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,596
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  This question is not easy as other people think.

  No one is safe! I repeat kama hamjui polisi wanatakiwa kufanya nini msishabikie haya mambo. better know what polisi are supposed to be

  unaweza kuzushiwa mwizi any time, unaweza ukapaki gari mtu akatilia mashaka na kuita polisi. hivi mnawajua polisi wanavyofanya kazi

  I hate majambazi, lakini kuna sababu ya polisi kuji-equip their solution iswe kuua tu. some of them are innocent!

  majamabazi wanaweza kumteka tax driver wakavamia sehemu polisi wanavyokuja tax driver naye anauawa!

  wanachojitetea wao ni kuwa zana hafifu za kazi!

  naona kuna majibu mapesi hapa kwa swali gumu
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  nadhani ni mambo ya timing ..
  Tukio lililopita tuliona police mmoja aliumizwa vibaya kichwa chake na ilisadikika imeingia zaidi kwenye ubongo
   
 16. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Naomba niongeze kidogo hapo. Kila mara utasikia makamanda kuwa 'Polisi walikuwa wakiwafuatilia majambazi na majambazi walipojua kuwa wanafuatiliwa walianza kutupa risasi na polisi wakajibu na katika mapambano hayo majambazi deshi deshi waliuawa"

  /tujiulize, taarifa hii tumeishaisikia mara ngapi?

  /inawezekana 'sinema' hii iwe inajirudia vile vile kila mara idadi kubwa ya majambazi inapouawa?

  /ile kanuni ya askari kumpiga risasi mhalifu miguuni imeishia wapi?

  /ina maana kuwa majambazi wetu sasa ni majasiri sana kiasi kwamba kila wanapogundua wanafuatiliwa na Polisi wanaamua kuanzisha mapambano ya risasi badala ya kutimua mbio na kuwaachia askari kazi ya kuwafukuza na kuwakamata kama ilivyokuwa zamani?

  /katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita zaidi ya majambazi 25 wameawa kwa staili hii hii ya "walipogundua wanafuatwa na Polisi waliamua kuwatupia risasi Polisi ambao nao walijibu mapigo na katika mapambano hayo Polisi walifaulu kuua majambazi deshi deshi"

  Hawa wanaouawa sio Viumbe wa ajabu waliotoka sayari ya Mars ama Pluto kuja kufanya uhalifu Tanzania. Ni ndugu zetu, jamaa zetu, marafiki zetu, wadogo zetu, waume wa watu, wababa wa watoto na kadhalika. Tunapaswa kujiuliza na kutafuta dawa ya kuzuia wao kupinda kushoto wakati jamii nzima inawenda kulia. Kamwe kutupiana risasi hakuwezi kuwa jawabu. Ni sawa na wale wanaosema adhabu ya mtu aliyeuwa ni kunyongwa.

  Nakuunga mkono Waberoya. Tuumize vichwa vyetu kujiuliza badala ya kutafuta majibu mepesi kwa maswali mazito.
   
 17. Shagiguku

  Shagiguku JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 400
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  wakati mwingine majambazi nayo huwaga yanawaoteaga mapolisi...!
  experience from songea , mwanza, ukerewe nk
   
 18. B

  Bumbwini Member

  #18
  Jan 20, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nyie wote mnaowalaumu polisi kwa kuua majambazi mimi nashindwa kuwaelewa kabisa,au nyie mnaona raha mijambazi inavyoua watu kikatili bila hata huruma ukerewe yamefanyika mauaji ya kutisha na kila siku raia wema wasio na hatia wanauawa na mijambazi nyie mnaona raha,nahisi hamjawahi kukutana na ukatili wa majambazi na iko siku mungu atawapambanisha na majambazi ndio mtajua kama muwatetee au vinginevyo,hawa washenzi ni wakatili sana hongera saaaaaaaana jeshi la polisi mkilipata jambazi na mkadhibitisha kama ni jambazi hata kama mmelikamata likiwa hai pigeni risasi uwa kabisa washenzi hawa wasio na hata chembe ya ubinadamu,ila polisi wawe makini wasiingize ubinafsi na chuki katika mapambano haya,bravo jeshi la polis ueni kila jambazi mnalopambana nalo mkithibitisha kama ni jambazi fumua kichwa washenzi hawa wanataka kuifanya nchi hii kama haina serikali.
   
 19. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hivi kuua ni rahisi kuzungumzia?tunazidi kudidimia kwenye unyama wa porini ama tunastaarabika?tukiruhusu jambazi liuwawe tunajenga precedence ya ajabu kuwa mtu akifumaniwa na mume/mke wa mtu atalambwa risasi mtaambiwa alirushiana risasi na polisi.land valuer wa arusha manispaa aliuliwa akisingiziwa jambazi huko moshi kwenye bar ya kwa rozi k.i.a. 2003/2004 ninyi acheni tu polisi ni wezi na wezi ni polisi na wanafahamiana vilivyo-this is a dark continent wajameni.take care of zombe and others
   
 20. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Mkuu, ndio maana tukasema tusitafute majibu mepesi kwa maswali mazito. Hakuna sentensi yoyote inayowalaumu Polisi kwa kuua Majambazi, lakini tunapaswa kuumiza vichwa kujiuliza kwamba je, hii ndio dawa??

  Wewe unasema kuwa tusubiri siku tuingiliwe na majambazi ndipo tutakapojua uchungu wa Kuwatetea lakini Ongeza pia na kwamba na wewe subiri siku ndugu yako anapita mahali na katika kelele za mwizi! Mwizi! akakosewa na kutwangwa risasi ya kichwa kwa makosa!

  Lakini pia tujiulize, mbona ujasiri huu wa kuwatwanga risasi za vichwa unakuja kwa majambazi ambayo mengine yanashukiwa tu na kuuawa hata kabla ya kufanya ujambazi wenyewe lakini Ujasiri huu hauonekani kwenye kuyatwanga risasi mijambazi iliyokubugu ambayo inaiba mabilioni na ambayo kila siku ushahidi wa Ujambazi wao unaanikwa sehemu kadhaa ikiwemo humu JF lakini hakuna anayechukua hatua bali kusuburi mwizi wa Kuku na kuondolea hasira zake hapo??

  Tusitafute majibu mepesi kwa maswali magumu.
   
Loading...