Polisi na "Bangi" Polisi na "Fuvu" la binadamu! Bomu inashindikana nini??

sokoinei

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,832
566
Baada ya tukio la bomu lililolipuka ktk mkutano wa CDM Soweto Arusha na kuuwa watu 4 huku zaidi ya 70 wakijeruhiwa,kumekuwepo na mabishano ya hapa na pale kati ya jeshi la polisi kwa upande mmoja na Cdm kwa upande wa pili.
Huku CDM wakilihusisha jeshi la polisi kuhusika na tukio zima,polisi nao wamekuwa wakijaribu kujinasua kutoka ktk tuhuma hizi nzito bila kujuwa kwamba CDM kwa upande wao wamejipanga na wanachozungumza wanao ushahidi na wala hawabahatishi!

Wakati wa mauaji ya Mwangosi mwaandishi wa habari wa channel 10,polisi wakiongozwa na kamanda wa operesheni maalum Paul Chagonja walisema kuwa Mwangosi aliuwawa na kitu kilichorushwa kutoka kwa Wafuasi wa Cdm wakati haikuwa kweli! Lakini baadae ilithibitika kuwa Mwangosi aliuwawa na Polisi kwa kumlipuwa na Bomu.

Leo kinachobishaniwa kwa bomu la Arusha kati ya CDM na Jeshi la polisi haina tofauti na kilichompata marehemu Mwangosi.
Cha kujiuliza ni kuwa kama Askari polisi alikamatwa akiwa na Fuvu la binadamu wakitaka kumbambikizia raia itawashinda nini kuwa na Bomu na kurusha kwenye mkutano wa CDM?
Kama polisi wanakamatwa na magunia zaidi ya 10 za bangi je ni lipi lisilowezekana kufanywa na hawa polisiccm?

Cdm wanadai wana video inayomuonyesha alierusha bomu kuwa ni polisi..... Mwigulu anadai huyo ni mtu alievalishwa nguo za polisi. Lakini binafsi nilikuwa uwanjani siku ya tukio cha kujiuliza ni kama alierusha Bomu hakuwa polisi,ni kwanini basi mara baada tu ya mlipuko kutokea,...Polisi walianza kurusha risasi na mabomu ya machozi?
Watu wengi waliojeruhiwa ktk tukio hilo walipigwa risasi na Polisi wakati wakikimbia kujiokoa.

Polisi wetu wanafanya kazi kimazoea na Kisiasa zaidi ndio maana baadhi ya watu humuita CHAGONJA katibu Mwenezi wa CCM! Chagonja alipokuja Arusha baada ya mlipuko huo hakufanya kazi ya uchunguzi bali alikuja na kuanza kumuandama mwenyekiti wa taifa CDM FREEMAN MBOWE,kwa kutaka kumlazimisha kutoa anachodai kuwa video ya tukio zima huku akijisahau kwamba Mbowe ni Muhanga wa tukio hilo na kuwa hana imani na yeye(Chagonja) kwa tabia yake ya kutaka kupotosha UMMA juu kifo cha Mwangosi.

Ikiwa polisi wanashiriki Kusafirisha bangi,kubeba Fuvu la binadamu,Kukamatwa na Meno ya Tembo nk, inashindikana nini polisi hao hao kutumika kuvurugakutano wa CDM kwa maslahi ya CCM? Polisi ni Pinda kabisa!!
 
Back
Top Bottom