kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,313
- 12,613
Siku moja nilipokuwa nchi za kigeni nilienda kwenye mgahawa mmoja usiku kwenda kujipunzisha baada ya kazi za mchana kutwa.
Nikiwa napata kinywaji kikali aina ya Magaritha pembeni kwangu kulikuwa na akina dada wawili ambao walikuwa wanaoneka kama walikuwa marafiki sana, lakini kilichonishangaza na kusababisha niwahoji usiku ule ni jinsi walivyotofautiana kwenye vinywaji vyao.
Wote walikuwa wanakula chicken wings kama mimi lakini mmoja wao anakunywa wisky na mwingine soda tu.
Nikawauliza kwanini wanaonekana marafiki lakini wanatofautiana sana aina ya vinywaji vyao, nilidhani labda mmoja ni mgonjwa kwa siku ile.
Jibu walilonipa ni kwamba mwenye zamu ya kuendesha gari leo hanywi kabisa pombe atakunywa kesho wakati na mimi nitakopokuwa na zamu ya kuendesha gari.
Wakanionyesha polisi na kipima pombe kwenye parking ya magari ambaye atampima kila dereva anayetoka pale kama amekunywa pombe amkamate kwa kosa la kunywa na kuendesha gari barabarani.
Niliipenda sana ile, nikaona kumbe hata sisi tunaweza kupunguza ajali kwa njia kama ile kwa polisi kukaa sehemu mbalimbali zenye vileo na parking kubwa za magari ili kukamata na kuwalipisha faini kubwa walevi wanaoendesha magari palepale bar kabla hawajaingia barabarani na kusababisha ajali.