Polisi ni mikono salama kweli?

ha ha ha

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
638
84
Wakuu,
Ni utaratibu kuwa mhalifu akibainika anapaswa kufikishwa polisi ili haki iweze kuendeka. Hii pia ni muhimu kwa ajili ya usalama wa mtuhumiwa. Ebu jionee, kweli jeshi linaheshimu haki za binadamu na usalama wa raia wake kama inavyoeleweka. hivi wanaongozwa na sheria ipi? Nani kawapa dhamana ya kupiga watuhumiwa? Nijeshi la taifa huru kweli? mauaji-songea.jpg imagesCA70AYGL.jpg 1023315.jpg imagesCA3FJI4A.jpg imagesCAQ38WVQ.jpg imagesCAHVSUFE.jpg imagesCATJMTFY.jpg polisi tena.jpg untitled.png mauaji-songea.jpg imagesCA70AYGL.jpg 1023315.jpg imagesCA3FJI4A.jpg imagesCAQ38WVQ.jpg imagesCAHVSUFE.jpg imagesCATJMTFY.jpg polisi tena.jpg untitled.png
 
Tuna hasara sana na hawa polisisisiem!

Namwamini Mbwa wangu mlinzi pale nyumbani kuliko hawa majambazi wauaji!
 
Ukitaka kujua polisi wetu hawajui wajibu wao, tazama maandamano ya wananchi wa Ugiriki katika kipindi hiki cha msukosuko wa wa uchumi,waandamanaji wavunja maduka,wanachoma moto majengo na wanapambana na polisi huku wakiwa na chupa walizojaza petrol kwa kuwashambulia polisi kwa moto,lakini pamoja na yote haya hukuti polisi hawabebi silaha za moto katika kuzibiti waandamanaji na kipindiki chote hiki husikii kuuwawa kwa waandamanaji.

Last edited by a moderator:
Polisi wa Tanzania sijui wamelishwa nini, wamekuwa kama si watoto wetu, kaka na dada zetu, wamekuwa kama hawana shida kama walizonazo watanzania wa kawaida wamekuwa kama vichaa kazi ni kuua tu tu tu!!
 
Wakileta fujo kushindana na dola, tandika tu, hakuna kuwawachia, wanatandikwa na bado wansema Serikali "legelege" jee, ukiwawachia, si watakutia vidole (vya macho).
 
umwana asha maana yake nini?

Sister pole kwani humjui Mwanaasha? Mwanaasha ni first student ambaye kwenye matokeo ya juzi ya form iv amepaata bahati ya kutunukiwa ulast student (so she is both first & last student) kwenye shule yake ya Feza Girls. Kwa hiyo mtoa hoja anamaanisha kuwa uwezo mdogo wa kufikiri (kama Mwanaasha mpaka akapata div iv ya 27 points) ndio unafanya polisi wetu wafanye hayo wanayofanya.
 
Wakileta fujo kushindana na dola, tandika tu, hakuna kuwawachia, wanatandikwa na bado wansema Serikali "legelege" jee, ukiwawachia, si watakutia vidole (vya macho).
Mkuu Mi najua kwanini unasema hivyo! Hauko kwa ajili ya Tanzania na Watanzania, Kwako wewe Maslahi yako kwanza na si Taifa. Na watu wa aina yako wako tayari kufanya lolote, hata ikiwa kuchinja watoto wenu ili mradi tu ugange njaa zenu..
 
Wakileta fujo kushindana na dola, tandika tu, hakuna kuwawachia, wanatandikwa na bado wansema Serikali "legelege" jee, ukiwawachia, si watakutia vidole (vya macho).
Unamaanisha nini kusema ukiwaachia? swala ni kuwa hawapaswi kisheria kufanya hivyo! Huu ni ushahidi wa utawala ulio juu ya sheria na ukiukwaji wa haki za binadamu. Jiulize, wanafanya kwa faida ya nani?Kweli roboti roboti tu.
 
Wakileta fujo kushindana na dola, tandika tu, hakuna kuwawachia, wanatandikwa na bado wansema Serikali "legelege" jee, ukiwawachia, si watakutia vidole (vya macho).
we kweli mvuta bangi na imeshafikia hatua ya kukuharibu kichwa, MKUU I AM PRAYING FOR U! SI KOSA LAKO.
 
attachment.php
attachment.php
attachment.php

Hivi Tanzania ni nchi ya amani kweli? Hawa polisi inaonekana wanfurahia kutoa kipigo kwa raia wasiokuwa na makosa. Kwa nini polisi achukue sheria mikononi mwake au na sisi tuwageuke? Huyo anyesaidiwa na trafick kavaa kabisa na vest ya kuzuia risasi isipenye, hiyo si dalili ya woga?
Polisi mnawapiga raia wasiokuwa na hatia lakini mnashindwa kwenda kuwakamata wei wanaojulikana wa raslimali za taifa, ole wenu siku kibao kitapobadilika mtajuta na kusaga meno. Ndo maana taaluma yenu mkistaafu hamna chochote mnachoweza kufanya, akili yenu inakuwa imedumaa kabisa.
 
Polisi wapo kwa ajili ya kutekeleza matakwa ya chama. kwa hiyo ili kupambana nao lazima tujitahidi tufanye kama nchi za afrika kaskazini.
 
Polisi wa Tanzania sijui wamelishwa nini, wamekuwa kama si watoto wetu, kaka na dada zetu, wamekuwa kama hawana shida kama walizonazo watanzania wa kawaida wamekuwa kama vichaa kazi ni kuua tu tu tu!!

Hawajalishwa chochote Mkuu! Njaa na stress za mazingira magumu ya kazi, posho kiduchu nk ndo zimewapeleka hapa. Wanapenda sana vurugu zikiibuka popote na wao kwenda "kutuliza" pale huwa ndo sehemu yao kujipatia chochote kupitia uporaji wanaoufanya kwa wahanga. wao wanaita 'KUTOA VITU VYA HATARI" wanakupekua na kuchukua ulichonacho kupitia "upekuzi" huo
 
Back
Top Bottom