Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Iimewakamata na kuwatia mbaroni watuhumiwa 12 wanaodaiwa kuwa wahalifu, wakiwa wamejificha kwenye mapango yaliyomo Mkoani humo, huku wakidaiwa kuwa na vifurushi vya bangi.
Akizungumza wakati wa doria hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, amesema operesheni hiyo ilianza rasmi Novemba 29, 2025, ikihusisha maeneo ya Kata za Mkolani, Buhongwa, Isamilo, Mhandu, Igoma Kati na Mahina Wilaya ya Nyamagana pamoja na Kitangili, Bwiru Ziwani, Kawekamo na Ibungilo, Wilaya ya Ilemela.
Kamanda Mutafungwa amesema Jeshi la Polisi Mkoani humo limeendesha operesheni maalumu ya msako na doria katika maeneo ya milima na mapango yanayotajwa kuwa maficho ya wahalifu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutokomeza uhalifu Mkoani humo.
“Tumekuwa tukipokea taarifa kutoka kwa Wananchi kuhusu wahalifu wanaojificha katika mapango na maeneo ya milimani wakijiandaa kutekeleza matukio ya uhalifu, hasa kuelekea mwishoni mwa mwaka. Hii imetulazimu kuchukua hatua za haraka,” amesema Kamanda Mutafungwa