Polisi: Tunachunguza sakata la Dada yake Polepole

Polisi: Tunachunguza sakata la Dada yake Polepole

Lkn kwanini mtu uishi peke ako tena mtu mzima wa 52yrs ukija kuumwa ghafla umo ndani nani atakusaidia?

Ishini na familia zenu ndugu
 
Polisi wanajichunguza!
Upuuzi mtupu.
Nilimpuuza huyu RPC tangu siku ile aliposema uongo kuwa wale viongozi wa Chadema waliotekwa pale Mahakama ya Kisutu kuwa waliofanya utekaji ule ni vibaka ilhali wote tuliona kuwa waliofanya hivyo ni askari polisi tena wakiwa wamevaa sare rasmi za jeshi hilo na wakitumia magari ya jeshi hilo kuwasomba viongozi hao na kwenda kuwatupa kwenye mapori mbali mbali pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.
 
Huyu angenyamaza tu
Anazidi kujidhalilisha

Ova
 
"Haloo ilipigwa simu moja tu... Kama hamtomrudisha naweka yote hadharani mliyoyafanya 2021.. " haya ni baadh ya vionjo vya riwaya ya "jasusi" itafute...
Itumike hii kuwalazimisha wawarudshe na wengine🤣🤣🤣
 
Polepole alitishia kukinukisha... Lazima wamuachie lilikua suala la muda tu, mtu kama yule anauelewa mfumo deep inside, muda huu nadhani anapigiwa simu na wakubwa kumuomba radhi..
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Wangejutaaaaa
 
Wapewe msaada,kwasababu matukio yamekua mengi sana,ambayo wanasema wanachunguza.
 
Nilimpuuza huyu RPC tangu siku ile aliposema uongo kuwa wale viongozi wa Chadema waliotekwa pale Mahakama ya Kisutu kuwa waliofanya utekaji ule ni vibaka ilhali wote tuliona kuwa waliofanya hivyo ni askari polisi tena wakiwa wamevaa sare rasmi za jeshi hilo na wakitumia magari ya jeshi hilo kuwasomba viongozi hao na kwenda kuwatupa kwenye mapori mbali mbali pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.
Alisema ukweli.....ni vibaka....waliovaa sare za polc....na ndo.hao.hao bas wanavamia nymba za watu na kunyenga watu pia....
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kupokea taarifa za kutekwa na kurejeshwa kwa mwanamke aliyejitambulika kwa jina la Christina Hezroni Polepole Kinyangazi, mwenye umri wa miaka 52, mkazi wa Bahari Beach, mtaa wa Katumba, Kinondoni.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro tukio hilo lilianza kuripotiwa kupitia mitandao ya kijamii mnamo Julai 17, 2025, ambapo mtu aliyejitambulisha kwa jina la Humphrey Polepole alidai kuwa dada yake alichukuliwa na watu wasiojulikana waliovamia nyumba yake kwa kuruka ukuta.

Soma, Pia :Polepole: Watu wameruka Nyumbani kwa Dada yangu Bahari Beach, wadai wamefuata taarifa

“Dada huyo alifika katika kituo cha Polisi Kawe na kutoa taarifa zinazohusiana na yeye kuchukuliwa na watu ambao hakuwafahamu na baadae walimrudisha nyumbani kwake jana hiyohiyo”, ameeleza Muliro.

Jeshi hilo limethibitisha kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo kwa kushirikiana na wananchi pamoja na vyombo vingine vya usalama, huku likitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati taratibu za uchunguzi zikiendelea.
Mpaka leo waliomshambulia tundu lisu hawajakamatwa bado polisi inachunguza
Wapo wapi wauaji wa mzee kibao? Bado polisi inachunguza na mafwele yupo ofsini anabugia karanga
 
Lkn kwanini mtu uishi peke ako tena mtu mzima wa 52yrs ukija kuumwa ghafla umo ndani nani atakusaidia?

Ishini na familia zenu ndugu
Anaishi na Yesu,hana haja ya kumtegemea binadamu🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom