Polisi Makete waua mteja wa benki

Polisi Makete waua mteja wa benki

mh ... bahati mbaya ikaingia kifuani... hawa wauaji....
 
Habari hiyo ya mtu mmoja kupigwa risasi wilayani Makete ni za kweli kabisa na walasi tetesi. Mazingira ya kupigwa shaba mtu huyo mpaka saizi ni kitendawili na askari aliyefanya tukio hilo tayari yupo lockup.

Nadhani Jeshi la Polisi lipo katika uchunguzi wa ndani juu ya tukio hilo ilikuwaje kuwaje mpaka askari wake akatumia bunduki??
 
Ni aibu kukosea kulenga miguu mpaka kufikia kifua....wakikosea na kumlenga prezidaa siku moja ndo ntawaona wanashabaha sana...pumbafu sana polis ya tanzania
 
waliuwa,wafanyabiashara wakaja wa maandamano,wakauwa mwandishi wa habari,sasa mwalimu...!tunaanza kuzoea taratibu,kikinuka nchi hii kuna watu watajibeba!
 
Vyombo vya habari tafadhali fuatilieni skendo hii, msiiache ipite marehemu huyu na mwangosi wote walikuwa wanaelimisha taifa kwa namna tofauti. Plz saidieni kuisemea familia ya marehemu ili muuaji huyu dhalimu afikishwe mahakaman ili haki itendeke. RIP mwalimu.
 
Vile vipolisi vya makete vinajidai sana. Inabidi kuhamishia vijana wa ivalalila pale mjini maana wao ndo wanajuaga nini cha kuwafanya polisi. Nakumbuka kipindi kile jamaa walikuwa wakitia tu mguu kijiji kile wanapewa kichapo! Haiwezekani! Polisi wanatumia kodi zetu kutuua, kutuibia yaani ni balaa tupu. Badala ya usalama wa raia imeguka uhasama wa raia
 
Duh!!Tunadunguliwa kama swala na rais kuuuuutwaaa kucheka cheka....kazi ipo jaman.
 
Jose n mpumbav kwa tunao mjua anapenda sana sifa kwanza n chapombe sasa ngoja sheria ichukue mkondo wake
 
IMG_1985.JPG

WAKATI mtuhumiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa kituo cha runinga cha Chanel Ten mkoani Iringa Daudi Mwangosi Daudi Mwangos, askari wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) akitarajiwa kufikishwa tena mahakamani leo kwa kesi hiyo kutajwa ,askari wilaya ya Makete mkoa wa Njombe wadaiwa kufanya mauwaji ya kinyama kwa kumpiga mteja wa benki ya NMB kwa risasi .

Huku askari askari mmoja nayetuhumiwa kufanya unyama huo aliyetambulika kwa jina moja la Jose akishikiliwa na jeshi la polisi kufuatia mauwaji hayo ya kinyama.

Tukio hilo limekuja huku bado watanzania hasa wakazi wa mikoa ya Iringa na Njombe wakiwa bado hawajasahau mauwaji ya kinyama yaliyomkuta mwanahabari Daudi Mwangosi ambapo kesi hiyo bado ikiendelea kutajwa na wanahabari waliokuwepo eneo la tukio siku ya mauwaji wakisubiri kuchukuliwa maelezo yao kama mashahidi wa kesi hiyo pindi itakapoanzwa kusikilizwa.

Mwandishi wa wetu kutoka Makete Njombe anaeleza kuwa tukio hilo wamedai kuwa mauwaji hayo ya kinyama yametokea jana jumatano majira ya saa 1.20 usiku baada ya mteja huyo aliyekuwa na usafiri wa boda boda kufika eneo hilo la benki kwa lengo la kuchukua fedha .

Imedaiwa kuwa aliyepigwa risasi anatambuliwa kwa jina la Casto Kawambwa mkazi Mbalizi mkoani Mbeya na kuwa baada ya kupigwa risasi alikimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Makete ambako inadaiwa kabla ya kupatiwa matibabu amefariki dunia .

Kutokana na tukio hilo jeshi la polisi liliwazuia wanahabari kutimiza wajibu wao kwa kupiga picha wala kusogea eneo hilo la Hospitali na badala yake kuweka ulinzi mkali eneo hilo la Hospitali ili kuzuia wanahabari kusogea eneo hilo .

Hata hivyo mmoja kati ya askari ambae jina lake halikufahamika mara moja alisikika akidai kuwa chanzo cha mteja huyo wa benki kupigwa risasi alikuwa akihisiwa kuwa ni jambazi na hivyo baada ya kufika eneo hilo kwa usafiri wake wa piki piki (boda boda ) walihisi kuwa amefika kwa ajili ya kufanya vitendo vya uporaji katika benki hiyo na hivyo askari katika hali ya kujihamia aliamua kumpiga risasi.

Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi wa mkoa wa Njombe ili kuzungumzia undani wa tukio hilo linafanyika na mtandao huu .

CHANZO: Blog ya Francis Godwin

Inasemekana ni mwalimu alie uawa, ni kweli? Ama huyu ni wa pili kuuliwa na polis kwa leo?
Tujuze tafadhar.
 
Jamani mimi mwenyewe majuzi Morogoro, nimekuta askari kalala fofofo CRDB na bunduki milikuwa sentimita chache toka kwenye mikono yake. Ningekuwa jambazi ningesepa nayo. Kwa kuwa network haikuwepo, nikaamua kumwamsha ili nimuulize ni kwa muda gani ATM haifanyi kazi. Alikurupuka kwa kasi ya ajabu, akakamata bunduki na kunilenga. Nikacheka, "afande ulikuwa umelala" akakana kwa sauti kubwa, "sijalala". Ni mbinu za maongezi ya kisaikolojia ndiyo yaliokoa maisha yangu. Na pia kwa sababu nilimwamsha nikiwa mbali naye. Hawa sungusungu wanavaa kaki badala ya manyoya.............
 
IMG_0016.JPG
IMG_0027.JPG

Mwalimu mmoja wa shule ya sekondari kitulo wilayani makete aliyefahamika kwa jina la casto sote kawamba ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi Makete

Akizungumza na mtandao huu wawww.francisgodwin.blogspot.com mkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza kuhusu tukio hilo lililotokea eneo la benki ya NMB tawi la Makete jana majira ya saa moja na robo alisema kuwa mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenki kupitia mashine ya kutolea pesa ya ATM akiwa na pikipiki ndipo alipo uwawa na askari mmoja aitwae Jose Msukuma na kukutwa na umauti huo .

Inadaiwa kuwa kisa cha mauwaji yake ni madai kutovaa kofia hiyo na baada ya kuitwa na askari hao alikaidi amri na kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa lindo.

Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Idd Nganya ambaye ndie mwajiri wa marehemu amesema kuwa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya makete wakati utaratibu wakusafirisha mwili huo kwenda kwao mbeya kwa ajili ya mazishi ukiendelea

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye jina lake limehifadhiwa amesema kuwa askari hao walikuwa wakiomba fedha kwa mwalimu huyo na baada ya kukataliwa ndipo walipo anza kumshushia kichapo na alipo wazidi walilazimka kutumi asilaha na kumpiga begani kwa risasi

Walimu wenzake na marehemu ambao walifika hospitali kujua kuhusina na kifo cha mwalimu mwenzake wameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kulifananisha na tukio la kikatili machoni pao.

Mganga mkuu mfawidhi ambaye ni msemaji wa hospitali ya wilaya ya makete Dr Michael Gulaka amesema kuwa wao walipokea mwili wa marehemu na sio majeruhi.

IMG_1985.JPG
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD]Askari wa FFU mkoani Iringa wakimwadhibu kwa kipigo
aliyekuwa mwandishi wa Chanel Ten mkoa wa Iringa
marehemu Daudi Mwangosi (wa pili kushoto) kabla ya
kuuwawa kwa bomu septemba 2 mwaka 2012 katika
kijiji cha Nyololo Mufindi.(picha na maktaba ya mtandao huu)
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
.....................................................................................................................................................................
WAKATI mtuhumiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa kituo cha runinga cha Chanel Ten mkoani Iringa Daudi Mwangosi Daudi Mwangos, askari wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) akitarajiwa kufikishwa tena mahakamani leo kwa kesi hiyo kutajwa ,askari wilaya ya Makete mkoa wa Njombe wadaiwa kufanya mauwaji ya kinyama kwa kumpiga mteja wa benki ya NMB kwa risasi. Huku askari askari mmoja nayetuhumiwa kufanya unyama huo akishikiliwa na jeshi la polisi kufuatia mauwaji hayo ya kinyama.

Tukio hilo limekuja huku bado watanzania hasa wakazi wa mikoa ya Iringa na Njombe wakiwa bado hawajasahau mauwaji ya kinyama yaliyomkuta mwanahabari Daudi Mwangosi ambapo kesi hiyo bado ikiendelea kutajwa na wanahabari waliokuwepo eneo la tukio siku ya mauwaji wakisubiri kuchukuliwa maelezo yao kama mashahidi wa kesi hiyo pindi itakapoanzwa kusikilizwa.

Mwandishi wa wetu wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Makete Njombe anaeleza kuwa tukio hilo wamedai kuwa mauwaji hayo ya kinyama yametokea jana jumatano majira ya saa 1.20 usiku baada ya mteja huyo aliyekuwa na usafiri wa boda boda kufika eneo hilo la benki kwa lengo la kuchukua fedha .

Imedaiwa kuwa aliyepigwa risasi anatambuliwa kwa jina la Casto Kawambwa mkazi Mbalizi mkoani Mbeya na kuwa baada ya kupigwa risasi alikimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Makete ambako inadaiwa kabla ya kupatiwa matibabu amefariki dunia .

Kutokana na tukio hilo jeshi la polisi liliwazuia wanahabari kutimiza wajibu wao kwa kupiga picha wala kusogea eneo hilo la Hospitali na badala yake kuweka ulinzi mkali eneo hilo la Hospitali ili kuzuia wanahabari kusogea eneo hilo .

Hata hivyo mmoja kati ya askari ambae jina lake halikufahamika mara moja alisikika akidai kuwa chanzo cha mteja huyo wa benki kupigwa risasi alikuwa akihisiwa kuwa ni jambazi na hivyo baada ya kufika eneo hilo kwa usafiri wake wa piki piki (boda boda ) walihisi kuwa amefika kwa ajili ya kufanya vitendo vya uporaji katika benki hiyo na hivyo askari katika hali ya kujihamia aliamua kumpiga risasi .

Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi wa mkoa wa Njombe ili kuzungumzia undani wa tukio hilo linafanyika na mtandao huu.

Hisani ya Mzee wa Matukio daima

Huyu pia amaeuliwa na "kitu chenye ncha kali"?

Maisha ya mdanganyika yamekuwa "lahisi" sana kuyapoteza.

Amani na utulivu ndio sifa ya Tanzania.

Tume itakayoundwa kuchunguza tukio hili, itatoa ripoti kuwa aliyeuawa na Polisi alikuwa ni jambazi.

Wadanganyika ,tumeyazoea haya...ze comedy husema "maisha bora kwa kila mdanganyika,yanawezekana". Sasa hii kauli mbiu imekuwa...kuwapeleka kuzimu wadanganyika ni jukumu la walinda usalama na amani.

Nani kama polisi ya Tanzania?
 
Kauawa na polisi akitoka kuchukua pesa atm nmb makete juzi;

Mod unaweza kurekebisha ili zionekane vizuri zaidi
attachment.php

attachment.php

attachment.php

=========UPdates============

Mwalimu mmoja wa shule ya sekondari kitulo wilayani makete aliyefahamika kwa jina la casto sote kawamba ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi Makete

Akizungumza na mtandao huu, mkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza kuhusu tukio hilo lililotokea eneo la benki ya NMB tawi la Makete jana majira ya saa moja na robo alisema kuwa mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenki kupitia mashine ya kutolea pesa ya ATM akiwa na pikipiki ndipo alipo amuliwa na askari mmoja aitwae Jose Msukuma na kukutwa na umauti huo .

Inadaiwa kuwa kisa cha mauwaji yake ni madai kutovaa kofia hiyo na baada ya kuitwa na askari hao alikaidi amri na kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa lindo.

Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Idd Nganya ambaye ndie mwajiri wa marehemu amesema kuwa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya makete wakati utaratibu wakusafirisha mwili huo kwenda kwao mbeya kwa ajili ya mazishi ukiendelea

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye jina lake limehifadhiwa amesema kuwa askari hao walikuwa wakiomba fedha kwa mwalimu huyo na baada ya kukataliwa ndipo walipo anza kumshushia kichapo na alipo wazidi walilazimka kutumi asilaha na kumpiga begani kwa risasi

Walimu wenzake na marehemu ambao walifika hospitali kujua kuhusina na kifo cha mwalimu mwenzake wameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kulifananisha na tukio la kikatili machoni pao.

Source: francisgodwin.blogspot.com
 
Attachments

  • IMG_0027.JPG
    IMG_0027.JPG
    10.7 KB · Views: 1,669
  • IMG_0028.JPG
    IMG_0028.JPG
    10.8 KB · Views: 186
Hebu tuelezee vizuri basi na sisi tusioijua hii story, ilikuwaje mpaka polisi wakampiga risasi?.
 
Ilikuwaje jamani!! au walimchukulia fedha yake? Jamani jamani huu ni unyama kabisa
 
Back
Top Bottom