Polisi punguzeni ajali kwa njia hii hapa

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,797
2,000
Siku moja nilipokuwa nchi za kigeni nilienda kwenye mgahawa mmoja usiku kwenda kujipunzisha baada ya kazi za mchana kutwa.

Nikiwa napata kinywaji kikali aina ya Magaritha pembeni kwangu kulikuwa na akina dada wawili ambao walikuwa wanaoneka kama walikuwa marafiki sana, lakini kilichonishangaza na kusababisha niwahoji usiku ule ni jinsi walivyotofautiana kwenye vinywaji vyao.

Wote walikuwa wanakula chicken wings kama mimi lakini mmoja wao anakunywa wisky na mwingine soda tu.

Nikawauliza kwanini wanaonekana marafiki lakini wanatofautiana sana aina ya vinywaji vyao, nilidhani labda mmoja ni mgonjwa kwa siku ile.

Jibu walilonipa ni kwamba mwenye zamu ya kuendesha gari leo hanywi kabisa pombe atakunywa kesho wakati na mimi nitakopokuwa na zamu ya kuendesha gari.

Wakanionyesha polisi na kipima pombe kwenye parking ya magari ambaye atampima kila dereva anayetoka pale kama amekunywa pombe amkamate kwa kosa la kunywa na kuendesha gari barabarani.

Niliipenda sana ile, nikaona kumbe hata sisi tunaweza kupunguza ajali kwa njia kama ile kwa polisi kukaa sehemu mbalimbali zenye vileo na parking kubwa za magari ili kukamata na kuwalipisha faini kubwa walevi wanaoendesha magari palepale bar kabla hawajaingia barabarani na kusababisha ajali.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
34,904
2,000
Wazo zuri, tatizo huku bar ni nyingi sana na wateja wakubwa ni haohao wanaotakiwa kukupima wao ndiyo wanaongoza kwa unywaji.
 
kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,797
2,000
Wazo zuri, tatizo huku bar ni nyingi sana na wateja wakubwa ni haohao wanaotakiwa kukupima wao ndiyo wanaongoza kwa unywaji.
Wakodi madereva au watumie taxi kwenda kunywa badala ya kunywa na kuendesha wenyewe. Bar ni nyingi lakini mabaa makubwa yenye parking kubwa za magari zinafahamika
 
Wanaokupima wao wenyewe ni wanywaji wazuri sana.
 
kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
5,797
2,000
Wanaokupima wao wenyewe ni wanywaji wazuri sana.
Sheria ni msumeno, hakuna anaependa kupata ajali wasaidieni hata hao. Tunafahamu mabaa ni mengi na wanywaji ni wengi lakini mnaweza kuyatembea hata kwa kushtukizia na kuotea
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
34,904
2,000
Sheria ni msumeno, hakuna anaependa kupata ajali wasaidieni hata hao. Tunafahamu mabaa ni mengi na wanywaji ni wengi lakini mnaweza kuyatembea hata kwa kushtukizia na kuotea
Ajali siyo pombe peke yake, mirungi, bangi n.k
 
Hajto

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
3,641
2,000
Tunahitaji sana kujifunza siye watanzania kila kitu,ungetuambia iyo ni inchi gani
 
kidodosi

JF-Expert Member
May 1, 2013
2,041
2,000
Wazo zuri, tatizo huku bar ni nyingi sana na wateja wakubwa ni haohao wanaotakiwa kukupima wao ndiyo wanaongoza kwa unywaji.
Yeah hili zoezi linaweza anzia kwenye night clubs kwanza itasaidia sana kwa kweli maana nimeisha poteza ndg na marafiki zangu na wengine kupata ulemavu.
 
Boniphace Bembele Ng'wita

Verified Member
Dec 25, 2013
2,919
2,000
Siku moja nilipokuwa nchi za kigeni nilienda kwenye mgahawa mmoja usiku kwenda kujipunzisha baada ya kazi za mchana kutwa. Nikiwa napata kinywaji kikali aina ya Magaritha pembeni kwangu kulikuwa na akina dada wawili ambao walikuwa wanaoneka kama walikuwa marafiki sana, lakini kilichonishangaza na kusababisha niwahoji usiku ule ni jinsi walivyotofautiana kwenye vinywaji vyao. Wote walikuwa wanakula chicken wings kama mimi lakini mmoja wao anakunywa wisky na mwingine soda tu. Nikawauliza kwanini wanaonekana marafiki lakini wanatofautiana sana aina ya vinywaji vyao, nilidhani labda mmoja ni mgonjwa kwa siku ile. Jibu walilonipa ni kwamba mwenye zamu ya kuendesha gari leo hanywi kabisa pombe atakunywa kesho wakati na mimi nitakopokuwa na zamu ya kuendesha gari. Wakanionyesha polisi na kipima pombe kwenye parking ya magari ambaye atampima kila dereva anayetoka pale kama amekunywa pombe amkamate kwa kosa la kunywa na kuendesha gari barabarani. Niliipenda sana ile, nikaona kumbe hata sisi tunaweza kupunguza ajali kwa njia kama ile kwa polisi kukaa sehemu mbalimbali zenye vileo na parking kubwa za magari ili kukamata na kuwalipisha faini kubwa walevi wanaoendesha magari palepale bar kabla hawajaingia barabarani na kusababisha ajali.
Mkuu kwa mtazamo wako umewaweka madreva wote wanabwiya? Anyway ni ushauri mzr bt haufai kwa mazingira yetu yote, maana si wote wanaokunywa, (bia) ila ushauri mhim ni huu kutokunywa pombe ni njia bora ya kupunguza ajari, ila kilichobora zaidi, ni kuwa makin barabarani has a mwendo kasi

Na kwa wale madreva Wa masafa matefu, wanapaswa kuwa 2au 3 kutegemeana na umbali, ndiyo maana kwa sasa pia ajari zimepungua...
 
sijakuelewa hapa ulichoandika. Lengo lao ilikuwa kupambana na ajali zinazotokana na madereva wanaokunywa pombe na kutembeza magari barabarani bila kujali wamelewa au la. Tunafahamu kuwa pombe anapunguza umakini kwenye kufikiri na kutenda, hii ni pamoja na kuendesha gari barabarani
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom