GE2025 Polisi na wanajeshi wapinga tizi zito Kinondoni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Mkoa huo umefanya mazoezi ya pamoja Oktoba 3, 2025.

Mazoezi hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Jeshi la Wananchi Mwenge – Kikosi cha Bendi, yalihusisha matembezi mafupi (route match) pamoja na mazoezi mbalimbali ya mwili kwa lengo la kuimarisha afya, mshikamano na utayari wa askari katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Soma: Mkoa wa Kipolisi Kinondoni wafanya mazoezi ya pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama

Viongozi wa Jeshi hilo wamesema kuwa mazoezi ya aina hiyo yataendelea kufanyika mara kwa mara ili kuongeza mshikamani na ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na usalama katika Mkoa wa Kinondoni.

Mgunda yupo kwa maslah ya nani haswa?
 
Mikwara ni mingi sana sikuhizi kuelekea tarehe 29 siku ya uchafuzi, ngoja tuone mikwara yao itaishia wapi.
 
Watahangaika sana, maandamano maana yake halisi ni kutokupiga kura..
 
Ninapoona wanajeshi nao wamo katika huu upuuzi ndo nazidi kuamini hawana tofauti na polisi. Wote ni failures tu.
 
Wanataka wananchi wajitokeze kupiga kura halafu wanafanya mazoezi yenye kutia hofu. Sasa hapa kuna mwananchi atajitokeza kupiga kura? Si atadhaniwa ni muandamanaji na kushughulikiwa huko vituoni?
 
Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Mkoa huo umefanya mazoezi ya pamoja Oktoba 3, 2025.

Mazoezi hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Jeshi la Wananchi Mwenge – Kikosi cha Bendi, yalihusisha matembezi mafupi (route match) pamoja na mazoezi mbalimbali ya mwili kwa lengo la kuimarisha afya, mshikamano na utayari wa askari katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Soma: Mkoa wa Kipolisi Kinondoni wafanya mazoezi ya pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama

Viongozi wa Jeshi hilo wamesema kuwa mazoezi ya aina hiyo yataendelea kufanyika mara kwa mara ili kuongeza mshikamani na ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na usalama katika Mkoa wa Kinondoni.

Ninapoona wanajeshi nao wamo katika huu upuuzi ndo nazidi kuamini hawana tofauti na polisi. Wote ni failures tu.

..sasa subiri kutokee tatizo, mfano ajali, uone kama watafika kwa wakati, na kama watafanya kazi kwa ushirikiano.
 
Back
Top Bottom