Polisi ripoti ya uongo mnatupa, za ukweli mbona hamtupi?

Polisi ripoti ya uongo mnatupa, za ukweli mbona hamtupi?

tikatika

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2011
Posts
2,330
Reaction score
4,124
Kumbe Polise wetu wanajua kufanya upelelezi tena kwa haraka. lakini wanajua kupeleleza matukio ya uongo tu!!

Tukio la Nondo kutekwa linalodaiwa kuwa la uongo limewaibua Polisi na kulitolea ufafanuzi. Hongereni kwa kazi nzuri polisi wetu lakini mbona mnabagua?

Mawazo ameuawa peupe ripoti yeke mpaka leo mmefungia kabatini.

Ben Saanane ni mwaka wa pili hata kumwongelea hamtaki naye alikuwa na mawasiliano ya simu kama haya ya Nondo na aliwaambia wanamtishia kumuua ila ripoti yake mmeitupa mnakojua.

Tundu Lissu alitoa tahadhari ya kuwa kwenye hatari na aliwapa na sehemu za kuanzia hata mmoja hamjamkamata pamoja na kupigwa risasi mchana kweupe.

Roma alitekwa, maskini ya Mungu ameishia kuimba tu kawimbo kake kwamba anamjua aliyemteka ila anauliza alitumwa au alijituma?

Ripoti yake hata kuichungulia hamtaki pamoja na ahadi kemu kemu za kutupatia ripoti yake.

Hivyo mnathibitisha nyie hamna uwezo wa kuchunguza matukio ya kutekwa ila ya kujiteka tu maana ya kujiteka hata wiki haijapita mmetoa ripoti. Na kama mnaweza kuchunguza basi mnabagua au mnawalinda waliofanya matukio hayo.

Polisi wetu achani ubaguzi toeni ripoti zote. msiwe mnabagua wa kuchunguza matukio yao.Hata hawa wengine ni watanzania vinginevyo hata hili tukio mtakuwa mmeliandaa toka mwanzo wake mpaka mwisho wake.
 
Kimsingi kuna mambo yanatia sana ukakasi na mashaka katika vyombo vyetu vya usalama wa raia
 
Kimsingi kuna mambo yanatia sana ukakasi na mashaka katika vyombo vyetu vya usalama wa raia

kesho utawasikia polisi haina upendeo. tunafanya kaz kwa misingi ya sheria . huku wanafanya kazi kwa misingi ya kisiasa
 
Aliyetuhumiwa ni nani, na aliyeunda tume ni nani? Ili tuweze kuamini wanachokiongea, ni lazima tulijue hilo.
 
Tuisaidie polisi ktk upelelezi, ukweli wa Nondo umepatikana sababu ya msaada wa watu, ukasaidia uchunguzi wa kisayansi.
Ben saa8 ametekwa taarifa za kwanza za wasemaji wa chama zilikuwa "Kaenda masomoni South Africa", mpaka sasa Ben ni kama hana familia wala ukoo wote kimya, kama wanaojua nini kinachoendelea. Polisi wanasema Shahidi muhimu kupigwa risasi Tundu Lissu ni Dereva wake, anajua gari lililokuwa linawafuatilia tangu viwanja vya Bunge na hata kabla ya hapo. Yamekamatwa magari 8 shahidi muhimu hapatikani na wanaoumizwa kupigwa risasi Tundu Lissu hawaoni umuhimu wa hilo, siku zinaenda. Cha ajabu ametekwa kiongozi wa chama Kinondoni akiwa na mwenzake, ameuwawa, aliyefanikiwa kutoroka mikononi mwa watesi akiwa na marehemu amefichwa, hao Polisi watawezaje kupata ushahidi wa kilichotokea.
Kuna watu wanadhani Polisini watu wanye uwezo wa kutabiri, kuwa uharifu ukitokea wana njozi za kujua lilitokeaje na nani kafanya.
 
Nukuu: "Polisi wetu acheni ubaguzi toeni ripoti zote. msiwe mnabagua wa kuchunguza matukio yao.Hata hawa wengine ni watanzania vinginevyo hata hili tukio mtakuwa mmeliandaa toka mwanzo wake mpaka mwisho wake" Mwisho wa kunukuu
 
Tuisaidie polisi ktk upelelezi, ukweli wa Nondo umepatikana sababu ya msaada wa watu, ukasaidia uchunguzi wa kisayansi.
Ben saa8 ametekwa taarifa za kwanza za wasemaji wa chama zilikuwa "Kaenda masomoni South Africa", mpaka sasa Ben ni kama hana familia wala ukoo wote kimya, kama wanaojua nini kinachoendelea. Polisi wanasema Shahidi muhimu kupigwa risasi Tundu Lissu ni Dereva wake, anajua gari lililokuwa linawafuatilia tangu viwanja vya Bunge na hata kabla ya hapo. Yamekamatwa magari 8 shahidi muhimu hapatikani na wanaoumizwa kupigwa risasi Tundu Lissu hawaoni umuhimu wa hilo, siku zinaenda. Cha ajabu ametekwa kiongozi wa chama Kinondoni akiwa na mwenzake, ameuwawa, aliyefanikiwa kutoroka mikononi mwa watesi akiwa na marehemu amefichwa, hao Polisi watawezaje kupata ushahidi wa kilichotokea.
Kuna watu wanadhani Polisini watu wanye uwezo wa kutabiri, kuwa uharifu ukitokea wana njozi za kujua lilitokeaje na nani kafanya.

je tundu Lissu angekua amekufa pamoja na dereva upelelezi haufanyiki??

ben saa nane alitoa namba zinazo mtishia hakuna hata aliye kamatwa.

roma yupo ripoti yake iko wap??

mjomba hawa watu huwez kuwabeba hata na mbeleko ya chuma
 
Tatizo vyeti fake Polisi havikukaguliwa hayo ndo madhara yake ya uchunguzi wa kisayansi. Embu toeni vyeti fake na huko kama kuna mtu atasalimika, wengi ni Bashites.
 
Back
Top Bottom